Kwa
mliganisho wa mahitaji na uzalishaji nchi ina ziada ya tani 3,013,515
na imejitosheleza kwa asilimia 123 na 120 mtawalia ambapo uzalishaji
katika msimu wa 2016/2017 na 2015/2016 ulikuwa tani 15,900,864 na
16,172,841 mtawalia ambapo mahitaji ya chakula yanayoendana na
uzalishaji huo ni tani 13,159,326, na 13,300,034 kwa mwaka wa ulaji
2017/2018 na 2016/2017 mtawalia.
Uzalishaji
wa mazao ya chakula katika msimu wa uzalishaji wa 2017/2018 ulifikia
tani 16,981,974 zikiwemo tani tani 9,537,857 za mazao ya nafaka na tani
7,354,117 mazao yasiyo nafaka, kiwango ambacho kimeiwezesha nchi
kutosheleza mahitaji yake ya chakula ya tani 13,569,285 katika mwaka
2018/2019 kwa kiwango cha utoshelevu (Self Sufficiency Ratio-SSR) cha
asilimia 124.
Waziri
wa Kilimo Mhe Japhet Hasunga (Mb) ameyasema hayo tarehe 2 Januari 2019
wakati akizungumza na waandishi wa habari katika ukumbi wa mikutano
maarufu kama Kilimo IV Jijini Dodoma.
Alisema
Uzalishaji wa mahindi katika msimu wa 2017/2018, 2016/2017 na 2015/2016
ulikuwa ni tani 6,273,150; 6,680,758 na 6,148,699 mtawalia,wakati
mahitaji yanayoendana na uzalishaji huo ni tani 5,462,390; 5,407,499 na
5,202,405 katika miaka ya ulaji ya 2018/2019, 2017/2018 na 2016/2017,
Ambapo ziada ya tani 810,760(2018/2019); 1,273,259(2017/2018) na
946,284(2016/2017) zilipatikana.
Uzalishaji
wa mchele katika msimu wa 2017/2018, 2016/2017 na 2015/2016 ulikuwa ni
tani 2,219,628; 1,593,609; na 2,229,071 mtawalia,mahitaji yanayoendana
na uzalishaji huo ni tani 990,044; 924,435; na 976,925 katika miaka ya
ulaji ya 2018/2019, 2017/2018 na 2016/2017,Ziada ya tani
1,229,583(2018/2019); 669,175(2017/2018) na 1,252,146(2016/2017)
zilipatikana.
Mhe
Hasunga alisema kuwa kutokana na ziada hizo za uzalishaji nchi
imeendelea kuwa ghala la chakula kwa nchi jirani. Kwa mfano, kulingana
na takwimu za Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA), katika kipindi cha mwezi
Juni 2017 hadi Juni 2018 jumla ya tani 64,477.95 za Mahindi zenye
thamani ya shillingi billioni 90.6 na Maharage tani 99,434.45 zenye
thamani ya shillingi bilioni 222.0 ziliuzwa katika nchi za DRC, Rwanda,
Burundi, Kenya, Uganda, Sudan ya Kusini na Uarabuni.
Hasunga
aliongeza kuwa Kati ya mwaka 2015/2016 na 2017/2018 uzalishaji wa mazao
ya Asili ya Biashara umeongezeka kwa viwango tofauti tofauti, ambapo
zao la korosho kwa sasa linalimwa katika mikoa 17 na Halmashauri 90 hapa
nchini baada ya kuanza kwa mpango wa kuongeza uzalishaji wa zao la
korosho mnamo mwaka 2013/2014 kupitia uhamasishaji wa kilimo hicho
katika mikoa mipya.
Amesema
kuwa Mikoa ya asili inayoongoza kwa kilimo cha zao la korosho ni
Mtwara, Lindi, Ruvuma, Pwani na Tanga. Katika miaka ya hivi karibuni
mikoa mingine mitano nayo imeanza kuzalisha korosho kwa kiasi kidogo
ambayo ni Singida, Dodoma, Morogoro, Mbeya na Njombe.
Alisema
kuwa taarifa ya uhakiki na malipo kwa wakulima mpaka kufikia tarehe 29
Desemba 2018 tayari Vyama vilivyohakikiwa na kulipwa ni 450.
Malipo
yaliyohakikiwa na kuwasilishwa benki ni tsh 231,937,341,674, Malipo
yaliyolipwa katika akaunti za Wakulima ni tsh 210,485,753,571, Korosho
iliyolipiwa ni Kilo 70,284,043, Kiasi cha Korosho iliyokusanywa katika
maghala makuu ni Tani 195,175.844, na Kiasi cha Korosho iliyosombwa na
kupelekwa katika maghala ya Hifadhi ni Tani 35,175.844
Katika
taarifa yake na waandishi wa habari Mhe Hasunga ameeleza kuwamatumizi
ya mbegu bora za pamba yameongezeka kutoka tani 14,500mwaka 2015/2016
hadi tani 18,500 mwaka 2017/2018 na matarajio ni kufikia tani 25,000
msimu wa 2018/2019. Mpaka sasa kiasi cha mbegu tani 27,769 zimesambazwa
na ni asilimia 37 zaidi ya kiasi kilichoombwa na Wilayaambacho kilikuwa
tani 20,284.
Aidha,
Uzalishaji wa chai kavu umeongezeka kutoka tani 32,628 mwaka 2015/2016
hadi kufikia tani 34,010 mwaka 2017/2018. Matumizi ya mfumo wa ushirika
umeongeza bei ya kilo moja ya majani mabichi kutoka wastani wa Shilingi
251 mwaka 2015/16 hadi shilingi 314 mwaka 2017/18. Thamani ya mauzo ya
chai nje ya nchi imeongezeka kutoka Dola za kimarekani51,794,854.00
mwaka 2015/2016 hadi kufikia Dola za kimarekani62,167,167.00 mwaka
2017/2018.
Kuhusu
zao la Mkonge uzalishaji umeongezeka kutoka tani 39,393 mwaka 2015/16
hadi tani 43,279 mwaka 2017/18. Bei ya tani moja ya Katani daraja la UG
mwaka 2015/2016 ilikuwa Shilingi 2,200,000 na mwaka 2017/2018 imefikia
Shilingi 3,330,000 sawa na asilimia 50. Thamani ya mauzo ya singa nje ya
nchi ni kutoka dola za Kimarekani 35,991,161 mwaka 2015/16 hadi dola za
Kimarekani 45,835,845 mwaka 2017/18.
Akieleza
kuhusu zao la Sukari Waziri Hasunga amesema kuwa Serikali imeimarisha
udhibiti wa uingizaji holela wa sukari kutoka nje hali iliyoimarisha
soko la sukari nchini.
Udhibiti
huo umechochea ongezeko la uzalishaji wa sukari kutoka tani 293,075
mwaka 2015/2016 hadi takriban tani 307,431.14 mwaka 2017/2018. Aidha,
uzalishaji wa sukari unatarajiwa kuongezeka na kufikia tani 352,600
mwaka 2018/2019.
Vilevile,
Serikali imeratibu uanzishwaji wa mashamba mapya ya miwa ya Mkulazi I
(Ngerengere), Mkulazi II (Mbigiri) na Shamba la Bakhresa –Bagamoyo Sugar
(Makurunge). Sekta ya Sukari kwa ujumla inatoa ajira isiyo ya moja kwa
moja kwa watu 57,000 pamoja na kutoa fursa ya ajira kwa watu wengine
takriban 75,000 ambao wanahusika na shughuli zinazotoa huduma kwenye
mnyororo wa thamani wa uzalishaji wa sukari nchini.
No comments:
Post a Comment