Spika wa Bunge, Job Ndugai amemzuia Waziri Mkuu Kassim Majaliwa kujibu swali juu ya kuitwa nchini kwake balozi wa Umoja wa Ulaya (EU) nchini, Roeland van de Geer kwa kile alichokisema swali hilo lilikuwa nje ya uwezo wa Serikali.
Swali
hilo liliwasilishwa bungeni na Mbunge Cecil Mwambe wakati wa kipindi
cha maswali na majibu kwa Waziri Mkuu ambapo alihoji juu ya wito wa
balozi huyo wa Umoja wa Ulaya.
“Hivi
karibuni tulishuhudia balozi wa EU alikuwa ameitwa kwao kujadili
mahusiano ya nchi yetu na jumuiya za kimataifa. Kuna nini
kinachoendelea?" Alihoji Mbunge Cecil
Akitoa
maelezo ya maswali hayo Spika Ndugai amesema “Napata wakati mgumu
kupitisha swali lako sasa kama ameitwa nchini kwao unataka Waziri Mkuu
ajibu nini, waziri Mkuu tunakushukuru nenda unaweza kwenda kupumzika.”
Ufafanuzi
wa wito wake ulitolewa na Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa
Afrika Mashariki, Balozi Dk.Augustine Mahiga ambapo aliweka wazi kuwa
balozi huyo hajafukuzwa kama inavyoelezwa bali ameitwa makao makuu ya
umoja huo.
''Balozi
wa Umoja wa Ulaya (EU) nchini Tanzania, Roeland van de Geer
anayetarajia kuondoka leo (jumamosi iliyopita) usiku kwenda makao makuu
ya EU hajafukuzwa bali ameitwa na umoja huo kikazi'', ilieleza taarifa
ya Waziri Dr.Mahiga.
Taarifa
za kufukuzwa kwa balozi Roeland van de Geer zilisambaa usiku wa Ijumaa
mitandaoni na kuzua mijadala mbalimbali, jambo ambalo ilipelekea Waziri
husika kutolea ufafanuzi.
No comments:
Post a Comment