Na Liluian Katabaro
KAHAMA.
Wakazi  wawili wa mtaa wa Mwime Wilayani KAHAMA Mkoani SHINYANGA, GODFEY JACOB (23) na KAVULA JACOB (21) amefikishwa katika Mahakama ya Wilaya ya KAHAMA kwa tuhuma ya kupatikana na dawa za kulevya aina ya bangi kinyume cha sheria. 
Mbele ya Hakimu Mkazi wa Mahakama hiyo IMANI BATENZI, mwendesha mashitaka wa Polisi SAADA ADAM amesema watuhumiwa  walikamatwa March 24  mwaka huu majira ya saa nane mchana  huko mtaa wa Mwime   wakiwa  na bangi  hiyo gram 35. 
SAADA amesema washitakiwa wametenda kosa hilo kinyume na kifungu namba 17 na kifungu namba 2 cha sheria ya kuzuia na kupambana na dawa za kulevya sura ya 5 marejeo ya mwaka 2015. 
Katika shauri hilo la jinai namba 135/2018 washitakiwa wamekana kutenda kosa hilo na wamerudishwa rumande kwa kukosa dhamana hadi Aprili 11 mwaka huu shauri hilo litakapotajwa tena mahakamani hapo. 
Home »
Habari za Kahama
 » WAWILI WAFIKISHWA MAHAKANI KWA TUHUMA YA KUKUTWA NA DAWA ZA KULEVYA







No comments:
Post a Comment