HALMASHAURI YA USHETU YAPIGA MARUFUKU UVUNAJI HOLELA WA MITI KWENYE MAENEO YA TAASISI ZA UMMA


Na Salatory Ntandu 
USHETU, KAHAMA

Halmashauri ya Ushetu Wilayani Kahama Mkoani Shinyanga imepiga marufuku uvunaji holela wa Miti kwenye Maeneo yote ya taasisi za umma zikiwemo shule, Zahanati na Vituo vya afya bila kibali kutoka kwa mamlaka husika. 

Agizo hilo limetolewa jana na Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri hiyo, MICHAEL MATOMORA kwenye mkutano wa hadhara wakati akizungumza na wakazi wa kijiji cha Ifunde baada ya kubaini kuwepo kwa uvunaji holela wa miti katika shule ya msingi Ifunde. 

Amesema serikali kwa sasa inaendesha kampeni ya Upandaji miti nchi nzima hivyo ni kosa kwa Mtumishi wa Umma au mwananchi kukata miti iliyopandwa kwenye maeneo ya Umma bila kufuata taratibu za kisheria. 

Mbali na hilo, MATOMORA amewataka wananchi katika Halmashauri hiyo kujenga vyoo bora katika nyumba zao ili kuepuka magonjwa ya Mlipuko.

Share:

No comments:

Post a Comment

IDADI YA WASOMAJI

TUSIKILIZE LIVE KUPITIA TUNEIN

UNGANA NASI FACEBOOK HAPA

10 ZILIZOSOMWA ZAIDI

Labels

Blog Archive