SHULE ZA MSINGI TATU ZAFUNGWA WILAYANI KAHAMA KWA AJILI YA MVUA ZINAZOENDELEA KUNYESHA

Image result for SHULE ZILIZOJAA MAJI
Na Amina Mbwambo
KAHAMA.

Kamati ya Maafa ya wilaya ya KAHAMA mkoani Shinyanga imelazimika kuzifunga shule tatu za msingi katika kata ya Jana Halmashauri ya Msalala baada ya kuzungukwa na maji kufuatia mvua kubwa zilizonyesha sehemu mbalimbali wilyani humo.

Mwenyekiti wa kamati hiyo Mkuu wa Wilaya ya Kahama, FADHILI NKURLU amesema wamelazimika kuifunga shule ya Izuga yenye wanafunzi 525, Kadati yenye wanafunzi 348 na Matindye yenye wanafunzi 355 kuanzia kesho Aprili 19 hadi Aprili 30, mwaka huu.

NKURLU amesema katika Halmashauri ya Ushetu watu wanne wamejeruhiwa baada ya kuangukiwa na ukuta wa nyumba katika kijiji cha Mbika, huku nyumba 74 zikibomolewa katika kata ya Uyogo na daraja kusombwa na maji katika kata ya Bulungwa.

Taarifa zaidi kutoka halmashauri ya Ushetu zinabainisha kuwa mawasiliano ya barabara kati ya mji wa Kahama na kata za Ulewe, Nyankende na Ubagwe kupitia kata ya Bulungwa katika Halmashauri hiyo, yamekatika kufuatia mvua kubwa iliyonyesha usiku wa kuamkia leo.

Akiongea na Kahama fm kutoka Bulungwa, mkazi wa mjini Kahama, MARCO MIPAWA ambaye ni miongoni mwa watu walioshindwa kusafiri kufuatia mvua hizo, amesema daraja la Kabanga katika kata ya Sabasabini, Halmashauri ya Ushetu limefunikwa maji na kusababisha magari kushindwa kupita.

Kufuatia hali hiyo, Mkuu wa wilaya ya Kahama, NKURLU wameuagiza wakala wa barabara za mjini na vijijini (TARURA), kuchukua hatua za haraka kuhakikisha mawasiliano yanarejea, huku akiwasihi Wananchi kuchukua tahadhari dhidi ya mvua zinazoendelea kunyesha kuepuka madhara.
Share:

No comments:

Post a Comment

IDADI YA WASOMAJI

TUSIKILIZE LIVE KUPITIA TUNEIN

UNGANA NASI FACEBOOK HAPA

10 ZILIZOSOMWA ZAIDI

Labels