Rais Magufuli atuma salamu za rambirambi za ajali kivuko cha MV- Nyerere Iliyoua Watu 44

 
Rais John Magufuli ametuma salamu za rambirambi na pole kutokana na ajali ya kivuko cha Mv Nyerere kilichozama jana mchana  Septemba 20,2018 huku watu 44 mpaka sasa wakiripotiwa kufariki dunia.

Kivuko hicho kilikuwa kinatoka Bugorora kwenda Ukara katika Ziwa Victoria kilizama kikidaiwa kuwa na watu zaidi ya 100.

Rais Magufuli ametoa salamu hizo  jana usiku saa 20:40   kupitia kwa Mkurugenzi wa Mawasiliano ya Rais- Ikulu, Gerson Msigwa aliyepiga simu Shirika la Utangazaji Tanzania (TBC) wakati wa taarifa ya habari.

“Rais anatoa pole kwa familia, ndugu, jamaa na marafiki waliofikwa na ajali,” alisema Msigwa

Msigwa alisema, “Rais anaomba Watanzania kuwa watulivu wakati juhudi za uokoaji zinaendelea na baadaye Serikali itaweza kutoa taarifa ya nini kitakachoendelea.”
Share:

No comments:

Post a Comment

IDADI YA WASOMAJI

TUSIKILIZE LIVE KUPITIA TUNEIN

UNGANA NASI FACEBOOK HAPA

10 ZILIZOSOMWA ZAIDI

Labels

Blog Archive