DIWANI WA KATA YA SABASABINI HALMASHAURI YA USHETU EMMANUEL MAKASHI ALIYEANGUA KILIO KWENYE BARAZA LA MADIWANI.
Na Salvatory Ntandu
KAHAMA
Katika
hali isiyokuwa ya kawaida Diwani wa Kata ya Sabasabini EMANUEL MAKASHI amengua
kilio kwenye kikao cha Baraza la Madiwani alilalamikia hoja yake kutopewa
nafasi ya kusikilizwa katika kikao hicho
aliyoiwasilisha juu ya kutoridhishwa na utendaji kazi wa afisa Mtendaji wa Kata hiyo CHRISTOPER
LYOGELO.
Katika
Madai aliyoyawasilisha MAKASHI amesema tangu afisa huyo apangiwe katika kituo
hicho cha kazi mwaka 2005 ,amekuwa hasomi mapatao na matumizi, hali ambayo imesababisha wananchi kugoma kuchangia shughuli za
maendeleo.
Baada
ya kumsikiliza MAKASHI hatimaye hoja hiyo imejibiwa na Kaimu Mkurugenzi
mtendaji wa Halmashauri ya Ushetu ONESMO BENJAMIN na haya hapa majibu yake aliyoyatoa kwenye
kikao.
Amesema
watahakikisha suala hilo linafanyiwa kazi kwa haraka ili muafaka upatikane.
Lakini
baaada ya kumalizika kwa kikao hicho cha Baraza la Madiwani Raha ya leo
ilimtafuta MH.MAKASHI kuzungumzia hoja aliyoiwasilisha katika Baraza hilo.
Baraza
la Ushetu limeketi kwa siku mbili kwa wakilishi wananchi(madiwani) kujadili
taarifa mbalimbali kuhusiana na maendeleo ya
wananchi.
No comments:
Post a Comment