Mamlaka ya Maji Safi na Usafi
wa Mazingira mjini Kahama, (KUWASA) imepata hasara ya takriban shilingi milioni 106 kutokana na
ukosefu wa maji ulioukumba mji wa Kahama kwa takriban siku 12.
Hayo yamebainishwa na Kaimu Mkurugenzi wa KUWASA,
Mhandisi CHANGANYA PAUL katika mkutano
wake na Wandishi wa Habari kuzungumzia athari zilizotokana na kusitishwa kwa
huduma hiyo na jinsi Mamlaka ilivyojipanga kukabiliana na hali hiyo siku za
usoni.
Kwa
upande wake, Mwenyekiti
wa Bodi ya Wakurugenzi ya KUWASA, Meja
Mtaafu BAHATI MATALA amesema wanafanya mazungumzo na KASHWASA ili
kutafuta nishati mbadala ya umeme kwenye chanzo kikuu cha maji
ya ziwa Viktoria kilichopo Ihelele wilayani Misungwi mkoani Mwanza.
Januari 17 mwaka huu, Shirika
la Umeme TANESCO lilisitisha huduma ya umeme kwenye chanzo hicho cha
Ihele, kutokana na deni la zaidi ya shilingi bilioni mbili
wanaloidai KASHWASA hatua iliyosababisha
mji wa Kahama kukosa maji kwa takriban siku kumi na mbili na hivyo uzalishaji
wa maji kusimama kabisa.
No comments:
Post a Comment