WAKAZI WA MALUNGA HALMASHAURI YA MJI WA KAHAMA WALALAMIKIA UBOVU WA KARAVATI LILILOPO JIRANI NA OFISI YA KATA


Na Ndalike Sonda
KAHAMA.

Wananchi wa kata ya Malunga katika Halmashauri ya Mji wa KAHAMA Mkoani SHINYANGA wamelalamikia ubovu wa karavati lililopo jirani na ofisi ya Kata hiyo kutokana na kuchimbuliwa na mvua zinazoendelea kunyesha katika maeneo mengi ya mji wa Kahama.

Wakizungumza kwenye kipindi cha Raha ya Leo cha KAHAMA FM, baadhi ya wananchi wamesema kutokana na ubovu wa barabara hiyo kwa sasa ajali nyingi zimekuwa zikitokea ikiwamo magari kuzama na kusababisha msongamano mkubwa wa watumiaji wa barabara hiyo.

Naye Mwenyekiti wa Mtaa wa Korogwe katika kata hiyo ya Malunga, EDWARD MBELELE amekiri kushuhudia ajali mbili katika eneo hilo kwa kuwa ni jirani na ofisi yake ambapo amesema suala hilo wamelifikisha kwenye kikao cha maendeleo ya kata (WDC).

Meneja wa wakala wa barabara mijini na vijijini (TARURA) katika halmashauri ya Mji wa Kahama, JOB MUTAGWABA amekiri kupokea taarifa ya ubovu wa karavati hilo na kwamba wako katika hatua ya kulirekebisha.

Aidha amesema kutokana na mvua zinazoendelea kunyesha katika wilaya ya Kahama, barabara nyingi zimeharibika na kwamba wanakusudia kuziimarisha baada ya masika kumalizika na kuwataka wananchi wawe na subira.
Share:

No comments:

Post a Comment

IDADI YA WASOMAJI

TUSIKILIZE LIVE KUPITIA TUNEIN

UNGANA NASI FACEBOOK HAPA

10 ZILIZOSOMWA ZAIDI

Labels