Jeshi
la Ulinzi la Wananchi wa Tanzania (JWTZ) wanatarajia kuwa wenyeji wa
zoezi la mafunzo yaitwayo Ushirikiano imara 2018 litakaloshirikisha nchi
za Afrika Mashariki zikiwemo Burundi, Rwanda, Kenya na Uganda ambapo
mafunzo yataendeshwa mkoani Tanga .
Akizungumza
na wanahabari jijini Dar es salaam Mkuu wa Mafunzo na Operesheni
(JWTZ) Meja Jenerali Alfred Fabian Kapinga amesema kuwa, zoezi hilo ni
la medani na litafanyika katika wilaya za mijini pamoja na Wilaya ya
Muheza mkoani Tanga.
Ameeleza
kuwa zoezi hilo litaanza rasmi tarehe 05 mpaka 21, sambamba na hilo
mafunzo hayo yatalenga kujenga uwezo wa kukabiliana na uharifu pamoja na
majanga.
Pia
amesema kuwa dhumuni la zoezi hilo kikanda ni kubadilishana uzoefu wa
kiutendaji, kuimarisha mahusiano baina ya nchi, majeshi ya Afrika
Mashariki pamoja na taasisi zingine za kiraia ambazo zitashiriki zoezi
hilo.
Sanjari
na hilo kutakuwa na kazi za kusaidia jamii katika shughuli mbalimbali
zikiwemo ujenzi wa madarasa, ofisi za walimu pamoja na vyoo katika Shule
ya msingi ya Machemba iliyopo Wilaya ya Muheza mkoani Tanga, pia
kutakuwa na utoaji wa huduma za tiba kwa wananchi katika eneo la zoezi.
Hivyo,
Meja Fabian ametoa rai kwa wakazi wa Tanga kuonyesha ukarimu pamoja na
amani baina ya wageni watakaokua kwa kipindi chote cha mafunzo kama
walivoonyesha mwaka jana ambapo mafunzo yalikua yakiendeshwa.
No comments:
Post a Comment