Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli ameagiza kusimamishwa kazi mara moja kwa Kamanda
wa Polisi wa Mkoa wa Kagera Augustine Ollomi, Kamanda wa Polisi wa
Wilaya ya Kyerwa Justine Joseph, Mkuu wa Upelelezi wa Wilaya ya Kyerwa
Everist Kivuyo na Mkuu wa Kituo cha Polisi cha Kyerwa Robert Marwa.
Viongozi
hao wa Polisi wanasimamishwa kazi ili kupisha uchunguzi wa tuhuma za
kuhusika katika magendo ya zao la kahawa katika Wilaya ya Kyerwa pamoja
na tuhuma nyingine.
Aidha,Rais
Magufuli amemuagiza Katibu Mkuu wa Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi
Mej. Jen Jacob Kingu na Inspekta Generali wa Polisi Simon Sirro
kuhakikisha uchunguzi wa kina unafanyika na hatua stahiki zinachukuliwa
endapo watabainika kuhusika katika magendo ya kahawa na makosa mengine
kwa mujibu wa sheria.
Tuhuma
dhidi ya viongozi wa polisi katika Wilaya ya Kyerwa zimebainika wakati
wa ziara ya Waziri Mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Kassim
Majaliwa Majaliwa.
No comments:
Post a Comment