Naibu Waziri wa Uchukuzi na Mawasiliano Ameitaka Mamlaka Ya Bandari Tanzania Kusitisha Mpango Wake Wa Kurasimisha Bandari Bubu

Naibu Waziri wa Uchukuzi na Mawasiliano Mhandisi Atashasta Nditiye ameitaka Mamlaka ya Usimamizi wa Bandari Tanzania (TPA) kusitisha mpango wake wa kurasimisha bandari bubu zilizopo mkoa wa Dar es Salaam

Hayo yameelezwa na Nditiye wakati wa ziara yake Wilayani Bagamoyo ya kukagua bandari bubu zilizopo ambapo amebaini uwepo wa bandari bubu zaidi ya kumi na tisa zinazosafirisha bidhaa  kwenye eneo la mwambao wa bahari lililopo wilayani Bagamoyo. 
Amesema kuwa uwepo wa bandari bubu hizo ni kipenyo cha baadhi ya wafanyabiashara kukwepa kulipa kodi kwa kutumia bandari rasmi na hivyo kupunguza mapato ya Serikali na kuihujumu nchi kwa kufifisha jitihada za Serikali za kufikia uchumi wa kati na azma yake ya ujenzi wa viwanda, utoaji wa huduma za afya, elimu, maji, umeme na ujenzi wa miudombinu ya sehemu mbali mbali nchini

Nditiye ameielekeza TPA iache mara moja mpango huo wa kurasimisha bandari bubu zilizopo Mbweni na Temeke kwa kuwa Dar es Salaam ipo bandari na itumike hiyo kwa shughuli za usafirishaji wa bidhaa na abiria. 
“TPA wafute mara moja mpango wao wa kurasimisha bandari bubu za Mbweni, Temeke kuwa bandari rasmi wakati kuna bandari ya Dar es Salaam,” amesema Nditiye. 
Pia, ameongeza kuwa fedha zilizotengwa na TPA kwa ajili ya mpango huo lipewe jeshi la bandari ili waweze kununua vifaa kwa ajili ya kufanya doria ya kuimarisha ulinzi kwenye mwambao wa bandari

Amefafanua kuwa yapo majahazi yanayofanya shughuli za usafirishaji ufukweni mwa bahari ya Hindi kwenye mwambao upatao kilomita 300 kwenye eneo la Bagamoyo ambapo majahazi yanashusha mizigo kinyemela. 
“Nimeshuhudia taratibu za nchi zikikiukwa na kamati ya ulinzi na usalama ya Wilaya ya Bagamoyo inapata changamoto ila inawadhibiti kwa namna moja au nyingine japo yapo majahazi yanayoshusha bidhaa na kuficha kwenye misitu iliyopo ndani ya bahari,” amesema Nditiye.

Pia ameielekeza Mamlaka ya Udhibiti wa Usafiri wa Majini (TASAC) kufanya utaratibu wa kusajili majahazi yasiyozidi ishirini kwenye eneo la Bagamoyo ili yaweze kuwahudumia wananchi wa Bagamoyo na wengine wote watumie bandari Dar es Salaam. 
“Yapo baadhi ya majahazi yamesajiliwa ila mengine yanafanya shughuli zake kinyemela na yanaenda sehemu mbali mbali na baadhi yao wasio waaminifu wanatumia vibaya vibali vyao na wanashusha mizigo baina ya saa tano na saa tisa usiku,” amesema Nditiye. 
Amefafanua kuwa majahazi haya yanakiuka taratibu za nchi kwa kuwawezesha wafanyabiashara kukwepa kodi na hivyo kupunguza mapato ya Serikali na jitihada za Serikali za kufikia uchumi wa wakati

Naye Mkuu wa Wilaya ya Bagamoyo, Zainabu Kawawa amekiri uwepo wa bandari bubu zaidi ya 19 na amemweleza Nditiye kuwa wilaya hiyo inakabiliwa na changamoto za uwepo wa bandari bubu ambazo zinatumia usafiri wa majahazi kuvusha bidhaa mbali ili kukwepa ushuru wa mamlaka mbali mbali kwa mujibu wa sheria za taasisi husika ambapo wanavusha sukari, mafuta ya kula, matairi ya magari, maziwa ya unga, vitenge, khanga, vipodozi na wahamiaji haramu ambapo hadi sasa kuna wafungwa wapatao 203 waliopo gerezani kutokana na uwepo wa wahamiaji haramu.

Kawawa amefafanua kuwa majahazi hayo yanashusha mizigo nyakati za usiku wakiwa ndani ya bahari mara nyingine bila kufika ufukweni kwa kufaulisha na kupakia kwenye mitumbwi ijulikanayo kwa jina maarufu la ngwanda ili iweze kufikishwa nchi kavu kwa ajili ya kusambazwa kwenye maeneo mbali mbali ili kukwepa kodi. 
Amesema kuwa kamati ya ulinzi na usalama imekuwa ikifanya doria kwenye maeneo hayo ili kudhibiti jambo hilo japo wanakabiliwa na changamoto ya ukosefu wa vifaa vya kufanya doria baharini na uwepo wa baadhi ya watumishi wa umma wachache wasio waaminifu ambao wanashirikiana na wafanyabiashara kuihujumu Serikali  kwa kutumia bandari bubu zinazotokana na uwepo wa bahari ya Hindi wilayani humo ambapo bandari bubu hizo ni pamoja na bandari bubu ya Mlingotini, Kasiki, Kaole, Magambani, Kilimani, Badeco, Msalabani, Nunge, Mtailindi, Jicho Kuu, Mto Ruvu, Razaba, Gama, Kayanjo – shamba la chumvi, Saadani, Kitongoji cha Gwaza, Changwahela na Duza
Share:

Kamishna wa zamani TRA Harry Kitilya na wenzake Kuendelea Kusota Rumande

Kamishna wa zamani wa Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA), Harry Kitilya na wenzake wawili wanaokabiliwa na kesi ya kutakatisha fedha wanaendelea kusota rumande kutokana na upelelezi wa kesi yao kutokamilika.

Mbali na Kitilya ambaye pia Mwenyekiti wa Kampuni inayoshughulikia Uwekezaji wa Mitaji na Dhamana (Egma), washtakiwa wengine katika kesi hiyo ni aliyekuwa Miss Tanzania (1996), Shose Sinare na Ofisa wa Benki ya Stanbic, Sioi Solomon.

Kesi hiyo imetajwa leo katika Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu mbele ya Hakimu Mkazi Mkuu, Huruma Shaidi ambapo upande wa Jamhuri ulidai upelelezi haujakamilika huku Wakili wa Serikali Mwandamizi, Mutalemwa Kishenyi akidai kesi hiyo ilipangwa kwa ajili ya kutajwa upelelezi wake haujakamilika  na kwamba wanaelekea ukingoni kukamilisha.

Akijibu Wakili wa utetezi Alex Mgongolwa alihoji ni ukingo gani huo ambao unazungumziwa na upande wa mashtaka.

Hakimu Shaidi aliutaka upande wa mashtaka kufanya jitihada za kukamilisha upelelezi wa kesi hiyo ili hatma ya washtakiwa hao ijulikane na kuahirisha kesi hiyo hadi Novemba 30, mwaka huu na kuutaka upande wa mashtaka kufanya jitihada kukamilisha upelelezi.

Washtakiwa hao kwa pamoja  wanakabiliwa na mashtaka ya kula njama, kujipatia fedha kwa njia ya udanganyifu na kutakatisha fedha ambapo Machi 2013 jijini Dar es Salaam walijipatia Dola za Marekani milioni sita, wakionyesha kuwa fedha hizo zilikuwa ni malipo ya ada ya uwezeshaji upatikanaji wa mkopo  na zililipwa kupitia  Kampuni ya Egma T Ltd.
Share:

Makamu wa Rais Abaini Ubadhirifu wa Milioni 807 Manyara

Makamu wa Rais, Samia Suluhu Hassan ameagiza uchunguzi ufanyike kwenye ujenzi wa madarasa na mabweni ya Shule ya Wasichana Nangwa wilayani Hanang’, Manyara kutokana na madai ya kuwapo kwa ubadhirifu wa Sh807 milioni unaodaiwa kufanywa na maofisa wa Wizara ya Elimu.

