AFIKISHWA MAHAKAMANI KWA KOSA LA KUINGIA NCHINI KINYUME CHA SHERIA


Na Lilian Katabaro
KAHAMA.

Raia wa Rwanda, NIYOMUGABO PASIFIQUE (21), amefikishwa katika Mahakama ya Wilaya ya KAHAMA kwa tuhuma ya kuingia na kuwepo nchini kinyume cha sheria.

Mbele ya Hakimu Mkazi wa Mahakama hiyo IMANI BATENZI, mwendesha mashitaka wa Idara ya ya Uhamiaji SALUM RASHIDI, amesema NIYOMUGABO alikamatwa March 6 mwaka katika mtaa wa Mwime wilayani Kahama akiwa hana kibali kinachomruhusu kuwepo nchini.

SALUM amesema katika shauri hilo la jinai namba 146/2018, NIYOMUGABO ametenda kosa hilo kinyume na kifungu namba 45 na kifungu cha pili cha sheria ya Uhamiaji namba 7 ya mwaka 1995 iliyofanyiwa marekebisho mwaka 2016.

NIYOMUGABO amekana kutenda kosa hilo na upelelezi wa shauri hilo umekamilika na hoja za awali zitasikilizwa Mahakamani hapo April 10 mwaka huu na amerudishwa rumande kwa kukosa dhamana.
Share:

No comments:

Post a Comment

IDADI YA WASOMAJI

TUSIKILIZE LIVE KUPITIA TUNEIN

UNGANA NASI FACEBOOK HAPA

10 ZILIZOSOMWA ZAIDI

Labels