
Serikali
 imesema itaendelea kushirikiana na wadau wa maendeleo nchini ili 
kuhakikisha kila mtoto wa kitanzania anapata elimu bora.
Hayo
 yameelezwa leo Jijini Dodoma na Waziri wa Elimu Sayansi na Teknolojia, 
Mhe. Prof. Joyce Ndalichako alipokuwa akifungua Mkutano Mkuu wa Mwaka wa
 Wadau wa Elimu wa kujadili mafanikio na changamoto za elimu nchini.
“Mkutano
 huu ni muhimu sababu unapitia na kujadili mafanikio na changamoto 
katika sekta ya elimu na kutoa mapendekezo ya changamoto hizo ili 
kuboresha sekta hii,” amesema Prof. Ndalichako.
Aidha,
 amesema Serikali itaendelea kutumia mapendekezo yanayotolewa na wadau 
wa maendeleo ya elimu nchini ili kuhakikisha hakuna mtoto wa Kitanzania 
anaachwa nyuma katika kupata elimu bora mijini na vijijini.
Amesema,
 Serikali ya Awamu ya Tano imekuwa na mafanikio makubwa katika sekta ya 
elimu ambapo imefanikiwa kutoa elimu bila malipo kwa shule za msingi na 
sekondari, mafunzo kwa mbalimbali kwa walimu, walimu wamepangiwa kazi 
kulingana na uhitaji pamoja na kuendelea kuwaajiri.
Vile vile Wadhibiti Ubora wa Elimu wamewezeshwa kwa kununuliwa magari na pikipiki ili kuzifikia shule kwa urahisi.
Prof.
 Ndalichako amewataka wadau hao kuutumia mkutano huo kujadili na kutoa 
mapendekezo ya namna ya kuimarisha ufundishaji wa masomo ya sayansi, 
kuunganisha elimu ya nadharia na vitendo, mafunzo ya walimu, elimu yenye
 usawa mijini na vijijini pamoja na mahudhurio shuleni.
Kwa
 upande wake, Katibu Mkuu wa Wizara ya Elimu Sayansi na Teknolojia, Dkt.
 Leonard Akwilapo amesema mkutano huo umehusisha wadau mbalimbali wa 
elimu hapa nchini zikiwemo taasisi za utafiti, wadau wa maendeleo ya 
elimu, maafisa elimu pamoja na wanafunzi ambapo kwa pamoja watajadili 
mafanikio na changamoto katika sekta ya elimu na kutoa mapendekezo ya 
namna ya kukabiliana na changamoto hizo.






No comments:
Post a Comment