Samia alisema hayo jana baada ya kuweka jiwe la msingi la bweni la wasichana wa shule hiyo lenye uwezo wa kulaza wanafunzi 160 lililojengwa na halmashauri ya wilaya hiyo kwa Sh150 milioni.

Alitoa agizo hilo baada ya mkuu wa Mkoa wa Manyara, Alexander Mnyeti kusema baadhi ya maofisa wa Wizara ya Elimu wanafanya ufisadi kwa kufuja fedha za ujenzi wa madarasa na mabweni ya shule hiyo. 
Alisema maofisa hao wametumia zaidi ya Sh807 milioni kujenga madarasa na mabweni wakati bweni lingine kubwa zaidi limejengwa na halmashauri kwa Sh150 milioni.

“Mheshimiwa Makamu wa Rais, nataka nikuhakikishie mkoa huu siyo wa majaribio wa watu kufuja fedha kwani nikiwaandikia barua wanipe taarifa wanadai jengo linajengwa na wizara siyo mkoa,” alisema Mnyeti.

“Kwenye Mkoa wa Manyara miradi inasimamiwa kwa ubora ndiyo sababu mwaka huu tukashika nafasi ya pili kitaifa kwenye mbio za Mwenge kwa ubora wa miradi.”

Aliwapongeza mkuu wa Wilaya ya Hanang Joseph Mkirikiti na mkurugenzi mtendaji Bryceson Kibassa kwa kusimamia maendeleo. “Hawa ni wasaidizi wangu wazuri wanaotimiza wajibu wao ipasavyo,” alisema Mnyeti.

Mama Samia ambaye yuko mkoani Manyara kwa ziara ya kikazi, aliagiza uchunguzi ufanyike mara moja ili kubaini namna ya fedha hizo zilivyotumika katika ujenzi huo.

“Kama jengo la bweni kubwa la halmashauri limetumia fedha kidogo na lina ubora inakuwaje huku wametumia fedha nyingi namna hivyo? Ni lazima hilo lichunguzwe,” alisema.

Pia, aliridhia bweni lililojengwa na halmshauri hiyo aliloweka jiwe la msingi kuitwa jina lake kisha akaendesha harambee ya kusaidia shule hiyo na kupatikana Sh20 milioni.
Share:

MC Luvanda Apewa ONYO na Mahakama


Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu imemuonya mshereheshaji maarufu nchini Tanzania, Anthony Luvanda maarufu kama MC Luvanda kwa kusafiri bila ya ruhusa ya Mahakama.

Onyo hilo limetolewa leo Jumatatu Novemba 19, 2018 na Hakimu Mkazi Mkuu, Huruma Shaidi mbele ya mshtakiwa Luvanda, wakili wake Jebra Kambole na wakili wa Serikali Mwandamizi, Kishenyi Mutalemwa.

Hatua hiyo ilifikiwa baada ya wakili Kishenyi kuieleza Mahakama kuwa upelelezi wa kesi hiyo bado haujakamilika na kwamba mara ya mwisho kulikuwepo na amri ya Mahakama ya kumkamata mshtakiwa huyo kwa kusafiri bila ruhusa ya Mahakama.

Wakili Kishenyi ameeleza Mahakama kwa sababu ametokea akumbushwe masharti ya dhamana.

Baada ya wakili Kishenyi kueleza hayo, wakili wa Luvanda, Jebra Kambole amedai yeye hana pingamizi kuhusu mshtakiwa kukumbushwa masharti ya dhamana na akaomba radhi kwa yaliyotokea na kwamba mambo hayo hayatajirudia tena.

Hakimu Shaidi alimwambia mshtakiwa huyo kila kitu kina nidhamu yake, pia hata katika kesi na kufika mahakamani kuna nidhamu yake.

"Kitendo cha wewe kusafiri bila kuitaarifu Mahakama si kitu kizuri, ukitaka kusafiri toa taarifa."

Hakimu Shaidi ameiahirisha kesi hiyo hadi Desemba 18, 2018 na akamuonya mshtakiwa huyo afuate utaratibu.

Awali, Hakimu Shaidi Oktoba 23, mwaka huu akitoa  hati ya kukamatwa kwa Luvanda wakati kesi hiyo ilipopangwa kwa ajili ya kutajwa lakini mshtakiwa huyo hakuwepo mahakamani.

MC Luvanda pamoja na kampuni yake, wanakabiliwa na mashtaka matatu likiwemo la kutumia kikoa ambacho akijasajiliwa Tanzania.
Share:

Mkapa Awasili Uganda Kuwasilisha Ripoti Ya Usuluhishi Ya Mgogoro Wa Burundi Kwa Rais Museveni

Rais Mstaafu wa awamu ya tatu, Mhe. Benjamin William Mkapa ambaye ni msuluhishi wa mgogoro wa Burundi akiwa katika chumba cha wageni maalum katika uwanja wa Ndege wa Entebbe leo. kulia ni Mwambata Jeshi wa Ubalozi wa Tanzania nchini Uganda, Brig Gen. Mkumbo, kushoto ni Msaidizi wa Rais Mkapa katika utatuzi wa mgogoro huo, Balozi David Kapya na anayemfuatia ni Balozi wa Tanzania nchini Uganda, Mhe. Dkt. Aziz Mlima. 
Mkapa aliwasili katika Uwanja wa Ndege wa Entebbe asubuhi ya tarehe 19 Novemba 2018 kwa ajili ya kuwasilisha ripoti ya mkutano wa upatanishi uliofanyika hivi karibuni jijini Arusha kwa Mpatanishi Mkuu wa mgogoro huo Rais wa Uganda, Mhe. Yoweri Kaguta Museveni. 
 
Balozi wa Tanzania nchini Uganda, Mhe. Dkt. Aziz Mlima (kushoto) akimsikiliza Rais Mstaafu wa awamu ya tatu, Mhe. Benjamin William Mkapa ambaye ni msuluhishi wa mgogoro wa Burundi.
Share:

Trump Amfuta Kazi Mwanasheria Mkuu wa Marekani Jeff Sessions

Mwanasheria Mkuu wa Marekani Jeff Sessions amejiuzulu wadhifa wake, baada ya kuombwa kufanya hivyo na Rais Donald Trump.

Trump ametangaza kuondoka kwa Sessions kupitia ukurasa wake wa Twitter leo Alhamis Oktoba 8, akimtakia kila la kheri.

Nafasi yake itashikiliwa kwa muda na aliyekuwa mkuu wake wa utumishi Matthew Whitaker. Whitaker sasa atasimamia uchunguzi wa madai ya Urusi kushirikiana na kampeni za rais Trump mwaka 2016.

Nancy Pelosi, anayetarajiwa kuliongoza Baraza la wawakilishi amesema kujiuzulu huko ni jaribio la wazi la Trump, kupunguza makali ya mchunguzi maalumu Robert Mueler anayeongoza uchunguzi huo wa Urusi.

Kiongozi mwingine wa Democratic katika seneti Chuck Schumer amesema mabunge yote ya Marekani ni lazima yalinde uchunguzi huo.
Kwa upande wake, Jeff Sessions katika barua yake ya kujiuzulu, aliweka bayana kuwa uamuzi wa kuondoka katika nafasi hiyo haukuwa wake.

Katika barua isiyokuwa na tarehe alimjulisha Rais kwamba anawasilisha barua yake ya kujiuzulu kama alivyomtaka afanye hivyo
Share:

Spika Ndugai Amzuia Waziri Mkuu Kujibu Swali Linahusu Balozi wa EU Aliyeitwa Nchini Kwao


Spika wa Bunge, Job Ndugai amemzuia Waziri Mkuu Kassim Majaliwa kujibu swali juu ya kuitwa nchini kwake balozi wa Umoja wa Ulaya (EU) nchini, Roeland van de Geer kwa kile alichokisema swali hilo lilikuwa nje ya uwezo wa Serikali.

