Katibu Mkuu wa Wizara ya Maliasili na Utalii, Meja Jenerali Gaudence Milanzi amewataka watumishi wa wizara hiyo kufanyakazi kwa weledi ili kuogeza tija kwa Taifa.
Katibu
mkuu huyo ametoa rai hiyo leo, Septemba 25, 2018 alipokuwa akiwaaga
watumishi wa wizara baada ya kustaafu jeshini na kwa mujibu wa sheria
tangu Septemba 16.
Milanzi
amesema kwa muda wote aliitumikia wizara hiyo alipata ushirikiano wa
kutosha uliomuwezesha kuiongoza vyema wizara hiyo na kuchangia mafanikio
yaliyojidhihirisha kwenye sekta za wanyamapori, utalii, misitu na nyuki
na malikale.
Katika kipindi cha uongozi wake wizarani hapo, amesema wizara imepata mafanikio katika vita dhidi ya ujangili.
“Tumekamilisha
mambo mengi. Kila mmoja wenu alikuwa akinisaidia ili wizara isonge
mbele. Hakuna aliyetaka kunikwamisha. Ninawashukuru sana,” amesema
Milanzi.
Akizungumza
kwenye hafla fupi ya kumuaga Milanzi iliyofanyika ukumbi wa mikutano wa
Chuo Kikuu cha Dodoma, kaimu katibu mkuu wa wizara hiyo, Dk Aloyce
Nzuki amempongeza kwa utumishi wake.
“Umeweka
mifumo mizuri na kubuni mikakati na mbinu za kutatua changamoto
zilizokuwa zinaikabili wizara na kuhakikisha watumishi wanapata utulivu
wa akili kwa kujali maslahi yao. Uliwawezesha kufanya kazi wakiwa
watulivu wa akili jambo liliongeza ufanisi kazini,” ameeleza Dk Nzuki.
Milanzi aliteuliwa kuwa katibu mkuu wa wizara hiyo Disemba 2015.
“Nashukuru
nimestaafu salama. Wizara hii ni muhimu sana kwa maendeleo ya nchi na
inagusa masilahi ya wengi. Jukumu nililopewa lilikuwa kusimamia maslahi
ya nchi, naamini kuna masilahi ya watu yalivurugwa hivyo mimi kuwa mwiba
kwao,” amesema akiaga kamanda huyo wa Jeshi la Wananchi (JWTZ).
No comments:
Post a Comment