HALMASHAURI YA MJI WA KAHAMA KUGAWA VYANDARUA VYENYE DAWA KWA WANAWAKE NA WATOTO WANAOFIKA KLINIKI


Na Ndalike Sonda
KAHAMA.

Halmashauri ya Mji wa KAHAMA imeanzisha utaratibu wa kugawa vyandarua vyenye dawa kwa wanawake na watoto wanaofika klinik katika hospitali ya Halmashauri hiyo ili kuhamasisha matumizi ya vyandarua na hivyo kupunguza vifo vitokanavyo na Ugonjwa wa malaria.

Akizungumza kwenye kipindi cha Raha ya Leo, cha KAHAMA FM, kaimu Mratibu wa Malaria wa halmashauri hiyo Dkt. HEMED BIHEMO amesema utaratibu huo umetokana na ongezeko la ugonjwa huo katika halmashauri hiyo.

Amesema, kipindi cha kuanzia mwezi Disemba 2017 hadi April Mwaka huu, Halmashauri hiyo ikuwa na asilimia 31 ya wagonjwa wa malaria ikilinganishwa na kipindi kama hicho mwaka jana ambayo ilikuwa ni asilimia 25.

Dkt. BIHEMO amesema kundi la watoto na wanawake wajawazito ndio wameonekana kuongoza kuugua ugonjwa huo na kwamba idadi hiyo inatokana na makundi hayo kuwa tayari kupima ugonjwa huo tofauti na wanaume ambao wamekuwa hawafanyi vipimo.

Halmashauri ya mji wa Kahama inajumla ya vituo 13 vya umma na 21 vya binafsi vinavyotumika kupima ugonjwa huo idadi ambayo inatajwa kuwa ni ndogo ikilinganishwa na wingi wa watu katika halmashauri hiyo.
Share:

No comments:

Post a Comment

IDADI YA WASOMAJI

TUSIKILIZE LIVE KUPITIA TUNEIN

UNGANA NASI FACEBOOK HAPA

10 ZILIZOSOMWA ZAIDI

Labels