SERIKALI YASEMA BADO KUNA UTOROSHAJI MWINGI WA DHAHABU MIGODI YA SHINYANGA



Na Ndalike Sonda
KAHAMA.

Serikali imesema bado kuna utoroshaji mwingi wa dhahabu katika machimbo madogo Mkoani SHINYANGA hali inayosababisha serikali kukosa mapato mengi ambayo yangesaidia kuboresha huduma mbalimbali za jamii.

Hayo yameelezwa Mjini KAHAMA na Naibu waziri wa Madini, DOTTO BITEKO wakati akizungumza na wachimbaji na wachenjuaji wa madini wa mkoa wa Shinyanga kwenye semina ya kujadili usalama mahala pa kazi.

Amesema kuanzia mwezi June 2016 hadi Februari mwaka huu, wachimbaji wadogo mkoani Shinyanga wamezalisha kilo 555.7 za dhahabu (sawa na shilingi milioni 45), kiwango ambacho amesema kipo chini ukilinganishwa na uzalishwaji.

BITEKO amesema wachimbaji wa madini wanazidiwa na wachimbaji wa kokoto na mchanga ambao mwaka jana wamechimba tani milioni 15 na kulipa mrabaha shilingi wa biloni 7.5 serikalini.

Wakizungumza na waandishi wa Habari baadhi ya wachimbaji na wachenjuaji wameshauri kuongezwa udhibiti dhidi ya utoroshaji madini hayo pamoja na kupunguza tozo na kodi mbalimbali kwa wachimbaji wadogo kwa manufaa ya serikali na wachimbaji hao.
Share:

No comments:

Post a Comment

IDADI YA WASOMAJI

TUSIKILIZE LIVE KUPITIA TUNEIN

UNGANA NASI FACEBOOK HAPA

10 ZILIZOSOMWA ZAIDI

Labels