JESHI LA POLISI MKOANI SHINYANGA LAENDELEA KUFANYA UCCHUNGUZI WA MAUAJI YA SHOMA MWENYE UMRI WA MIAKA 70

Na Sebastian Mnakaya
SHINYANGA.

Jeshi la polisi mkoani SHINYANGA, linaendelea kufanya uchunguzi katika tukio la mauaji ya mwanamke aitwaye, SHOMA SHIJA mwenye umri wa miaka 70 yaliyotokea juzi katika kijiji cha Shabuluba kata ya Busanda wilaya ya Shinyanga pamoja na vifo vingine vya watu wawili.

Kamanda wa polisi wa Mkoa huo, SIMON HAULE amewaambia wandishi wa habari kuwa tukio hilo limetokea juzi usiku wakati marehemu SHOMA akiwa nyumbani kwake ambapo alivamiwa na watu ambao idadi yao haikuweza kufahamika.

Katika tukio lingine lililotokea jana asubuhi katika mtaa wa Muhungula mjini Kahama, Kamanda HAULE amesema, mwanafunzi wa darasa la tatu katika shule ya msingi Nyahanga, DANIEL YOHANA MAZIKU mwenye miaka 9 amegundulika akiwa amefariki dunia baada ya kutumbukia kwenye karo.

Kamanda HAULE ameongeza kuwa katika manispaa ya Shinyanga mwanafunzi wa kidato cha pili katika shule ya sekondari Mwasele aliyetambulika kwa jina la HAPPINESS amegundulika amefariki dunia baada ya kujinyonga kwa kutumia kamba aliyoifunga katika dari la nyumba aliyokuwa anaishi na wazazi wake.

Kamanda HAULE ametoa rai kwa wazazi na walezi kuchukua tahadhari kubwa ya kuwatunza, kuwalinda na kuwafuatilia watoto wao hususan katika kipindi hiki cha msimu wa mvua.

Amesema jamii ni vizuri pia ikawa karibu na watoto na vijana ili kujua shida na changamoto zinazowakabili ili kuchukua hatua za kuwashauri na kuwatia moyo wa matumaini pale wanapokata tamaa ya maisha.

Share:

No comments:

Post a Comment

IDADI YA WASOMAJI

TUSIKILIZE LIVE KUPITIA TUNEIN

UNGANA NASI FACEBOOK HAPA

10 ZILIZOSOMWA ZAIDI

Labels