Naibu
waziri wa Habarui, sanaa utamaduni na michezo Mhe. Juliana Shonza
amewataka wasanii wa Injili kjijengea tabia ya kujiwekea akiba ili punde
wapatapo matatizo waweze kuyatatua kwa urahisi.
Ameyasema
hayo hivi karibuni alipokuwa akizindua mfuko wa Tagoane LoanFund Jijini
Arusha ambapo amepongeza uongozi wa Tagoane kufikia hatua hiyo.
Ameyataka mashirikisho yote ya muziki wa Injili nchini Tanzania kuiga
mfano nzuri wa Tagoane ili waweze kuwa na mashirikisho ambayo ni hai na
yanayoleta mshindo kwenye jamii.
Amesema
yeye kama mlezi wa wasanii wote nchi amewaomba waamke wachangamkie
fursa na wasiwe wavivu kujifunza kutoka kwa wenzao waliofanikiwa
.Amewataka wasanii kukaa kwa pamoja Kuonyeshe Uzalendo kwa nchi yao
wajadili changamoto mbalimbali wanazozipitia na kutafuta namna ya
kutazua changamoto zinazowakabili.
Kwa
upande wake Rais wa Tagoane Taifa Dkt. Godwin Maimu amesema kuwa
wanedhamiria kuanzisha mfuko wao wa Tagoane Loan Fund ambapo mpaka sasa
umekuwa na wanachama ambao wameshachangia akiba zao zipatazo shilingi
milioni kumi.Amesema mfuko huo unatarajiwa kuanza kutoa mikopo kwa
wanachama wavhqngiaji kuanzia 2 januari 2019
Maendeleo
kama vijana hayawezi kuendelea ukiwa na jitihada za mtu mmoja mmoja
bali balintunapounganisha nguvu zetu kwa pamoja mwisho wa siku tunapata
kitu cha kuweza kutusaidia. Alisema Dkt Maimu
Amesema
lengo la mfuko huo ni kuwakwamua wasanii watakaokuwa na miradi ya
uwekezaji, makampuni makubwa, na watakaoweza kutoa fursa na ajira kwa
vijana hapa nchini na kulipa kodi kama wananchi wengine
Aidha
tamasha hilo lililoshorikisha wasanii mbalimbali wakiwemo
wajasiriamali, wachoraji, wachongaji, sanaa za ubunifu ni fursa ambayo
Tagoane wameileta na kuwataka wasanii waitumie kwaajili ya kujikwamua
kiuchumi na kuoata maendeleo katia jamii nzima
Tamasha
hilo la Tukuza festival lilizinduliwa rasmi mwaka 2017 likiwa
linafanyika kwa mara ya pili limebeba kauli mbiu isemayo toto yatima
haihitaji chakula a mavazi peke yake ila awezeshwe nyenzo za kutimiza
malengo yake.
No comments:
Post a Comment