KAMPUNI YA ACACIA YAKABIDHI MRADI WA MAJI NA UZIO WA SHULE KWA KIJIJI CHA KAKOLA WILAYANI KAHAMA

Na Faraji Mfinanga
KAHAMA
Kampuni ya ACACIA ambayo inamiliki mgodi wa dhahabu wa Bulyanhulu wilayani Kahama, imekabidhi mradi wa maji na uzio wa shule vyote vikiwa na thamani ya zaidi ya shilingi milioni 334.9 kwa kijiji cha Kakola halmashauri ya Msalala wilayani Kahama.

Miradi hiyo imekabidhiwa na kaimu Meneja wa mgodi wa ACACIA Bulyanhulu, JOHN ALMOND kwa kaimu mkurugenzi wa halmashauri ya Msalala, LEONARD MABULA Machi 02 mwaka huu katika hafla iliyofanyika viwanja vya shule ya msingi Kakola.


Akikabidhi miradi hiyo, ALMOND amesema mradi wa maji uliogharimu zaidi ya shs 189 utawanufaisha zaidi ya wakazi 3000 wa kijiji hicho, huku uzio wa shule uliogharimu zaidi ya shs 145 utawanufaisha zaidi ya wanafunzi 2000 wa shule za msingi Kakola A na B.


Akipokea miradi hiyo kwa niaba ya wananchi, MABULA amemshukuru mwekezaji ACACIA kwa kuendelea kuchangia maendeleo ya jamii huku akiwataka wananchi kuwa na tabia ya kushukuru wanapochangiwa badala ya kubaki wakilalamika, kwani matatizo hayawezi kwisha mara.


Mabula pia ametumia nafasi hiyo kuihusia jamii kutumia uzazi wa mpango baada ya kushtushwa na idadi kubwa ya wanafunzi katika shule hizo mbili ambapo ni zaidi ya 5000, na amewaomba wananchi kuitunza miradi hiyo yenye gharama kubwa.


Miradi hiyo in mwendelezo wa Kampuni ya ACACIA katika kuunga mkono serikali na jamii kwenye shughuli za maendeleo, ambapo mabilioni ya shilingi yamewekezwa katika muda uliopita, kwenye miradi ya Elimu, Maji, Afya na mingine mingi kwenye jamii inayouzunguka mgodi.

Share:

No comments:

Post a Comment

IDADI YA WASOMAJI

TUSIKILIZE LIVE KUPITIA TUNEIN

UNGANA NASI FACEBOOK HAPA

10 ZILIZOSOMWA ZAIDI

Labels

Blog Archive