UHABA WA VYUMBA VYA MADARASA SHULE YA MSINGI NYAHANGA YAWA CHANG.AMOTO KWA WANAFUNZI


Na Salvatory Ntandu
KAHAMA.

Uhaba wa vyumba vya Madarasa katika Shule tatu za Msingi zilizopo katika Kata ya NYAHANGA, Halmashauri ya Mji wa KAHAMA huenda ukasababisha wanafunzi kutofanya vizuri katika masomo yao.

Hayo yamebainishwa jana na diwani wa Kata hiyo, MICHAEL MAGILE wakati akizungumza na wananchi kwenye mkutano wa hadhara kuhusiana na namna watakavyojipanga kutatua tatizo hilo kwa kuchangia.

Amesema endapo wananchi watakubali kuchangia maendeleo ya shule kwa hiari wataweza kujenga vyumba vya madarasa vya kutosha na kumaliza tatizo la upungufu wa vyumba vya madarasa katika kata hiyo.

Awali akiwasilisha taarifa ya shule hizo, Afisa elimu kata ya Nyahanga HELENA KABOYA amesema kata hiyo inaupungufu wa vyumba vya madarasa 81 kwa shule zake tatu ambazo ni shule ya Msingi Nyahanga A,B na Shunu.

Amesema katika shule ya Msingi Nyahanga A vinahitajika vyumba vya madarasa 31 ambapo vilivyopo ni 12 na pungufu ni 19.

Amesema katika shule ya Nyahanga B vinahitajika vyumba 37 wakati vilivyopo ni 14 na upungufu ni vyumba 23, huku shule ya Shunu ikihitaji vyumba 47 vilivyopo ni 8 na pungufu ni 34.

Nao baadhi ya wananchi waoshiriki katika Mkutano huo BUNDALA SENGASENGA na SELEMAN KIJA wamesema endapo viongozi wa kata hiyo wataondoa tofauti zao binafsi, wananchi wakotayari kuchangia maendeleo ya kata hiyo.

Kata ya Nyahanga ina jumla ya shule za msingi saba ambapo tatu ni za serikali na 5 ni za binafsi
Share:

No comments:

Post a Comment

IDADI YA WASOMAJI

TUSIKILIZE LIVE KUPITIA TUNEIN

UNGANA NASI FACEBOOK HAPA

10 ZILIZOSOMWA ZAIDI

Labels