Mtoto wa Miaka 15 Amuua Mwenzake wa Miaka 16 Kwa Panga


Mwanafunzi wa kidato cha pili Shule ya sekondari Naisinyai wilayani Simanjiro Mkoa wa Manyara Godfrey Otieno (16) amefariki dunia kwa kukatwa panga kichwani na rafiki yake baada ya kumtania kwa kumwita albino.

Watoto hao ambao ni marafiki na majirani walikuwa pamoja wakisubiria kushangilia mwaka mpya wa 2019 ambao uligeuka kuwa kilio.

Kamanda wa polisi wa Mkoa wa Manyara, Agostino Senga amesema tukio hilo limetokea Desemba 31, 2018 saa tatu usiku katika kitongoji cha Songambele kata ya Mirerani wilayani Simanjiro.

Amemtaja anayedaiwa kufanya mauaji hayo ni George Damas (15) mwanafunzi aliyemaliza shule ya msingi hivi karibuni na kufaulu, alikuwa akisubiri kupangiwa shule ya sekondari.

Ametaja chanzo cha kifo hicho ni utani kwani Otieno alimtania mwenzake kwa kumwita albino ndipo akakasirika na kuchukua panga na kumkata kichwani.

Amesema wanamshikilia Damas huku wakiendelea na uchunguzi wa tukio hilo kabla ya kumfikisha mahakamani.
Share:

No comments:

Post a Comment

IDADI YA WASOMAJI

TUSIKILIZE LIVE KUPITIA TUNEIN

UNGANA NASI FACEBOOK HAPA

10 ZILIZOSOMWA ZAIDI

Labels