VIONGOZI WA SUNGUSUNGU KATA YA NYANDEKWA KAHAMA WAPIGA MARUFUKU MIFUGO KUSAFIRI USIKU

Image result for PICHA ZA ASKARI WA SUNGUSUNGU
Na William Bundala
KAHAMA.

Uongozi wa Sungusungu katika kata ya NYANDEKWA Wilayani KAHAMA Mkoani SHINYANGA umepiga marufuku watu wanaosafirisha mifugo usiku kupita katika eneo hilo,ikiwa ni pamoja na madereva boda boda wanaosomba watu na mizigo usiku kutofanya shughuli hizo.

Wito huo umetolewa na Mtemi wa Kata wa Sungusungu katika kata hiyo KABHILO MACHIBYA katika mkutano wa kata wa sungusungu uliofanyika katika viwanja vya shule ya msingi Nyandekwa.

MACHIBYA Amesema kumekuwa na wizi mkubwa wa mifugo na mazao katika kata hiyo hali inayohatarisha amani na usalama na kwamba mtu yoyoye atakayepitisha mifugo usiku akamatwe na kuweka chini ya ulinzi yeye pamoja na mifugo yake.

Katika hatua nyingine Machibya Ameiomba halmashauri ya mji wa Kahama kufanya msako na kuwazuia wafanyabiashara wa mifugo kupakia Ng’ombe usiku kwani ng’ombe wengi wa wizi wanasafirishwa nyakati hizo bila kukaguliwa vibali.

Naye diwani wa kata ya Nyandekwa KULWA KADEBE amewataka vijana kujiunga na vikundi vya ujasiliamali ili kuondokana na tabia ya kukaa vijiweni huku diwani wa viti maalumu Cesilia Mpemba akitoa wito kwa wanawake kuwaelimisha watoto kuhusu maadili na kuepuka makundi.

Kata ya Nyandekwa imekumbwa na wizi wa mifugo na Chakula katika siku za hivi karibuni ambapo kati ya mwezi wa saba na nane Familia ya Juakali Mashimba imeibiwa magunia 11 ya Mpunga na Ng’ombe 7 huku familia zingine zikiibiwa kuku.
Share:

No comments:

Post a Comment

IDADI YA WASOMAJI

TUSIKILIZE LIVE KUPITIA TUNEIN

UNGANA NASI FACEBOOK HAPA

10 ZILIZOSOMWA ZAIDI

Labels

Blog Archive