Waganga
wafawidhi wametakiwa kujadili sababu ya vifo vinavyotokea kwenye
hospitali zao ili kuzifanyia kazi changamoto hizo na kurudisha taarifa
Wizara ya Afya.
Hayo
yamesemwa na Mkurugenzi wa Mafunzo na Rasilimali watu Wizara ya Afya,
Dk. Otilia Gowelle, wakati wa ufunguzi wa mkutano wa waganga wafawidhi
nchini, Dodoma jana.
“Waganga
wafawidhi mnatakiwa kukaa vikao vya utabibu kujadili tiba pamoja na
kujadili kifo cha kila mgonjwa kujua changamoto iliyotokea na kuipatia
ufumbuzi na kuandikia taarifa kuondokana na vifo hasa vinavyotokana na
uzazi,” alisema Dk. Gowelle.
Aliwataka
wataalamu wa tiba kuzingatia vikao vya tiba na kufanyia kazi changamoto
au maboresho ili kuzitolea taarifa na kuzitatua pamoja na kushirikisha
wadau wengine.
Dk.
Gowelle aliwataka pia waganga wafawidhi kuweka mifumo ya ufuatiliaji
wagonjwa na kupokea malalamiko katika hospitali zao kufanya
maboresho ya huduma za afya wanazozitoa na kuchukua hatua zinazostahili.
“Kupitia
kikao hiki, nawataka mkae kama timu na kuandaa mipango kazi ya kuanza
kushughulikia kwa ukamilifu yale yote yaliyobainika katika taarifa hiyo.
“Lengo ni kuondokana na kero wanazokabiliana nazo wananchi wanapokuja kupata huduma katika hospitali zenu,” alisema Dk. Gowelle.
No comments:
Post a Comment