Katibu Mkuu wa Chama Cha Mapinduzi, Dkt Bashiru Ally, amesema chama hicho hakitasita kuyakata majina ya wananchama wake ambao watabainika kutumia njia ambazo si halali ili kuhakikisha wanapewa nafasi ya kugombea uongozi kwenye chama hicho.
Dkt
Bashiru ametoa kauli hiyo wakati akiwa kwenye ziara ya kikazi Mkoani
Bukoba, ambapo alikutana na viongozi mbalimbali wa CCM, pamoja na
viongozi wa vyama vya mazao.
"Ukifuatilia
siasa za CCM wakati wa uchaguzi, ilikuwa ni za kutumia pesa, kununulia
wanachama kadi, mfumo wa uteuzi umebadilika, kura za maoni watu wengi
hawatahusika, si kwa sababu hawatakiwi kupata haki bali kutakuwa na
mchujo utaosimamiwa vizuri," amesema Dk Bashiru.
Aidha
kuelekeea Uchaguzi wa serikali za mitaa utakaofanyika mwaka huu,
kiongozi huyo amewataka wananchi kutowachagua viongozi wanaowapa hela,
kwakuwa uchaguzi wa serikali za mitaa ni uchaguzi muhimu kuliko uchaguzi
mkuu kwa sababu serikali za mitaa ndizo zilizo karibu na wananchi na
zinazogusa maisha ya kila siku ya wananchi.
"Tumeanza
kuhamasisha wanachama wenye sifa waanze kujitokeza hasa sehemu za
vitongoji na vijiji, kwasababu uchaguzi wa mwaka huu utakua ni uchaguzi
wa wanachama wenye sifa, sio wanachama wanaoweza kufanya siasa za
kutumia pesa au kupendeleana," ameongeza Dkt Bashiru.
No comments:
Post a Comment