Ikiwa
 ni siku moja toka Mkuu wa Mkoa wa Dar es salaam, Paul Makonda atangaze 
kampeni ya kuanza kuwakamata mashoga pamoja na malaya ambao wanajiuza 
kupitia mitandao ya kijamii, ameanza kupata mrejesho.
Hatua
 hiyo imekuja baada ya msanii wa muziki, Amber Rutty kuachia video chafu
 mtandaoni hali ambayo ilimfanya mkuu huyo kutoa tamko la kutaka 
akamatwe.
RC
 Makonda alisema kwa tukio ambalo amelifanya msichana huyo anapaswa 
kufungwa jela, kwani ni ukiukwaji wa sheria za nchi huku akiwataka 
Wanadar es salaam kumtumia majina ya mashoga pamoja na watu ambao 
wanafanya biashara ya ngono mtandaoni.
“Nimepokea
 msg zaidi 5,763 na majina ya Mashoga zaidi ya 100 hii inaonyesha Wana 
DSM hawataki laana ya mashonga. Naendelea kupokea majina ya Mashoga,” amesema RC Makonda kupitia taarifa aliyoitoa siku ya leo.
Mkuu
 huyo amesema msako mkali wa kamata kamata ya mashoga na watu wanaojiuza
 utaanza wiki ijayo kwani kwa sasa anakiandaa kikosi kazi pamoja na 
kupokea baadhi ya majina.






No comments:
Post a Comment