BI ROSE HAJI MWALIMU AKIWASILISHA MADA KWENYE MAFUNZO YA TATHIMINI NA UFUATILIAJI KWA WANDISHI WA HABARI MJINI DODOMA
|
|
|
Wandishi
wa habari wanawake nchini wametakiwa
kutumia uwezo wao kitaaluma wanapotekeleza majukumu yao wawapo kazini na si
kujiingiza katika masuala ya mapenzi na waajiri wao ili wapandishwe vyeo.
Hayo
yamesemwa na mkufunzi wa Radio za
kijamii nchini Kutoka Unesco Bi Rose Mwalimu kupitia semina ya radio za
kijamiii iliyofanyika ukumbi wa wakala wa majengo mjini Dodoma ambayo ilikutanisha vituo 24 vya
radio za kijamii .
Akiwasilisha
mada ya maadili kupitia semina hiyo Bi Rose amesema wazazi na walezi wamewasomesha watoto wao ili
waweze kupata taaluma na kurudi katika jamiii
kuitumikia ikiwa ni paamoja na
kujipatia kipato badala yake wandishi wengi wanawake wamekuwa wakishindwa
kutumia elimu waliyoipata katika utendaji kazi
Kwa
upande wao baadhi ya washiriki wa semina hiyo wamesema kuwa wanawake wengi
hushindwa kufanya kazi zao vizuri kutokana na tamaa za maisha kwa sababu huhitaji kupata pesa amabazo ziko nje ya uwezo wao.
Mafunzo
hayo yameanza Februari 6, 2018 na yanatarajiwa
kumalizika tarehe 12 Februari 12, siku moja kabla ya maadhimisho ya siku ya
radio duniani.
MATUKIO KATIKA PICHA:
WANDISHI WA HABARI WA REDIO ZA KIJAMII WAKIWA KWENYE MAFUNZO YANAYOENDELEA MJINI DODOMA
|
WANDISHI WA HABARI ZA REDIO ZA JAMII KUTOKA MAENEO TOFAUTI YA TANZANIA WAKIWA KWENYE MAFUNZO YANAYOENDELEA MJINI DODOMA
|
MWALIMU MARKO
AKIWA ANATAYARISHA MADA KWA AJILI YA KUIWASILISHA KWA WANDISHI WA HABARI
WA REDIO ZA JAMII TANZANIA KWENYE MAFUNZO YANAYOENDELEA MJINI DODOMA
|
No comments:
Post a Comment