Mbunge
wa Mafia, Mbaraka Dau (CCM), amemtuhumu Waziri wa Ujenzi, Uchukuzi na
Mawasiliano, Isaack Kamwele, akidai amekiuka agizo la Waziri Mkuu,
Kassim Majaliwa, la kupeleka Mafia meli iliyotolewa na mfanyabiashara
Said Salim Bakhressa akidai ni maagizo ya kisiasa.
Dau
amesema hayo bungeni jijini Dodoma leo Jumanne Novemba 6, wakati
akiwasilisha Mapendekezo ya Mpango wa Maendeleo wa Taifa na Mwongozo wa
Maandalizi ya Mpango na Bajeti ya Mwaka 2019/20.
Alidai
kuwa, suala la kupeleka meli hiyo Mafia walilijadili na Waziri Mkuu
Majaliwa na akakubali ipelekwe Mafia jambo ambalo hata Profesa Makame
Mbarawa aliyekuwa waziri wa wizara hiyo, aliliridhia.
“Sasa
hivi nimemfuata na kumkumbusha suala hilo lakini Waziri Kamwele anasema
ni kauli za kisiasa, sasa inakuwaje waziri anasema agizo la Waziri Mkuu
ni la kisiasa,” alihoji.
Alisema
pia alimtuma mbunge mwenzake ili azungumze na Waziri Kamwele, lakini
naye alijibiwa kuwa ili meli ipelekwe huko labda nauli iwe Sh 100,000.
Kabla
ya mchangiaji wa mwisho kusimama, Waziri Kamwele alisimama na kusema;
“Mbunge wa Mafia amenituhumu kuwa nilitoa maneno yanayoosha nimemdharau
Waziri Mkuu, sijawahi kusema hayo maneno na waziri mkuu ila nakumbuka
alinipigia simu akanimbia meli hiyo iliyotolewa na mfanyabiashara
Bakhresa ifanye safari Mafia, nikatoa maagizo suala hilo liangaliwe kama
linawezekana nikaambiwa meli hiyo inafanyiwa matengenezo,” amesema
Kamwelwe akidai kauli ya Dau si nzuri kwa sababu Waziri Mkuu ni bosi
wake.
No comments:
Post a Comment