WANANCHI WA NYIHOGO KAHAMA WAANZA UJENZI WA SHULE YAO YA MSINGI


Na Ndalike Sonda
KAHAMA.

WANANCHI wa Mtaa wa Mayila Kata ya NYIHOGO katika Halmashauri ya Mji wa KAHAMA wameanza ujenzi wa shule yao ya msingi ili kuwaondolea watoto wao adha inayowakabili sasa ya kutembea umbali mrefu kwenda shule za msingi Kilima na Mhungula.

Wakazi wa Mtaa huo, AGNETHA JUVINUS na JOEL MWENDAPOLE wamesema kukamilika kwa shule hiyo kutapunguza ajali na vifo vya wanafunzi wakati wa kuvuka barabara kuu ya Isaka - Ushirombo ambapo vifo 17 vimeshatokea tangu kukamilika kwa barabara hiyo mwaka 2014.

Nao baadhi ya wanafunzi wanaoishi mtaa huo, pamoja na kufurahia ujenzi wa shule hiyo, wameiomba serikali kuharakisha ujenzi huo na pamoja na kuifungua kwaajili ya kusajili wanafunzi.

Kwa mujibu wa Diwani wa Kata ya Nyihogo, SHADRACK MGWAMI shule hiyo itakuwa imekamilika na kuanza kutumika ifikapo mwaka 2020 na amewataka Wananchi kuendelea kujitolea kwa hali na mali kukamilisha ujenzi huo.

Mwenyekiti wa Ujenzi huo, SOLOMON JUMA ukubwa wa ekari 8 limetengwa kwa ajili ya ujenzi wa shule hiyo ambapo wananchi wamekwisha kusomba mawe huku wadau mbalimbali wakiahidi kuchangia vifaa vya ujenzi.
Share:

1 comment:

  1. Hongereni kwa majukumu ,nmehitimu kozi ya ualimu daraja 3A endapo kuna uhitaji nipo tyari kuwafundsha watoto,asanteni 0621469138 au 0715281376 nipo mtaani natamani sana kutumia kipaji nilichopata nipo kilimanjaro Region

    ReplyDelete

IDADI YA WASOMAJI

TUSIKILIZE LIVE KUPITIA TUNEIN

UNGANA NASI FACEBOOK HAPA

10 ZILIZOSOMWA ZAIDI

Labels

Blog Archive