Swali hilo liliwasilishwa bungeni na Mbunge Cecil Mwambe wakati wa kipindi cha maswali na majibu kwa Waziri Mkuu ambapo alihoji juu ya wito wa balozi huyo wa Umoja wa Ulaya.

“Hivi karibuni tulishuhudia balozi wa EU alikuwa ameitwa kwao kujadili mahusiano ya nchi yetu na jumuiya za kimataifa. Kuna nini kinachoendelea?" Alihoji Mbunge Cecil

Akitoa maelezo ya maswali hayo Spika Ndugai amesema “Napata wakati mgumu kupitisha swali lako sasa kama ameitwa nchini kwao unataka Waziri Mkuu ajibu nini, waziri Mkuu tunakushukuru nenda unaweza kwenda kupumzika.”

Ufafanuzi wa wito wake ulitolewa na Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Balozi Dk.Augustine Mahiga ambapo aliweka wazi kuwa balozi huyo hajafukuzwa kama inavyoelezwa bali ameitwa makao makuu ya umoja huo.

''Balozi wa Umoja wa Ulaya (EU) nchini Tanzania, Roeland van de Geer anayetarajia kuondoka leo (jumamosi iliyopita)  usiku kwenda makao makuu ya EU hajafukuzwa bali ameitwa na umoja huo kikazi'', ilieleza taarifa ya Waziri Dr.Mahiga.

Taarifa za kufukuzwa kwa balozi Roeland van de Geer zilisambaa usiku wa Ijumaa mitandaoni na kuzua mijadala mbalimbali, jambo ambalo ilipelekea Waziri husika kutolea ufafanuzi.
Share:

Kigogo wa IPTL Harbinder Sethi Ahojiwa Upya na TAKUKURU

Wakili wa Serikali kutoka Taasisi ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa (Takukuru), Leonard Swai, amedai mahakamani kwamba wamemaliza kumhoji kigogo wa IPTL, Harbinder Sethi baada ya kuomba mahakamani kufanya hivyo.

Swai amedai hayo leo Alhamisi Novemba  8, katika Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu mbele ya Hakimu Mkazi Mkuu, Huruma Shaidi wakati kesi hiyo inatajwa.

Alidai upelelezi wa kesi hiyo ya kutakatisha fedha inayomkabili Sethi na James Rugemarila haujakamilika isipokuwa walipata nafasi ya kumuhoji Sethi.

Swai aliomba mahakama ipange tarehe nyingine ya kesi kutajwa na upelelezi unaendelea.

Mahakama iliahirisha kesi hiyo hadi Novemba 22 mwaka huu kwa ajili ya kutajwa. Watuhumiwa hao bado wanaendelea kusota rumande
Share:

Serikali Kuendelea Kufuta Hatimiliki za Mashamba Yaliyotelekezwa

Serikali imeendelea kuchukua hatua za kubatilisha milki za ardhi za mashamba yaliyotekelezwa katika maeneo mbalimbali nchini.

Hayo yamesema Bungeni jana na Naibu Waziri wa Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi Angelina Mabula  wakati akijibu swali la Mhe. Dustan Kitandula Mbunge wa Mkinga kuhusu kufuta hati za mashamba yaliyotelekezwa.

“Katika kipindi cha Disemba, 2015 mpaka Octoba, 2018 mashamba yenye ukubwa wa ekari 84,240.803 yamebatilishwa katika Halmashauri za Ngorongoro, Arumeru, Moshi, Kinondoni,(Manispaa), Kigamboni(Manispaa), Mvomero, Kilombero, Kilosa, Mvomero, Iringa, Bukoba, Tarime, Kibaha, Serengeti, Busega, Muheza, Lushoto na Mkinga” amefafanua Naibu Waziri Mabula.

Mabula anasema kuwa, katika Halmashauri ya Wilaya ya Mkinga, Shamba Na. 278 Mkomazi lenye ukubwa wa ekari 15,442 lililokuwa likimilikiwa na kampuni ya M/S Mkomazi Plantations Limited kwa Hati Namba 4268, 9780  na 9781 milki yake ilithibitishwa tarehe 20 Juni, 2018.

Aidha anafafanua kuwa, baada ya kubatilishwa kwa milki ya shamba hilo, Serikali ya Mkoa wa Tanga kwa kushirikiana na Halmashauri ya Wilaya ya Mkinga zipange matumizi mapya ya shamba hilo kwa kuzingatia mahitaji ya ardhi katika eneo hilo kipaumbele kikiwa ni mahitaji ya wananchi na ardhi kwa ajili ya uwekezaji.

Mbali na hayo Mabula amezitaka Halmashauri zote nchini kubaini mashamba yaliyotelekezwa kutuma ilani kwa wamiliki wa mashamba hayo kwa mujibu wa Sheria ya Ardhi (Sura 113) na kuwasilisha mapendekezo katika Wizara ya Ardhi kwa hatua za kubatilisha milki za mashamba hayo ziweze kufanyika.
Share:

Msemaji Mkuu wa Serikali: Serikali Itaendelea Kutekeleza Miradi Mikubwa Ya Kimkakati

SERIKALI imesema kamwe haitokatishwa tamaa na kauli ya baadhi ya Viongozi na wanasiasa kuhusu dhamira yake ya kutekeleza miradi mikubwa ya kimamkati yenye malengo ya kuleta maguezi ya kijamii na kiuchumi kwa Watanzania.

Hayo yamesemwa leo Jijini Dar es Salaam na Mkurugenzi wa Idara ya Habari (MAELEZO) na Msemaji Mkuu wa Serikali, Dkt. Hassan Abbasi wakati wa ziara ya kutembelea Kituo cha Redio ya TBC Taifa na tathmini ya utendaji kazi katika kipindi cha miaka mitatu ya Serikali ya Awamu ya Tano.

Dkt. Abbasi alisema tangu kuingia madarakani kwa Rais Dkt. John Pombe Magufuli, Serikali ya Awamu imekuwa ikitekeleza miradi mikubwa ya maendeleo ambayo wadau mbalimbali wa maendeleo wameipongeza Serikai yake kwa mafanikio makubwa yaliyofikiwa lakini wapo baadhi ya baadhi ya Viongozi na wanasiasa wachache wamekuwa wakipinga mageuzi hayo pasipo na kutoa hoja za msingi.

“Mageuzi yanayoendelea kufanywa hayatakuwa na mwisho, Serikali ya Awamu ya Tano na Watendaji wote tunaomsaidia Rais John Pombe Magufuli tumedhamiria kuleta mapinduzi ya kweli kwa kuboresha huduma za msingi kwa wananchi na tutapokea maoni na ushauri lakini kamwe haturudishwi nyuma na Viongozi na watendaji wanaopinga mageuzi haya” alisema Dkt. Abbasi.

Akitolea mfano Dkt. Abbasi alisema mara baada ya Serikali kutangaza dhamira ya kuanzisha mradi wa kihistoria wa kufua umeme wa Stiegler’s Gorge uliopo Wilayani Rufiji mkoani Pwani wapo baadhi ya wanasiasa na Viongozi wamekuwa wakipinga mradi huo kwa kigezo cha uharibifu wa mazingira ya eneo hilo, jambo ambalo lililenga kupeleka taswira hasi kwa wananchi na wadau mbalimbali wa maendeleo.

Anasema mageuzi mengine yaliyofanywa na Serikali ya Awamu ya Tano ni pamoja na ujenzi wa ukuta katika machimbo ya madini ya Tanzanite, ambapo kutokana na hatua hizo katika kipindi cha mwezi Julai hadi Novemba Serikali imeweza kukusanya mapato ya kiasi cha Tsh Milioni 890.

