Waziri wa Mambo ya Ndani, Kangi Lugola amewataka polisi kuja na njia mbadala za kuwakamata madereva bodaboda badala ya kuwavizia kwenye minada na magulio na kusababisha ajali.
Lugola amesema hayo jana Jumatano Januari 2, 2019 Bukoba mkoani Kagera katika mkutano wa hadhara.
Amesema
hakuna ulazima wa kufukuzana na waendesha pikipiki kwa kuwa vyombo
wanavyoendesha vinaweza kuchukuliwa namba kuliko kuwavizia na kufukuzana
nao.
Ameonya
hatua ya kuwavizia kwenye minada, magulio na maeneo mengine inawaathiri
hata abiria wanaokuwa wamebebwa katika pikipiki hizo kwa kupata ajali.
Katika
mkutano huo wa hadhara uliofanyika uwanja wa Mashujaa baadhi ya
waendesha pikipiki wamedai hakuna mazingira rafiki ya kufanya kazi kati
yao na Polisi.
Hata
hivyo, Waziri Lugola amewataka waendesha pikipiki kuzingatia sheria za
usalama barabarani ili kulinda haki za watumiaji wengine wa barabara.
No comments:
Post a Comment