ASKARI WA JWTZ ASHIKILIWA NA JESHI LA POLISI KWA TUHUMA YA KUSABABISHA VIFO VYA WATU WAWILI BBAADA YA KUWAGONGA NA GARI.


Na Salvatory Ntandu
KAHAMA.

Mkazi wa Old Shinyanga mkoani SHINYANGA, PHINEHAS CHOGELO (29) ambaye pia ni Askari wa Jeshi la Wananchi Tanzania (JWTZ) anashikiliwa na jeshi la polisi kwa Tuhuma ya kusababisha vifo vya watu wawili baada ya kuwagonga kwa gari.

Kwa Mujibu wa Kamanda wa polisi mkoa wa SHINYANGA SIMON HAULE, tukio hilo limetokea Aprili 8 mwaka huu, majira ya saa tano asubuhi katika eneo la Ibinzamata barabara itokayo Shinyanga mjini kuelekea Tinde, Shinyanga vijijini.

Amesema gari T. 105 DGQ Subaru Forester likiendeshwa na CHOGELO liliigonga pikipiki aina ya San Lg namba za T. 974 BSL iliyokuwa ikiendeshwa na YAHYA NASORO(36) mkazi wa Kitangili aliyekuwa amempakia CATHERINE MWIGULU(35) mkazi wa Nhelegani na kuwavunja miguu yao ya kulia.

Amefafanua kuwa CHOGELO pia alimgonga mwendesha baiskeli STEVEN JOSEPH(25), mkazi wa Isela aliyekuwa amempakia NEMEM JOSEPH(26) mwanafunzi wa Chuo cha Uuguzi Kolandoto, na kusababisha vifo vyao wakati wakipatiwa matibabu katika hospitali ya rufaa ya mkoa wa Shinyanga.

Kamanda HAULE amesema chanzo cha ajali hiyo ni mwendokasi wa gari husika na kwamba mtuhumiwa anashikiliwa na polisi kwa mahojiano zaidi na vielelezo vipo kituoni.

Share:

No comments:

Post a Comment

IDADI YA WASOMAJI

TUSIKILIZE LIVE KUPITIA TUNEIN

UNGANA NASI FACEBOOK HAPA

10 ZILIZOSOMWA ZAIDI

Labels