Jeshi
 la Polisi Mkoani Mbeya, linalishikilia lori la mafuta mali ya Kampuni 
ya Oil Com, baada ya kukutwa limebeba vipodozi na pombe  vilivyopigwa 
marufuku kuingia nchini.
Kamanda
 wa Polisi Mkoa wa Mbeya, Ulrich Matei, amesema gari hilo lenye namba za
 usajili T 233 CXL limekamatwa eneo la Mbarali jijini hapa, jana saa 
nane mchana, likitokea nchini Zambia.
Kamanda Matei amesema katoni 15 za vipodozi na katoni mbili za pombe kali zimekutwa ndani ya gari hilo.
Amesema dereva wa gari hilo anatafutwa na polisi kwani baada ya gari hilo kukamatwa alifanikiwa kukimbia.






No comments:
Post a Comment