KIJANA ANAYEDHANIWA KUTAPELI NYAMA BUCHANI ANUSURIKA KIFO


Na Ndalike Sonda
KAHAMA.

Mkazi wa Nyahanga Mjini KAHAMA RAMADHAN HAMIS (36) amenusurika kuuawa na wananachi wenye hasira kali baada ya kutuhumiwa kuiba nyama katika chucha Moja iliyopo Mtaa wa Nyahanga.

Tukio hilo hilo limetokea leo majira ya saa tatu asubuhi ambapo RAMADHAN anadaiwa kufika katika bucha hiyo na kuomba apimiwe nusu kilo ya Nyama yenye thamani ya Shilingi 3000.

Akizungumza na KAHAMA FM, Muuzaji wa bucha Hiyo JOHN JOSEPH amesema Mtuhumiwa (RAMADHAN) huyo alifika katika bucha hiyo na kumwambia kuwa ampimie kiasi hicho cha nyama ili ampeleke kwenye hoteli ya mke wake iliyopo jirani na bucha hiyo ambapo pia aliomba pesa aifuate hapo.

Alisema baada ya kumpimia Nyama mtuhumiwa (RAMADHAN) alikwenda kwenye hoteli hiyo na kisha kutoka pasipo kulipa ambapo alimuomba alipe pesa hiyo kama alivyoahidi ambapo alianza kukimbia na ndipo wananchi walipoanza kumfukuza na kisha kumkamata.

Naye RAMADHAN ambaye ni Mtuhumiwa amesema amekuwa akienda akukopa kwenye bucha hiyo kwa kutokana na muuzaji wa zamani aliyemuita MURA, hivyo ni kama mazoea kwake kwenda pale kukopa na kulipa baadaye.

Mmoja wa Mashuhuda ERIC JOHN ambaye anaegesha pikipiki eneo hilo, amesema hajawahi kumuona katika eneo hilo mtuhumiwa huyo na kwamba alifika asubuhi akanunua pombe ya shilingi 1000, katika duka moja lililopo eneo hilo ambapo baada ya kudaiwa pesa aliamua kuacha simu yake kama mdhamana.

Hata hiyo wanawake wanauza hoteli katika eneo hilo wamesema hawamjui mtuhumiwa huyo na kwamba alifika hapo kisha kuondoka huku akiwaambia kuwa ni fundi ujenzi ambapo kunavijana wake watakuja kunywa chai baadaye.

Hata hivyo msamaria Mmoja alimlipia kiasi hicho cha fedha kwenye bucha hiyo pamoja na kwenye duka analodaiwa kisha wananchi wakamuachia akaenda zake.

Share:

No comments:

Post a Comment

IDADI YA WASOMAJI

TUSIKILIZE LIVE KUPITIA TUNEIN

UNGANA NASI FACEBOOK HAPA

10 ZILIZOSOMWA ZAIDI

Labels