Mkuu wa mkoa wa Dar Es Salaam Paul Makonda amefunguka tena kuhusiana na video chafu za mrembo Amber Rutty na mpenzi wake lakini pia kuhusiana na ongezeko la mashoga katika jiji la Dar es Salaam.
Akiongea
 na waandishi wa habari jana October 29, 2018, RC Makonda alisema kuwa 
Amber Rutty na mpenzi  wake bado  wapo lupango  wakati wanasubiriwa 
kupandishwa kizimbani na kuweka wazi kuwa adhabu yao ni kifungo cha  
maisha jela au miaka 30 kama itatbitika wanafanya kinyume na maumbile.
"Tayari
 yule binti anayeitwa Amber Rutty pamoja na bwana yake wapo chini ya 
polisi tangu kipindi kile nilivyotoa maelekezo na niseme kuwa kosa lile 
liko wazi na sheria inasema ni aidha kifungo cha maisha au miaka 30, 
hiyo yote ni kuonyesha ni jinsi gani serikali isivyopendezwa na mienendo
 inayomomonyoa maadili ya taifa letu”. Alisema Makonda
Lakini pia RC Makonda alitangaza vita na mashoga wote ambao wanajihusisha na shughuli za kufanya mapenzi kinyume na maumbile;
"Naomba
 nitoe fursa hii kwa wakazi wa Dar es Salaam, namba yangu ya simu 
inafahamika .Nimepata taarifa kwamba kuna mashoga wengi sana kwenye mkoa
 wetu na mashoga hawa ndio kazi yao wanajinadi kwenye mitandao ya 
kijamii, kwa hiyo nawaambia wananchi kama kuna shoga yoyote unamfahamu 
leo mpaka jumapili napokea taarifa zao”.






No comments:
Post a Comment