Chama
 Cha Mapinduzi (CCM) kimewapitisha makada wake wanne kuwania nafasi ya 
ubunge katika maeneo yao kufuatia kikao cha kamati kuu ya Halmashauri 
Kuu ya Taifa kukutana leo jijini Dar es salaam.
CCM
 imewapitisha waliokuwa wabunge wa maeneo hayo kupitia Chama Cha 
Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA), waliotangaza kujiunga na chama hicho 
kwa sababu mbalimbali ikiwemo kuunga mkono juhudi za Rais Magufuli.
Wabunge
 hao waliopitishwa ni Pauline Gekui wa jimbo la Babati, James Milya 
jimbo la Simanjiro, Joseph Mkundi Jimbo la Ukerewe, na Marwa Ryoba 
ambaye atawania nafasi ya ubunge jimbo la Serengeti.
Aidha
 Chama hicho kimetaja tarehe 15 novemba kuwa ndio tarehe ya mwisho kwa 
Chama hicho kuwapokea maombi ya wenye nia ya kujiunga na Chama hicho na 
kupewa dhamana ya uwakilishi kupitia tiketi ya CCM kwa wabunge na 
madiwani kutoka vyama vingine.
Aidha
 taarifa hiyo imesema baada ya tarehe hiyo hakuna kiongozi yeyote 
atakayepewa nafasi ya kugombea uwakilishi wa Chama hicho katika uchaguzi
 wa marudio badala yake watakuwa wanachama wa kawaida.
 






No comments:
Post a Comment