Kwa mujibu wa Dkt. Abbasi alisema katika kuelekea katika mageuzi ya kijamii na kiuchumi, Serikali ya Awamu ya Tano imeendelea kuungwa mkono na wadau mbalimbali wa maendeleo pamoja na kuweka mfumo imara wa usimamizi wa fedha za umma ikiwemo makusanyo ya kodi, hatua inayoiwezesha Serikali kutekeleza miradi mbalimbali ya maendeleo.

Aliongeza kuwa Serikali ya Awamu ya Tano inayoongozwa na Rais Dkt. John Pombe Magufuli itaendelea kutekeleza sera na programu mbalimbali ikiwemo sera ya elimu bure katika ngazi za elimu ya awali, msingi na sekondari, ambapo Serikali imekuwa ikitoa Tsh Bilioni 23 kila mwezi kwa ajili ya gharama za uendeshaji wake.

Akifafanua zaidi alisema kutokana na kuongezeka kwa kiwango cha ukusanyaji wa kodi, Serikali imeweza kufanya mageuzi makubwa katika sekta mbalimbali za kijamii ikihusisha afya, maji, barabara pamoja na ununuzi wa ndege mpya nne za Serikali na hivyo kufufua upya huduma za Shirika la ndege Nchini (ATCL) ambazo zilisimama kwa kipindi kirefu.

Akianisha mafanikio ya ATCL, Dkt. Abbasi anasema moja ya mageuzi makubwa yaliyofikiwa kwa sasa na shirika hilo ni pamoja na ongezeko la abiria kutoka abiria 3000-4000 kwa mwezi ambapo kwa sasa wateja wanaotumia Ndege za Shirika hilo wamefikia 30,000 kwa mwezi.

“Mpaka sasa tuna ndege nne za Serikali, na mwezi Desemba tutapokea ndege nyingine 2 aina ya Airbus na mwakani (2019) mwezi Oktoba tutapokea ndege nyingine 1 na kuzifanya ndege mpya za Serikali kufikia saba, na hivyo kufanya sekta ya uchukuzi kuwa katika mabadiliko makubwa ya utendaji na uendeshaji” alisema Dkt. Abbasi.
Share:

Waziri Mkuu Awaonya Waagizaji Wa Taulo Za Kike....Ni Wale Wanaoziuza Kwa Bei Ya Juu Licha Ya Serikali Kuziondolea Kodi


WAZIRI Mkuu Kassim Majaliwa amewatakabaadhi ya waagizaji wa taulo za kike ambao wanaziuza kwa bei ya juu licha ya kufutwa kwa kodi, waache mara moja na Serikali haitasita kuwafutia leseni zao za uagizaji mara watakapogundulika kutotekeleza maelekezo hayo.

Waziri Mkuu ametoa onyo hilo jana (Jumatano, Novemba 7, 2018) wakati akizindua mkakati wa Bunge wa masuala ya kijinsia, Bungeni jijini Dodoma. Amesema Serikali imeendelea kuchukua hatua mbalimbali kwa lengo la kuhakikisha kuwa wanawake wanawekewa mazingira mazuri yatakayowawezesha kupiga hatua zaidi.

Amesema hatua hizo ni pamoja na kuondoa kodi ya  taulio za kike ili kuwezesha wanafunzi wa kike ambao walikuwa wanaacha masomo kutokana na changamoto ya kununua taulo za kike kwa ajili ya kujisitiri wakati wa hedhi wazipate kwa gharama nafuu.

Waziri Mkuu amesema hatua nyingine ni mpango wa Serikali wa kujenga zahanati kila kijiji na kituo cha afya katika kila kata kwa lengo la kupunguza vifo vya wanawake na watoto vilivyokuwa vinasababishwa na uhaba wa huduma za afya ya mama na mtoto.

Amesema mpango huo wa Serikali unatarajiwa kuongeza tija kwa wanawake hususan katika kuwapunguzia muda ambao wamekuwa wakiutumia katika kutafuta huduma hizo ambazo zilikuwa zinapatikana kutoka umbali mrefu.

“Imethibitika kupitia tafiti za kitaifa na kimataifa kwamba uzazi wa mpango huweza kupunguza vifo vitokanavyo na uzazi kwa hadi asilimia 44 na vifo vya watoto kwa hadi asilimia 35.

 Pamoja na kulinda afya ya mama na mtoto, huduma hizi zinawasaidia wanawake na wasichana kupata nafasi za kujiendeleza zaidi pamoja na familia zao na kuongeza ushiriki wao katika shughuli za kiuchumi, kijamii, na kimaendeleo.”

Hata hivyo, Waziri Mkuu amesema Serikali imeendelea kuwahamasisha wanafunzi wa kike kusoma masomo ya sayansi sambamba na kuwawekea mazingira wezeshi.

Amesema hatua nyingine ni mpango wa Serikali wa kuwasomesha wanawake katika ngazi ya uzamili ili waweze kushika nafasi nyingi zaidi za uongozi Serikalini na mahali pa kazi. Zoezi hilo linaratibiwa na Idara Kuu ya Utumishi.

Katika hatua nyingine,Waziri Mkuu amesema mifumo yetu, mila na historia vimewafanya wanawake na wasichana wabaki nyuma kwa kujiajiri kwenye sekta isiyo rasmi na isiyo na kipato cha uhakika wala maslahi na kubaki wakiwa wategemezi kiuchumi.

Amesema hivi karibuni Serikali imeanza  kutekeleza kampeni ya Rais Dkt. John Magufuli ya kumtua mama ndoo kichwani. Kampeni hiyo inalenga kuwaondolea wananchi hususani wanawake tatizo la upatikanaji wa haraka wa huduma ya maji safi na salama.

Kwa upande wake, Spika wa Bunge, Job Ndugai amesema Bunge linaendeshwa kwa kuzingatia uwiano wa kijinsia kwa kiwango cha kuridhisha. “Hata tunapoteua baadhi ya wabunge kwa ajili ya kutuwakilisha katika mikutano mbalimbali huwa tunazingatia uwiano wa kijinsia.

Amesema atahakikisha Bunge linaendeleza azma ya Serikali ya kujenga Taifa lenye usawa wa kijinsia inatimia, ambapo amewataka mawaziri wanapowasilish hotuba za makadirio ya mapato na matumizi ya wizara zao waeleze namna walivyotekeleza jambo hilo.

IMETOLEWA NA:
OFISI YA WAZIRI MKUU,
Share:

Serikali Yapiga Marufuku Watumishi Wa Umma Waliohamia Dodoma Kuomba Uhamisho Kurejea Dar Es Salaam

Serikali imepiga marufuku Watumishi wa Umma waliohamia Makao Makuu ya Nchi Dodoma kwa gharama za Serikali kuomba uhamisho wa kurejea jijini Dar es Salaam.

Hayo yamesemwa jana na Katibu Mkuu, Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma, Dkt. Laurean Ndumbaro alipokuwa akifanya mahojiano maalum na Shirika la Utangazaji Tanzania (TBC) kuhusiana na zoezi zima la uhamisho wa watumishi wa umma kutoka Dar es Salaam kwenda Dodoma.

Dkt. Ndumbaro amesema kuwa,  Ofisi yake imekuwa ikipokea barua mbili au tatu kwa siku za watumishi waliohamia Dodoma kuomba uhamisho wa kurejea Dar es Salaam kutokana na sababu mbalimbali ikiwa ni pamoja na za kiafya wakati hospitali ya Rufaa ya Benjamin Mkapa ina vifaa vya kisasa na uwezo mkubwa wa kutoa huduma za matibabu kwa watumishi hao.

Dkt. Ndumbaro amefafanua kwamba,  kabla ya watumishi kuhamia Dodoma, Serikali ilitoa maelekezo kwa waajiri kuwasilisha orodha ya watumishi wenye matatizo ya kimsingi ili wabaki kwenye vituo vya kazi vilivyopo Dar es Salaam wakiendelea kutekeleza majukumu yao.

Dkt. Ndumbaro ameongeza kuwa, baadhi ya watumishi waliohamia Dodoma, wamegeuza uhamisho huo kuwa mradi  wa kuwaingizia kipato kwani mara baada ya kuripoti Dodoma, ndani ya kipindi kifupi wanaomba uhamisho wa kurejea Dar es Salaam.

