Wakili
 wa Serikali kutoka Taasisi ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa (Takukuru),
 Leonard Swai, amedai mahakamani kwamba wamemaliza kumhoji kigogo wa 
IPTL, Harbinder Sethi baada ya kuomba mahakamani kufanya hivyo.
Swai
 amedai hayo leo Alhamisi Novemba  8, katika Mahakama ya Hakimu Mkazi 
Kisutu mbele ya Hakimu Mkazi Mkuu, Huruma Shaidi wakati kesi hiyo 
inatajwa.
Alidai
 upelelezi wa kesi hiyo ya kutakatisha fedha inayomkabili Sethi na James
 Rugemarila haujakamilika isipokuwa walipata nafasi ya kumuhoji Sethi.
Swai aliomba mahakama ipange tarehe nyingine ya kesi kutajwa na upelelezi unaendelea.
Mahakama iliahirisha kesi hiyo hadi Novemba 22 mwaka huu kwa ajili ya kutajwa. Watuhumiwa hao bado wanaendelea kusota rumande






No comments:
Post a Comment