Treni
 ya abiria inayofanya safari zake kati ya Stesheni na Pugu, jijini Dar 
es Salaam imepata ajali baada ya mabehewa yake mawili kuanguka eneo la 
Karakata wilayani Ilala na kujeruhi watu 9, leo asubuhi, Ijumaa, Novemba
 2, 2018.
Kamanda wa Reli nchini, David Mnyambuga amethibitisha kutokea kwa ajali hiyo na kusema mabehewa hayo mawili yameharibika vibaya na kwamba majeruhi tayari walikimbizwa hospitali kwa ajili ya kupatiwa matibabu.
 






No comments:
Post a Comment