Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu imemuonya mshereheshaji maarufu nchini Tanzania, Anthony Luvanda maarufu kama MC Luvanda kwa kusafiri bila ya ruhusa ya Mahakama.
Onyo
hilo limetolewa leo Jumatatu Novemba 19, 2018 na Hakimu Mkazi Mkuu,
Huruma Shaidi mbele ya mshtakiwa Luvanda, wakili wake Jebra Kambole na
wakili wa Serikali Mwandamizi, Kishenyi Mutalemwa.
Hatua
hiyo ilifikiwa baada ya wakili Kishenyi kuieleza Mahakama kuwa
upelelezi wa kesi hiyo bado haujakamilika na kwamba mara ya mwisho
kulikuwepo na amri ya Mahakama ya kumkamata mshtakiwa huyo kwa kusafiri
bila ruhusa ya Mahakama.
Wakili Kishenyi ameeleza Mahakama kwa sababu ametokea akumbushwe masharti ya dhamana.
Baada
ya wakili Kishenyi kueleza hayo, wakili wa Luvanda, Jebra Kambole
amedai yeye hana pingamizi kuhusu mshtakiwa kukumbushwa masharti ya
dhamana na akaomba radhi kwa yaliyotokea na kwamba mambo hayo
hayatajirudia tena.
Hakimu
Shaidi alimwambia mshtakiwa huyo kila kitu kina nidhamu yake, pia hata
katika kesi na kufika mahakamani kuna nidhamu yake.
"Kitendo cha wewe kusafiri bila kuitaarifu Mahakama si kitu kizuri, ukitaka kusafiri toa taarifa."
Hakimu Shaidi ameiahirisha kesi hiyo hadi Desemba 18, 2018 na akamuonya mshtakiwa huyo afuate utaratibu.
Awali,
Hakimu Shaidi Oktoba 23, mwaka huu akitoa hati ya kukamatwa kwa
Luvanda wakati kesi hiyo ilipopangwa kwa ajili ya kutajwa lakini
mshtakiwa huyo hakuwepo mahakamani.
MC Luvanda pamoja na kampuni yake, wanakabiliwa na mashtaka matatu likiwemo la kutumia kikoa ambacho akijasajiliwa Tanzania.
No comments:
Post a Comment