WANANCHI WA BUKONDAMOYO WILAYANI KAHAMA WAUNGANA KUTENGENEZA MITARO YA BARABARA

Image result for PICHA WANANCHI WAKIJENGA MITARO
Na Ndalike Sonda
KAHAMA.

Wananchi wa Kitongoji cha Mlimani Katika Mtaa wa Bukondamoyo, Kata ya Mhungula Mjini KAHAMA kwa pamoja wameungana kutengeneza barabara kwa kujenga mitaro na kumwaga vifusi katika maeneo korofi ili kupata barabara ya uhakika inayofika hadi kwenye makazi yao.

Wakizungumza leo na KAHAMA FM, baadhi ya wananchi hao, wamesema wameamua kutengeneza barabara hiyo baada ya eneo la shule kupandwa miti na hivyo kuwa na usumbufu mkubwa wa barabara inayounganisha kitongoji hicho na barabara kuu inayokwenda mjini Kahama.

Wananchi hao, JENNY GINDON, PETER MASANJA, na SELESTINA MICHAEL mbali na kujitolea kutengenza barabara hiyo, wameiomba serikali kuwasaidia kuboresha barabara hiyo kwa kuweka makaravati yatakayosaidia kupitsisha maji yanayotoka Mlimani.

Naye Mwenyekiti wa Mtaa wa Bukondamoyo, NASHON YOHANA amesema Kukamilika kwa barabara hiyo itasaidia kupunguza adha wanayoipata kwa sasa wananchi wa mtaa huo, na kwamba hadi sasa wananchi wamechangia zaidi ya shilingi laki tano kwaajili ya kuboresha barabara hiyo.

Hii ni mara ya Pili kwa wananchi wa Mtaa wa Bukondamoyo kujitolea kutengeneza barabara ambapo hivi karibuni walishiriki kumwaga vifusi vya changalawe kwenye karavati lililopo Kitongoji cha Pugu katika mtaa huo ili kuunganisha mawasiliano ya barabara.
Share:

No comments:

Post a Comment

IDADI YA WASOMAJI

TUSIKILIZE LIVE KUPITIA TUNEIN

UNGANA NASI FACEBOOK HAPA

10 ZILIZOSOMWA ZAIDI

Labels