Dkt. Ndumbaro amesisitiza kuwa, kutokana na suala hilo, Serikali imetoa Waraka wa Barua wenye Kumb. Na. CAC 228/257/01/A/53 wa tarehe 25 Septemba, 2018 kuhusu Uhamisho wa Watumishi Waliohamia Dodoma Kutekeleza Uamuzi wa Serikali Kuhamishia Makao Makuu ya Nchi Dodoma ambao unazuia mtumishi aliyehamishiwa Dodoma kwa gharama za Serikali kuomba uhamisho wa kurejea Dar es Salaam mpaka atimize miaka mitatu katika kituo cha Dodoma.

Watumishi wa Umma kuhamia Dodoma ni utekelezaji wa agizo la Serikali lililotolewa na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Dkt. John Pombe Magufuli tarehe 25 Julai, 2016 wakati wa maadhimisho ya Kumbukumbu ya Siku ya Mashujaa.
Share:

Benki Kuu ya Tanzania Yatangaza kuongeza muda siku sitini (60) wa usimamizi wa Bank M PLC.

Benki Kuu ya Tanzania imeongeza muda wa usimamizi wa Bank M Tanzania Plc (Bank M) kwa siku 60 zaidi kuanzia tarehe 2 Novemba 2018.

Kwa mamlaka iliyopewa chini ya kifungu namba 56 (1) (g) (iii) cha Sheria ya Mabenki na Taasisi za Fedha ya mwaka 2006, Benki Kuu ya Tanzania ilichukua usimamizi wa Bank M kuanzia tarehe 2 Agosti 2018 baada ya kubaini kuwa benki hiyo ilikuwa na upungufu mkubwa wa ukwasi kinyume na matakwa ya sheria ya Mabenki na Taasisi za Fedha ya mwaka 2006 na kanuni zake.

Baada ya kuchukua usimamizi, Benki Kuu ya Tanzania ilisitisha shughuli za utoaji wa huduma za kibenki za Bank M kwa muda wa siku tisini (90) ili kuipa nafasi Benki Kuu ya Tanzania kutathmini hatua za kuchukua ili kupata ufumbuzi wa suala hilo.

“Benki Kuu ya Tanzania inapenda kuuarifu umma kuwa mchakato wa kutathmini hatua za kuchukua ili kupata ufumbuzi wa matatizo ya Bank M haujakamilika; hivyo muda wa usimamizi umeongezwa kwa kipindi cha siku 60 kuanzia tarehe 2 Novemba 2018,” kwa mujibu wa taarifa kwa umma iliyotolewa leo.

Aidha, Benki Kuu ya Tanzania inauhakikishia umma kuwa itaendelea kulinda maslahi ya wenye amana katika mabenki kwa lengo la kuleta ustahimilivu katika sekta ya fedha.
Share:

Kamati Ya Bunge Ya Bajeti Yawaalika Wadau Wa Masuala Ya Fedha Kutoa Maoni Kuhusu Muswada Wa Sheria Ya Huduma Ndogo Za Fedha Wa Mwaka 2018


Share:

Maandalizi Ya Ujenzi Wa Barabara Ya Njia Sita Ya Ubungo-chalinze


Muonekano wa barabara ya Morogoro eneo la Kimara mwisho Jijini Dar es salaam hivi leo ambapo tayari maandalizi  ya ule mradi wa ujenzi wa barabara ya njia sita kutoka Ubungo hadi Kibaha Mkoani Pwani yenye urefu wa kilometa 16 umeiva. 

Ujenzi wa barabara hiyo unaotarajia kuanza mwishoni mwa mwezi Disemba mwaka huu utasaidia kukuza uchumi kwa kuongeza kasi ya usafirishaji wa bidhaa katika nchi jirani kupitia bandari ya Dar es Salaam.  

Pia inatarajiwa utasaidia kupambana na changamoto ya msongamano wa magari na kuziwezesha barabara zote za Jiji la Dar es Salaam kupitika katika majira yote ya mwaka. 
Picha na IKULU
Share:

Sakata la Mauaji ya Wananchi Kigoma Linalodaiwa Kufanywa na Wakala wa Misitu Tanzania (TFS) Laibuka Bungeni

Sakata la vifo vya wananchi na polisi mkoani Kigoma vilivyosababishwa na mgogoro wa ardhi hivi karibuni limeibukia bungeni, ikiwa ni siku chache baada ya Mbunge wa Kigoma Mjini (ACT-Wazalendo), Zitto Kabwe kukamatwa na kisha kushtakiwa.

Zitto alikamatwa wiki iliyopita na kushtakiwa katika Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu jijini Dar es Salaam, baada ya mkutano wake na wanahabari kuzungumzia suala hilo.

Wiki chache zilizopita, polisi walikiri kutokea kwa mapigano yaliyosababisha vifo vya watu wawili na askari wawili waliokwenda kwa ajili ya kulinda amani huko Uvinza.

Jana, mbunge wa Viti Maalumu (CCM), Josephine Genzabuke ndiye aliyeliibua bungeni akihoji ni kwa nini Wakala wa Misitu Tanzania (TFS) wamekuwa wakiua na kuwatesa wananchi ambao Rais John Magufuli aliwataka kukaa eneo la Kagerankanda bila ya kuongeza mipaka wakati Serikali ikiwatafutia maeneo mengine.

Baada ya majibu ya Serikali kutoka kwa Naibu Waziri wa Malisili na Utalii, Japhet Hasunga, mbunge Genzabuke alisimama kwa kuuliza swali la nyongeza lililoonekana kumkera Spika Job Ndugai. Genzabuke alihoji,

“Hawa TFS wanaua watu, wanawakata mikono na kuwatesa, kwa nini wanafanya hivyo wakati Rais aliagiza wasibuguziwe.”

Katika swali lake la nyongeza, mbunge huyo alihoji kama TFS wanapingana na agizo la Rais lililotaka wananchi wa maeneo ya Kagerankanda waendelee kulima bila kuongeza maeneo.

Hata hivyo, Spika Ndugai alimzuia kuendelea na swali hilo akisema mambo anayozungumza ni mazito na kumtaka akae chini. Licha ya mbunge huyo kutaka kuendelea kujenga swali lake, lakini aliitwa mbunge mwingine.

Baadaye Ndugai alisimama na kutoa ufafanuzi kwa kukemea maswali aliyosema ni mazito ambayo yalipaswa kupelekwa kwa Waziri Mkuu na si kuulizwa kama ya nyongeza bungeni.

Baada ya kipindi cha maswali na majibu, Mbunge wa Mbozi (Chadema), Pascal Haonga aliomba mwongozo akitaka kuhoji ni kwa nini Spika alimzuia mbunge huyo kuuliza swali la nyongeza.

Spika alimkatiza akisema jambo hilo alishaliondoa kwenye mjadala, hivyo halikuwa na ulazima tena wa kuulizwa mbele ya Bunge.

Awali, katika majibu ya swali la msingi, Naibu Waziri Hasunga alikiri kuwa Rais Magufuli aliagiza ofisi ya mkuu wa Mkoa wa Kigoma kuwapimia wananchi eneo hilo.

Hasunga alisema jumla ya hekta 10,012.61 zilitengwa kwa ajili ya kilimo kwa wananchi wa maeneo hayo na kijiji cha Mvinza kilipewa hekta 2,174, Kagerankanda 2,496 na eneo lingine la hekta 5,342.61 lilitengwa kwa ajili ya wananchi wengine.
Share:

Taifa Stars Wakwea Pipa Kuelekea Afrika Kusini Kwa Ajili ya Maandalizi ya Kuikabili Lesotho

Kikosi cha timu ya Taifa ya Tanzania "Taifa Stars"  kimeondoka alfajiri ya jana kwenda Afrika Kusini kuweka kambi ya kujiandaa na mchezo dhidi ya Lesotho katikati ya mwezi huu kwa ajili ya kufuzu Fainali za Kombe la Mataifa ya Afrika (AFCON) mwakani, nchini Cameroon.

