KAHAMA.
Uongozi wa Kata ya Igunda Halmashauri ya USHETU wilayani KAHAMA Mkoani SHINYANGA umeahidi kuendelea kuweka miundombunu rafiki kwenye gulio la Kijiji cha Mhulidede ili wafanyabiashara na wananchi walitumie bila kupata adha yoyote.
Akizungumza wakati wa uzinduzi wa soko hilo Diwani wa Kata ya Igunda, TABU KATOTO amesema wataongeza msukumo wa kupeleka huduma muhimu katika gulio hilo huku Kaimu Afisa Mtendaji wa kata hiyo EVODIUS MWESIGE, akiwataka wananchi kutumia gulio hilo kujiimarisha kiuchumi.
Nao baadhi ya wananchi wa Kijiji cha Mhulidede, wameipongeza serikali ya kijiji hicho kwa kuweka gulio ambalo litawasaidia kubuni biashara mbalimbali za kuwaingizia kipato.
Akizungumza kwa niaba ya wafanyabiashara wenzake katika gulio hilo, WILIAM JOSEPH amesema wamekusudia kujipanga ili kuomba mikopo mbalimbali kwa halmashauri ya Ushetu, kwa lengo la kujiimrisha biashara.
Gulio la Kijiji cha Mhulidede limefunguliwa rasmi leo ambapo litakuwa likifanyika kila siku ya jumatatu katika kijiji hicho.
No comments:
Post a Comment