Zaidi ya madawati 160 yamekabidhiwa
na bodi ya elimu-Msalala, katika shule tatu za Secondari za halmashauri ya hiyo
ili kupunguza tatizo uhaba wa madawati kwa shule za sekondari.
Akizungumza leo katika
makabidhiano ya madawati hayo kaimu katibu wa bodi ya elimu Msalala MASATU
MNYORO amezitaja shule zilizokabidhiwa
madawati hayo kuwa ni shule ya sekondari Segese, Isaka na Mwalimu nyerere.
MNYORO amesema halmashauri hiyo, imekusudia kuboresha
sheria ya mfuko wa elimu ili iwe na vyanzo vingi vya
mapato na kwamba amewataka walimu wakuu
kusimamia utunzaji wa madawati hayo.
Kwa upande wao walimu wakuu
wa shule hizo wameishukuru Halmashuri hiyo na kwamba madawati hayo yatasaidia
kupunguza changamato ya madawati.
Naye mkurugenzi mtendaji wa
Halmashauri ya msalala SIMON BEREGE amewataka wadau mbali mbali kushirikiana kwa
pamoja ili kujenga vyumba vya madarasa na madawati ili kuondokana na tatizo
hilo.
Bodi ya mfuko wa elimu kwa
Halmshauri ya msalala ilianza kufanya kazi mwaka 2016 kwa kuhakikisha inaboresha
miundombinu ya elimu na kutafuta fedha kwa ajili ya kutengeneza madawati,
kujenga maabara na vyumba vya madarasa.
No comments:
Post a Comment