Kikosi hicho kimeondoka kikiwa na matumaini makubwa kwamba mazoezi watakayoyafanya yatawasaidia kuibuka na ushindi mchezo wao ujao dhidi ya Lesotho ugenini.

Taifa Stars watakuwa wageni wa Mamba wa Lesotho Novemba 18, mwaka huu, Uwanja wa Setsoto mjini Maseru, katika mchezo wa Kundi L kufuzu AFCON ya mwakani, itakayofanyika Cameroon.

Kikosi hicho kitaweka kambi ya siku 10 nchini Afrika Kusini kikijifua vikali chini ya Kocha wake Mkuu, Mnigeria Emmanuel Amunike na msaidizi wake, Hemed Morocco.

Wachezaji waliosafiri na Stars ni pamoja na makipa Aishi Manula wa Simba SC, Aaron Kalambo wa Tanzania Prisons, Beno Kakolanya wa Yanga SC na Benedictor Tinocco wa Mtibwa Sugar.

Mabeki ni Shomary Kapombe, Erasto Nyoni wa Simba SC, Ally ëSonsoí Abdulkarim wa Lipuli FC, Kelvin Yondan, Gardiel Michael wa Yanga SC, Aggrey Morris na Abdallah Kheri wa Azam FC.

Viungo ni Salum Abubakar ëSure Boyí, Mudathir Yahya wa Azam FC, Salum Kimenya wa Tanzania Prisons, Feisal Salum wa Yanga SC, Jonas Mkude na Shiza Kichuya wa Simba SC.

Washambuliaji ni Thomas Ulimwengu aliye huru baada ya kuvunja mkataba na Al Hilal ya Sudan mwishoni mwa wiki, John Bocco wa Simba SC na Yahya Zayed wa Azam FC.
Share:

Teknolojia Mpya Yaanza Kuwaumbua Wabunge Wakorofi Bungeni

Wabunge wasumbufu wanapokuwa ndani ya ukumbi wa Bunge, wamepatiwa mwarobaini baada ya Spika wa Bunge, Job Ndugai, kusema anaweza kuwaona wabunge wote ukumbinu kupitia kwenye kifaa maalumu kilichofungwa kwenye meza yake.

Ndugai alisema hayo bungeni   Dodoma jana alipokuwa akiendesha kikao cha 13 cha Bunge la 11.

Wakati Waziri Kivuli wa Fedha, Halima Mdee akiwasilisha maoni ya Kambi Rasmi ya Upinzani bungeni juu ya Mapendekezo ya Mpango wa Maendeleo wa Taifa na Mwongozo wa Maandalizi ya Mpango na Bajeti ya Mwaka 2019/20, Ndugai alionekana kukemea wabunge waliokuwa wakipiga makofi kwa kutumia vitabu.

“Waheshimiwa wabunge siyo busara kutumia vitabu kupiga makofi, halafu mnatumia kitabu chenu (cha hotuba ya kambi ya upinzani) hiki.

“Siyo vizuri tumieni mikono, nawaona wote uipitia hiki kifaa hapa,” alisema Ndugai.

Pia katika kikao hicho cha asubuhi, kuna wakati wabunge walikuwa wakipiga kelele huku shughuli zikiendelea.

Spika Ndugai aliwakemea akitaja upande (wa upinzani au CCM) wenye kelele zaidi huku akisisitiza kuwa alikuwa anawaona wabunge hao kupitia kifaa hicho.

Kifaa hicho kipo kwenye kiti ambacho Spika ama mtu mwingine anayeongoza kikao cha Bunge huketi wakati Bunge likiendelea na kikao cha kawaida.

Kifaa hicho pia kipo eneo la makatibu wa Bunge ambako wakati Bunge likiwa limekaa kama kamati, Mwenyekiti anayeongoza kikao hicho huketi eneo hilo.

Jana, Ndugai alitoa kauli hiyo wakati Bunge likiwa limekaa kusikiliza Waziri wa Fedha na Mipango Dk. Philip Mpango, akiwasilisha Mpango wa Maendeleo ya Taifa na lilipokaa kama kamati ya mipango kusikiliza hotua ya Kamati ya Bajeti ya ile ya Kambi ya Upinzani.

Ndugai akiwa ameketi kama Spika na hata alipoketi kama mwenyekiti wa kamati ya mipango, alionekana akiwakemea wabunge kwa nyakati tofauti huku akisema alikuwa anawaona kupitia teknolojia hiyo.

Teknolojia hiyo, mbali na kusaidia kuona wabunge wasumbufu pia itasaidia kuona haraka   Mbunge anayetaka kuuliza swali au kutoa hoja yoyote.
Share:

Mbunge CCM amtuhumu Waziri wa Ujenzi kutoa kauli ya kumdharau Waziri Mkuu

Mbunge wa Mafia, Mbaraka Dau (CCM), amemtuhumu Waziri wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano, Isaack Kamwele, akidai amekiuka agizo la Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa, la kupeleka Mafia meli iliyotolewa na mfanyabiashara  Said Salim Bakhressa akidai ni maagizo ya kisiasa.

Dau amesema hayo bungeni jijini Dodoma leo Jumanne Novemba 6, wakati akiwasilisha Mapendekezo ya Mpango wa Maendeleo wa Taifa na Mwongozo wa Maandalizi ya Mpango na Bajeti ya Mwaka 2019/20.

Alidai kuwa, suala la kupeleka meli hiyo Mafia walilijadili na Waziri Mkuu Majaliwa na akakubali ipelekwe Mafia jambo ambalo hata Profesa Makame Mbarawa aliyekuwa waziri wa wizara hiyo, aliliridhia.

“Sasa hivi nimemfuata na kumkumbusha suala hilo lakini Waziri Kamwele anasema ni kauli za kisiasa, sasa inakuwaje waziri anasema agizo la Waziri Mkuu ni la kisiasa,” alihoji.

Alisema pia alimtuma mbunge mwenzake ili azungumze  na Waziri Kamwele, lakini naye alijibiwa kuwa ili meli ipelekwe huko labda nauli iwe Sh 100,000.

Kabla ya mchangiaji wa mwisho kusimama, Waziri Kamwele alisimama na kusema; “Mbunge wa Mafia amenituhumu kuwa nilitoa maneno yanayoosha nimemdharau Waziri Mkuu, sijawahi kusema hayo maneno na waziri mkuu ila nakumbuka alinipigia simu akanimbia meli hiyo iliyotolewa na mfanyabiashara Bakhresa ifanye safari Mafia, nikatoa maagizo suala hilo liangaliwe kama linawezekana nikaambiwa meli hiyo inafanyiwa matengenezo,” amesema Kamwelwe akidai kauli ya Dau si nzuri kwa sababu Waziri Mkuu ni bosi wake.
Share:

Jeshi la Polisi: Tunaendelea Kumsaka Mpenzi wa Wema Sepetu

Polisi Kanda Maalum ya Dar es Salaam wamesema wanamsaka mwanaume aliyeonekana kwenye mitandao ya kijamii akiwa na msanii Wema Sepetu.

Akizungumza leo Jumanne Novemba 6, 2018, Kaimu Kamanda wa Kanda hiyo, Liberatus Sabas amesema polisi wanaendelea kumsaka mwanaume huyo na wakimpata wanamfikisha mahakamani.

“Polisi tunaendelea kumtafuta huyu jamaa, hatujakata tamaa na ikiwa tutamkamata lazima tumfikishe mahakamani kwani ana kesi ya kujibu,’’ amesema.

Amesema kwamba watu wanadhani labda jeshi la polisi limeshaachana na mwanaume huyo lakini bado ni mtuhumiwa na hivyo akikamatwa anapelekwa mahakamani.
Share:

CCM Yawapa Onyo Viongozi Mizigo Uchaguzi Mkuu 2020

Katibu wa Itikadi na Uenezi wa CCM, Hamphrey Polepole amesema licha ya ushindi mkubwa wanaoendelea kuupata kwenye chaguzi mbalimbali, lakini hawatakua tayari kuwarudisha viongozi mizigo kwa wananchi katika uchaguzi mkuu mwaka 2020.

