Rais
 Mstaafu wa awamu ya tatu, Mhe. Benjamin William Mkapa ambaye ni 
msuluhishi wa mgogoro wa Burundi akiwa katika chumba cha wageni maalum 
katika uwanja wa Ndege wa Entebbe leo. kulia ni Mwambata Jeshi wa 
Ubalozi wa Tanzania nchini Uganda, Brig Gen. Mkumbo, kushoto ni Msaidizi
 wa Rais Mkapa katika utatuzi wa mgogoro huo, Balozi David Kapya na 
anayemfuatia ni Balozi wa Tanzania nchini Uganda, Mhe. Dkt. Aziz Mlima. 
Mkapa
 aliwasili katika Uwanja wa Ndege wa Entebbe asubuhi ya tarehe 19 
Novemba 2018 kwa ajili ya kuwasilisha ripoti ya mkutano wa upatanishi 
uliofanyika hivi karibuni jijini Arusha kwa Mpatanishi Mkuu wa mgogoro 
huo Rais wa Uganda, Mhe. Yoweri Kaguta Museveni. 
Balozi
 wa Tanzania nchini Uganda, Mhe. Dkt. Aziz Mlima (kushoto) akimsikiliza 
Rais Mstaafu wa awamu ya tatu, Mhe. Benjamin William Mkapa ambaye ni 
msuluhishi wa mgogoro wa Burundi. 






No comments:
Post a Comment