Bodi ya Nyama Tanzania imetoa tahadhari kwa wananchi na kuwataka kuacha kula nyama inayouzwa ikiwa imewekwa kwenye ndoo au kupangwa kwenye meza za mabucha kwa sababu si salama kwa afya.
Vilevile
imewataka wauza nyama kwenye mabucha kuacha kukata nyama kwa kutumia
magogo kwa vile wanahatarisha usalama wa walaji.
Akizungumza
na waandishi wa habari Dar es Salaam jana, Ofisa Nyama wa Bodi hiyo,
Edgar Mbio, alisema nyama hiyo na ile inayokaa buchani zaidi ya saa
nne.
Mbio alisema kwa utaalamu nyama kama hiyo inakosa sifa ya kuwa na ubora unaofaa kwa matumizi ya binadamu.
“Biashara ya mifugo hufanyika machinjioni na buchani, hatutegemei kuona kinyume na hapo.
“Watu
wanaonunua nyama kwenye meza… ndoo hizi ndizo zinazoleta madhara kwa
sababu hazijakaguliwa, pia wale wanaonunua nyama ambayo imeshinda
inanig’inia buchani nayo inakuwa imeshapoteza ubora kwa kuwa kwa kawaida
nyama inapaswa kuhifadhiwa si zadi ya saa nane,” alisema Mbio.
Alisema
wapo pia ambao hununua nyama katika bucha ambayo wanatumia vibao
kukatia navyo si salama kwa sababu muuzaji anapokata anaacha ubora wa
kitoweo hicho kwenye kibao.
Alisema
mtu yeyote anayekula nyama iliyochinjwa na kuhifahiwa holela lazima
apate madhara kwa kuwa inakuwa si bora na salama hivyo haifai kwa
matumizi ya binadamu.
Ofisa
huyo alisema bodi ya nyama inaamini nyama bora na salama inaanzia kwa
mfugaji kwa kufauta kanuni za ufugaji bora zinazofuata taratibu ikiwamo
kuuza ng’ombe wa umri chini ya miaka kumi.
Awali,
Kaimu Msajili wa Bodi hiyo, Imani Sichalwe aliwataka wananchi kuongeza
kasi ya kula nyama ili kufikia kilo 50 kwa mwaka kwa kila mmoja.
Mbio alisema hicho ndicho kiwango kilichopendekezwa na Shirika la Chakula na Kilimo la Umoja wa Mataifa (FAO).
Alisema
takwimu zinaonyesha kila mwananchi nchini kwa kwa sasa anakula kilo 15
tu ya nyama kwa mwaka hivyo kuwa na tofauti ya kiko 35 kwa kila
mlaji.
“Tunakula nyama kwa kiwango cha chini ikilinganishwa na mahitaji yanayopaswa ndani ya miili yetu.
“Pamoja na hali ya uzalishaji wa nyama nchini kuwa juu lakini bado watu hawali nyama,” alisema Sichalwe.
Alisema
uchunguzi uliofanywa na bodi umebaini hali hiyo inatokana na bidhaa
hiyo kuuzwa kwa bei ghali ambayo kwa wastani huuzwa kuanzia Sh 6,000
hadi Sh 15,000 kwa kilo moja.
Alisema
ili kuboresha ulaji wa nyama bodi imeanza kuhamasisha utumiaji wa
mizani za digitali ambao utamuwezesha mlaji kununua kulingana na uwezo.
“Hii
mizani itawaisaidia wananchi ambao wanahitaji kula nyama lakini hawana
fedha za kununua kwa bei ya kiwango cha mizani iliyopo sasa.
“Mfano
mwenye bucha akiwa na mzani wa digitali anaweza kumuuzia mlaji nyama
hata ya Sh 500, tunaamini tutaongeza idadi ya walaji kwa njia hii,”
alisema Sichalwe.
Alisema kwa mujibu wa bajeti ya Wizara ya Mifugo na Uvuvi, Tanzania ni nchi ya pili ikifuatiwa na Ethiopiakwa mifugo mingi.
Kwa
sasa nchi ina ng’ombe wapatao milioni 30.5, mbuzi milioni 18.8,
kondoo milioni 5.3, kuku wa asili milioni 38.2, kuku wa kisasa milioni
36.6, nguruwe milioni 1.9 na punda 595,160.
Alisema
bajeti hiyo imeonyesha pia uzalishaji nyama nchini mwaka 2017/18
ulikuwa tani 679,992 za nyama ya ng’ombe, mbuzi, kondoo na nguruwe.
“Kati
ya tani 2,608.93 za nyama, tani 1,030.78 ni za ng’ombe, tani 1,248.14
mbuzi, kondoo tani 50.00 na punda tani 280.00 ziliuzwa nje ya nchi,”
alisema Sichalwe.
Alisema
tani 1,224.55 za nyama ikiwamo nguruwe tani 506.05, ng’ombe tani
711.03 na kondoo tani 7.47 ziliingizwa ndani ya nchini.
No comments:
Post a Comment