Polepole aliyasema hayo leo Jumanne Novemba 6, 2018 wakati akizungumza na wajumbe wa kamati za siasa mkoa na wilaya ya Kusini Unguja visiwani Zanzibar katika ukumbi wa mkutano wa TC Dunga.

Alisema wabunge na madiwani pamoja na wawakilishi wa CCM wanapaswa kujitathmini wakifahamu wana jukumu kubwa la kuwaletea maendeleo wananchi.

"Chama chetu hakikuwapa nafasi ya uongozo kama zawadi ili mwende mkale bata, tumewapa nafasi ya kuwatetea wananchi wenu na kutetea ilani ya chama chetu" alisema.

Pamoja na hayo, Polepole aliwataka watendaji wa Serikali wakiwamo wakurugenzi wa manispaa na viongozi wengine wa wilaya na mikoa kuhudhuria vikao vyote vya chama kueleza utekelezaji wa ilani ya chama katika majukumu yao.

Alisema haiwezekani kuona wana CCM wanafanya kazi halafu kuna watendaji wanashindwa kuwajibika ipasavyo.

Polepole alisema watendaji hao wanapofanya vibaya lawama kubwa inawenda kwenye chama ambacho ndiyo chenye kutekeleza ilani yake.
Share:

Polisi Dar Yakamata Silaha Aina ya ShortGun na Watuhumiwa 14 wa Wizi wa Magari

Jeshi la Polisi Kanda Maalum Dar es salaam limefanikiwa kukamata silaha moja aina ya Short Gun, risasi nne za short gun na mlipuko moja uliotengenezwa kienyeji.


Kaimu Kamanda wa Polisi Kanda Maalum Dar es Salaam, LIBERATUS SABAS-DCP ametoa taarifa hiyo mbele ya waandishi wa habari leo Jijini Dar es Salaam, amesema Silaha hiyo ilikamatwa tarehe 25 Oktoba 2018 majira ya saa 21:30 huko maeneo ya Kijichi. Askari wakiwa doria waliitilia mashaka pikipiki iliyokuwa haina namba za usajili ikiendeshwa na kijana mmoja akiwa amewapakia wenzake wawili.

Vijana hao baada ya kutambua kuwa wanafuatiliwa na Polisi walianza kuwafyatulia risasi huku wakikimbia, ndipo askari walipojibu mapigo na kufanikiwa kumjeruhi kijana mmoja na kupelekea kufariki akiwa anapelekwa hospitali.

Kijana huyo alipekuliwa na kukutwa akiwa na silaha aina ya Shotgun iliyokatwa mtutu na kitako ikiwa na risasi nne pamoja na mlipuko mmoja.

Msako mkali unaendelea kuwasaka watuhumiwa wote waliotoroka ikiwa ni pamoja na wahalifu wengine wanaofanya matukio ya kihalifu kwa kutumia silaha za moto ndani ya jiji la Dar es Salaam.

Katika tukio lingine, Jeshi la Polisi Kanda Maalum ya Dar es Salaam huko maeneo ya Kijichi limefanikiwa kukamata silaha ndogo bastola aina ya Star ambayo haikuwa na namba za usajili na risasi nne ndani ya magazine.

Katika tukio hilo lililotokea tarehe 1 Novemba 2018 majira ya saa 22:15 huko maeneo ya Kijichi Mgeninani askari wakiwa doria walitilia mashaka waendesha pikipiki yenye usajili wa namba MC 854 BBY aina ya TVS iliyokuwa ikiendeshwa na mtu mmoja huku akiwa amepakia watu wengine wawili.

Askari walipowasimamisha watu hao walikataa kutii amri halali na ghafla watu hao walifyatua risasi hewani ndipo Polisi walijibu mapigo na kuwajeruhi majambazi hao ambao walifariki wakiwa wanapatiwa matibabu hospitalini. Watu hao walipekuliwa na kukutwa na silaha hiyo.

Kukamatwa kwa mtandandao wa wizi wa magari
Jeshi la Polisi Kanda Maalum ya Dar es Salaam linawashikilia watuhumiwa 14 kwa tuhuma za wizi wa magari.

Watuhumiwa hao wamekamatwa sehemu mbalimbali hapa jijini Dar es Salaam na mikoa mingine wakiwa na magari 7, Bajaji moja na pikipiki moja ya wizi vyote vimeibwa maeno mbalimbali ya Jiji la Dar es salaam.

Watuhumiwa hao ni Luckman Ramadhani (36 , Ignasi Faustine (35), Ally Shaweji (30), Stephen Mwanzalima (43), Emmanuel Mabula (42), Dismas Mfoyi (32), Nyamuhanga Matiko (29), Freeman Paul (35), Ayubu Makame (41), Erasto Nyamboneke (35), Seleman Saidi (42), Dickson Mbembaji (32), Ally Rashidi (35) na Robert Nassoro (46)

Magari yaliyokamatwa ni T 162 BLW Toyota land Cruiser MALI YA UWT-TANZANIA, STL 6434 Toyota Land Cruise MALI YA WIZARA YA AFYA, T 855 DLE Toyota Harrier, T 199 DEU Toyota Noah, T 249 DLL Toyota IST, T 255 AJG Rav4 gari hii ILIIBIWA udsm IKIWA na namba T 271 DFF, T 556 DJQ Toyota Allion ,  MC 854 BYY pikipiki aina ya  TVS Honda , MC 639 BYA Bajaji

Aidha kuna magari zaidi ya manne ambayo yamekamatwa mikoani, na yako njiani yanaletwa hapa jijini Dar es salaam kwa ajili ya uchunguzi na utambuzi.

Watuhumiwa wanahojiwa na watafikishwa mahamani kwa hatua zaidi. Jeshi la polisi linaendelea na msako mkali dhidi ya wezi wa magari na watuhumiwa wengine.
Share:

Watanzania Kufaidi Matunda Ya Reli Ya Kisasa Mwakani.....Waziri Mkuu alidhishwa na kasi ya ujenzi, Asilimia 96 ya walioajiriwa ni Watanzania


MIUNDOMBINU ni muhimu katika maendeleo ya Taifa lolote ambalo linalohitaji kusonga mbele kiuchumi, kijamii kwa sababu husaidia Serikali katika kufanikisha malengo iliyojiwekea.


Miundombinu hiyo ambayo inalenga kuboresha na kuimarisha uchumi inajumuisha ujenzi wa miradi mbalimbali ya uchukuzi na usafirishaji kama reli, barabara, viwanja vya ndege, bandari, ununuzi wa ndege na meli.

Kukosekana kwa miundombinu ya uhakika kunachangia kupanda kwa gharama za maisha kutokana na kuongezeka gharama za uchukuzi.

Katika kutambua umuhimu wa miundombinu kwenye kukuza uchumi Serikali ya awamu ya tano inayoongozwa na Rais Dkt. John Magufuli imeamua kujikita katika kuboresha miundombinu ikiwemo ujenzi wa reli ili kuhakikisha Taifa linasonga mbele kiuchumi.

Mradi huo wa ujenzi wa mfumo wa reli mpya ya kisasa (SGR) unaojengwa na Serikali kupitia Shirika la Reli Tanzania (TRC), unatekelezwa kwa awamu, ambapo awamu ya kwanza kati ya Dar es Salaam na Mwanza ina urefu wa km. 1,219.

Jumamosi, Novemba 3 mwaka huu Waziri Mkuu Kassim Majaliwa alifanya ziara ya kutembelea ujenzi wa reli hiyo kuanzia eneo la Shaurimoyo (Dar es Salaam) hadi Soga (Pwani) ambapo alisema ameridhishwa na kasi na viwango vya ujenzi huo.

