Trump Amfuta Kazi Mwanasheria Mkuu wa Marekani Jeff Sessions

Mwanasheria Mkuu wa Marekani Jeff Sessions amejiuzulu wadhifa wake, baada ya kuombwa kufanya hivyo na Rais Donald Trump.

Trump ametangaza kuondoka kwa Sessions kupitia ukurasa wake wa Twitter leo Alhamis Oktoba 8, akimtakia kila la kheri.

Nafasi yake itashikiliwa kwa muda na aliyekuwa mkuu wake wa utumishi Matthew Whitaker. Whitaker sasa atasimamia uchunguzi wa madai ya Urusi kushirikiana na kampeni za rais Trump mwaka 2016.

Nancy Pelosi, anayetarajiwa kuliongoza Baraza la wawakilishi amesema kujiuzulu huko ni jaribio la wazi la Trump, kupunguza makali ya mchunguzi maalumu Robert Mueler anayeongoza uchunguzi huo wa Urusi.

Kiongozi mwingine wa Democratic katika seneti Chuck Schumer amesema mabunge yote ya Marekani ni lazima yalinde uchunguzi huo.
Kwa upande wake, Jeff Sessions katika barua yake ya kujiuzulu, aliweka bayana kuwa uamuzi wa kuondoka katika nafasi hiyo haukuwa wake.

Katika barua isiyokuwa na tarehe alimjulisha Rais kwamba anawasilisha barua yake ya kujiuzulu kama alivyomtaka afanye hivyo
Share:

No comments:

Post a Comment

IDADI YA WASOMAJI

TUSIKILIZE LIVE KUPITIA TUNEIN

UNGANA NASI FACEBOOK HAPA

10 ZILIZOSOMWA ZAIDI

Labels

Blog Archive