Jeshi
la Polisi Kanda Maalum Dar es salaam limefanikiwa kukamata silaha moja
aina ya Short Gun, risasi nne za short gun na mlipuko moja
uliotengenezwa kienyeji.
Kaimu
Kamanda wa Polisi Kanda Maalum Dar es Salaam, LIBERATUS SABAS-DCP
ametoa taarifa hiyo mbele ya waandishi wa habari leo Jijini Dar es
Salaam, amesema Silaha hiyo ilikamatwa tarehe 25 Oktoba 2018 majira ya
saa 21:30 huko maeneo ya Kijichi. Askari wakiwa doria waliitilia mashaka
pikipiki iliyokuwa haina namba za usajili ikiendeshwa na kijana mmoja
akiwa amewapakia wenzake wawili.
Vijana
hao baada ya kutambua kuwa wanafuatiliwa na Polisi walianza
kuwafyatulia risasi huku wakikimbia, ndipo askari walipojibu mapigo na
kufanikiwa kumjeruhi kijana mmoja na kupelekea kufariki akiwa anapelekwa
hospitali.
Kijana
huyo alipekuliwa na kukutwa akiwa na silaha aina ya Shotgun iliyokatwa
mtutu na kitako ikiwa na risasi nne pamoja na mlipuko mmoja.
Msako
mkali unaendelea kuwasaka watuhumiwa wote waliotoroka ikiwa ni pamoja
na wahalifu wengine wanaofanya matukio ya kihalifu kwa kutumia silaha za
moto ndani ya jiji la Dar es Salaam.
Katika
tukio lingine, Jeshi la Polisi Kanda Maalum ya Dar es Salaam huko
maeneo ya Kijichi limefanikiwa kukamata silaha ndogo bastola aina ya
Star ambayo haikuwa na namba za usajili na risasi nne ndani ya magazine.
Katika
tukio hilo lililotokea tarehe 1 Novemba 2018 majira ya saa 22:15 huko
maeneo ya Kijichi Mgeninani askari wakiwa doria walitilia mashaka
waendesha pikipiki yenye usajili wa namba MC 854 BBY aina ya TVS
iliyokuwa ikiendeshwa na mtu mmoja huku akiwa amepakia watu wengine
wawili.
Askari
walipowasimamisha watu hao walikataa kutii amri halali na ghafla watu
hao walifyatua risasi hewani ndipo Polisi walijibu mapigo na kuwajeruhi
majambazi hao ambao walifariki wakiwa wanapatiwa matibabu hospitalini.
Watu hao walipekuliwa na kukutwa na silaha hiyo.
Kukamatwa kwa mtandandao wa wizi wa magari
Jeshi la Polisi Kanda Maalum ya Dar es Salaam linawashikilia watuhumiwa 14 kwa tuhuma za wizi wa magari.
Watuhumiwa
hao wamekamatwa sehemu mbalimbali hapa jijini Dar es Salaam na mikoa
mingine wakiwa na magari 7, Bajaji moja na pikipiki moja ya wizi vyote
vimeibwa maeno mbalimbali ya Jiji la Dar es salaam.
Watuhumiwa
hao ni Luckman Ramadhani (36 , Ignasi Faustine (35), Ally Shaweji (30),
Stephen Mwanzalima (43), Emmanuel Mabula (42), Dismas Mfoyi (32),
Nyamuhanga Matiko (29), Freeman Paul (35), Ayubu Makame (41), Erasto
Nyamboneke (35), Seleman Saidi (42), Dickson Mbembaji (32), Ally Rashidi
(35) na Robert Nassoro (46)
Magari
yaliyokamatwa ni T 162 BLW Toyota land Cruiser MALI YA UWT-TANZANIA,
STL 6434 Toyota Land Cruise MALI YA WIZARA YA AFYA, T 855 DLE Toyota
Harrier, T 199 DEU Toyota Noah, T 249 DLL Toyota IST, T 255 AJG Rav4
gari hii ILIIBIWA udsm IKIWA na namba T 271 DFF, T 556 DJQ Toyota Allion
, MC 854 BYY pikipiki aina ya TVS Honda , MC 639 BYA Bajaji
Aidha
kuna magari zaidi ya manne ambayo yamekamatwa mikoani, na yako njiani
yanaletwa hapa jijini Dar es salaam kwa ajili ya uchunguzi na utambuzi.
Watuhumiwa
wanahojiwa na watafikishwa mahamani kwa hatua zaidi. Jeshi la polisi
linaendelea na msako mkali dhidi ya wezi wa magari na watuhumiwa
wengine.
No comments:
Post a Comment