Wazee  wilayani Kahama mkoani Shinyanga, wametajwa
kuwa na nafasi kubwa ya kuimarisha mila na desturi katika jamii endapo
waataendelea kusimamia  na kuelekeza
maadili mema kwa jamii.
Hayo yameelezwa hivi
karibuni na  Katibu wa Umoja wa  wazee wilaya ya Kahama (UWAKA) PAUL NTELYA
wakati akizungumza kwenye  Uzinduzi wa
tawi la umoja huo kata ya Bulungwa halmashauri ya Ushetu.
NTELYA amesema ili kuwa na
taifa lenye watu waadilifu ni lazima wazee wachukue nafasi ya kukemea maovu
yote yanayoharibu maadili mema katika jamii na kwamba jamii izidi kudumisha
mila na desturi zao.
Katika huzinduzi huo wa
tawi  la UWAKA kata ya Bulungwa, umeundwa
uongozi wa  Kata hiyo ambao utaratibu
shughuli zote zinazuhusu umoja huo ikiwamo kutetea haki za  wazee hasa katika upande wa matibabu na
migogoro ya ardhi.
Mwneyekiti wa UWAKA , Kata
ya Bulungwa,  KAGEMO KAYANDA,
amewaomba  wazee katika kata hiyo kuwa na
umoja ili kuisdaidia jamii katika masuala mbalimbali ikiwamo suala la Migogoro
ya Ardhi ambalo limekuwa ni tatizo kubwa katika maeneo mengi nchini.






No comments:
Post a Comment