WAFANYABIASHARA WA SOKO LA NAMANGA HALMASHAURI YA MJI WA KAHAMA WAPO HATARINI KUKUMBWA NA MLIPUKO WA MAGONJWA

Image result for WAFANYABIASHARA WALIO KATIKA HALI MBAYA
Na Ndalike Sonda
KAHAMA.

Wafanyabiashara na wananchi waliopo katika soko la Namanga Mjini KAHAMA wapo hatarini kukumbwa na mlipuko wa magonjwa kutokana na kukithiri kwa mlundikano wa taka katika milango ya kuingia na kutoka sokoni hapo.

Wakizungumza kwenye kipindi cha Raha ya leo, Baadhi ya wafanyabiashara na wananchi wamesema harufu mbaya imekuwa ikitoka katika uchafu huo na kwamba hali hiyo inatokana na uchafu huo kuchukua muda mrefu pasiko kuzolewa.

Kutokana na hali hiyo wameiomba serikali kuingilia kati, ili kudhibiti mlundikano wa uchafu huo na kwamba imekuwa ni kero kwa wananchi waishio jirani na soko hilo pomoja na wanafunzi wa shule ya Msingi Kilima A na B.

Mmoja wa viongozi wa katika Eneo hilo (NZENGO), HAMIS SAID amesema wamekuduia kuandika barua kwa Mkurugenzi Mtendaji wa Mji wa Kahama ili kumuomba afike eneo hilo kujionea hali halisi.

Naye Katibu wa Soko la Namanga, WILLIUM CHALYA amesema uchafu huo umekaa zaidi ya wiki mbili na kwamba wameweka ulinzi ili kudhibiti wananchi wasiendelee kutupa taka eneo hilo.

Soko la Namanga ni Soko linalohudumia idadi kubwa ya watu katika halmashauri ya mji wa Kahama kwa sasa ambapo lina zaidi ya wafanyabishara 1500 wanaofanya biashara zao ndani ya soko hilo.
Share:

No comments:

Post a Comment

IDADI YA WASOMAJI

TUSIKILIZE LIVE KUPITIA TUNEIN

UNGANA NASI FACEBOOK HAPA

10 ZILIZOSOMWA ZAIDI

Labels