Alisema kipande cha kutoka Dar es Salaam hadi Morogoro chenye urefu wa km. 300 kinatarajiwa kukamilika Novemba 2019 na kipande wa cha kutoka Shaurimoyo hadi  eneo la Pugu chenye urefu wa km. 20 ambacho kilipangwa kukamilika Julai 2019, lakini kwa kasi ya mkandarasi kitakamilika Machi 2019.

“Nimeridhishwa na kasi ya ujenzi kwa sehemu ulivyofikia pamoja na ushiriki wa Watanzania wengi katika mradi huu, tunataka muendelee kujenga kwa kasi hii na kiwango hikihiki. Kazi mnayoifanya inavutia,” alieleza.

Waziri Mkuu alisema Serikali inataka kuona malengo ya Rais Dkt. Magufuli ya kutaka kuona SGR  inakamilika kwa wakati na kuanza kutumika nchini yanatimia kwani wananchi nao watakuwa wamerahisishiwa usafiri.

Alisema kukamilika kwa ujenzi wa reli hiyo kutaimarisha biashara kati ya Tanzania na nchi jirani hususani ambazo hazijapakana bahari pamoja na kupunguza muda wa safari katika maeneo ambayo mradi huo unapita.

Pia  itasaidia katika kutunza barabara na kupunguza gharama za ukarabati wa mara kwa mara kwa sababu mizigo mingi itakuwa inasafirishwa kwa njia ya reli na maroli yatapungua barabarani, hivyo kuzifanya ziwe imara na kudumu.

Waziri Mkuu aliongeza kuwa SGR inakwenda kukuza sekta zingine za kiuchumi nchini kwa sababu nazo zinategemea uimara wa miundombinu ya usafiri wa uhakika.

Katika  sekta ya viwanda reli hiyo itasaidia kusafirisha bidhaa zinazozalishwa kwenye viwanda mbalimbali na kuwafikia watumia kwa wakati na kwa gharama nafuu.

Akizungumzia kuhusu suala la ajira katika ujenzi wa mradi wa SGR, Waziri Mkuu alisema amefarijika kusikia asilimia 96 ya watu walioajiriwa katika mradi huo ni Watanzania, amewataka wawe mabalozi wazuri.

“Watanzania mnaofanya kazi katika mradi huu, hakikisheni mnawajibika kwa kufanyakazi kwa bidii, uadilifu na muwe mabalozi wazuri ili wananchi wengine waweze kupata ajira kwenye miradi mbalimbali inayoendelea kutekelezwa nchini ikiwemo ya ujenzi.”

Kwa upande wake, Mkurugenzi Mkuu wa Shirika la Reli Tanzania (TRC), Masanja Kadogosa alisema awamu ya kwanza ya mradi huo wa reli  kutoka Dar es Salaam hadi Makutupora unagharimu sh. trilioni 7.1.

Alisema awamu hiyo ya mradi wa ujenzi wa reli hiyo yenye urefu wa km 1,219 kutoka Dar es Salaam hadi Mwanza umegawanyika katika vipande vitano, kipande cha kwanza ni kutoka Dar es Salaam hadi Morogoro chenye urefu km 300 na njia kuu 205 ambazo km 95 zitakuwa zinapisha kitagharimu sh. trilioni 2.7.

“Kipande kingine ni kutoka Morogoro hadi Makutupora chenye urefu wa km. 422  na njia kuu 336 ambazo km 86 zitakuwa zinapishana kitagharimu sh. trilioni 4.4, Makutupora hadi Tabora km. 376.5 chenye njia kuu 294 na km 73.5 zitakuwa zinapishana.

Kipande kingine ni cha kutoka Tabora hadi Isaka km 162.5 chenye njia kuu 130 na km 32.5 zitakuwa za kupishana na Isaka hadi Mwanza km. 311.25 njia kuu 249 huku km 62.5 zitakuwa za kupishana.”

Mkurugenzi huyo alisema kukamilika kwa reli hiyo ya kisasa itachochea mipango ya Serikali ya awamu ya tano katika kutekeleza sera ya Tanzania ya viwanda na kulifikisha Taifa kwenye uchumi wa kati ifikapo mwaka 2025.

Pia Mkurugenzi huyo alisema reli hiyo itachochea mapinduzi ya kiuchumi kwa kanda nzima ya Afrika Mashariki na Kati hususan kwa nchi zisizopakana na bahari kwani watasafirisha mizigo yao kwa haraka na uhakika.

“Kuchangia katika pato la Taifa na sera ya viwanda kwani mradi huo umeongeza mahitaji ya saruji, kokoto, nondo pamoja na vifaa vingine vya ujenzi, hivyo kuvifanya viwanda vyetu vya ndani kupata soko la bidhaa zake.”

Akizungumzia mradi huo kwa ujumla, Mkurugenzi huyo alisema maendeleo ya mradi huo ni asilimia 32 kwa kipande cha Dar es Salaam-Morogoro na asilimia 3. 31 kwa kipande cha Morogoro-Makutupora.

Alisema jumla ya km. 722 za ujenzi wa mradi wa reli ya kisasa kwa sasa zinatekelezwa katika vipande viwili, kipande cha Dar Es Salaam-Morogoro km. 300 kinajengwa kwa ubia wa kampuni ya YAPI MERKEZI ya Uturuki na MOTA-ENGIL ya Ureno na kipande wa Morogoro-Makutupora km. 422 kinajengwa na kampuni ya YAPI MERKEZI.

Kadogosa alisema katika mradi huo wa reli za kisasa mfumo wa uendeshaji wa treni utatumia nishati ya umeme kutoka Shirika la Umeme Tanzania (TANESCO) na tayari taratibu za kumpata mkandarasi za kujenga njia za umeme upo katika hatia za mwisho.

Kuhusu ujenzi wa madaraja Kadogosa alisema kazi ya ujenzi wa madaraja na makaravati unaendelea ambapo daraja refu katikati ya jiji la Dar es Salaam ina jumla ya urefu wa km. 2.56 na ujenzi wake umefikia asilimia 46.

 “Kuna madaraja ya kati 26 na makaravati 243, madaraja ya treni kupita juu yapo 17, madaraja ya treni kupita chini yapo 15 na madaraja reli juu ya reli yapo matano, pia jumla ya stesheni sita zitajengwa kati ya Dar es Salaam na Morogoro, kati ya hizo kubwa zitakuwa mbili na nne zitakuwa ndogo.”

Alisema usanifu wa stesheni hizo umezingatia mazingira na asili ya Tanzania ambapo stesheni ya Dar es Salaam ina sura ya madini adimu ya Tanzanite wakati stesheni za kati usanifu wake umezingatia utamaduni na nyumba za asili na stesheni ya Morogoro itaonesha uhalisia wa milima ya Uruguru.

Kadhalika, Mkurugenzi huyo alizungumzia kuhusu ajira katika mradi huo ambapo alisema una jumla ya wafanyakazi 5,440, vibarua 4,743 ambapo jumla ya asilimia 96 ni Watanzania na asilimia nne ni wageni, wataalamu 189 wa Kitanzania na 258 wa kigeni kwa uwiano wa asilimia 42 Watanzania na wageni asilimia 58.

Pia jumla ya ajira 626 za Watanzania wasio na utaalamu na 19 za wenye utaalamu zimepatikana kupitia kampuni za wazawa (sub-contractors) wanaoshiriki moja kwa moja kwenye mradi huo.

Akizungumzia kuhusu ardhi na mali nyingine, Kadogosa alisema mali za wananchi wapatao 6,514 zenye thamani ya kiasi cha sh. bilioni 83.099 zitakiwa kuhamishwa ili kupisha ujenzi wa reli kwa kipande wa Dar es Salaam-Morogoro.

IMETOLEWA NA:
OFISI YA WAZIRI MKUU,
JUMANNE, NOVEMBA 6, 2018.
Share:

IDADI YA WASOMAJI

TUSIKILIZE LIVE KUPITIA TUNEIN

UNGANA NASI FACEBOOK HAPA

10 ZILIZOSOMWA ZAIDI

Labels

Blog Archive