Abiria wawili Raia wa Sudan Kusini na Syria jana wamekamatwa Kiwanja cha Ndege cha Kimataifa cha Julius Nyerere (JNIA) wakisafirisha fedha taslim dola 70,000 za Kimarekani sawa na shilingi milioni 156 za Kitanzania na paundi 3410 za Sudan bila kufuata taratibu.
Akizungumza
na waandishi wa habari kwenye ukumbi wa mikutano wa Jengo la Pili la
abiria la JNIA, Msemaji wa Jeshi la Polisi, Kamishna Msaidizi, Barnabas
Mwakalukwa alimtaja Raia wa Sudan Kusini Bi. Nada Zaelnoon Ahamed (38)
mwenye hati ya kusafiria namba P01563534 amekamatwa saa 10:00 jioni
akiwa eneo la ukaguzi wakati akiingia ndani tayari kusafiri kwa ndege ya
Shirika la Ndege la Kenya (KQ 485) akielekea Nairobi.
Hatahivyo,
Afande Mwakalukwa amesema abiria huyo amekamatwa na dola 60,000 za
Kimarekani na paundi za Sudan 3410, ambazo zote kwa pamoja alishindwa
kutoa taarifa ya fedha alizokutwa nazo kwa mujibu wa sheria ya
utakatishaji fedha ya mwaka 2006 iliyofanyiwa marekebisho mwaka 2012.
Pia
alimtaja Bw. Mohamed Belal (31), Raia wa Syria mwenye hati ya kusafiria
namba 003-16L096876 aliyekuwa akisafiri kwa ndege ya Shirika la ndege
la Ethiopia (ET 864) kuelekea Syria kupitia Addis Ababa amekamatwa na
dola za kimarekani 10,000 sawa na Tsh. milioni 20 za Kitanzania, ambazo
naye alishindwa kuzitolea taarifa.
“Watuhumiwa
wote wawili wamezuiwa na hawawezi kuendelea na safari zao kwa ajili ya
uchunguzi zaidi na hatua za kisheria zilizopo,” amesema Afande
Mwakalukwa.
Naye
Mkurugenzi Mkuu wa Mamlaka ya Viwanja vya Ndege Tanzania (TAA), Bw.
Richard Mayongela amewapongeza maafisa usalama wa JNIA kwa kufanya kazi
kwa weledi na uadilifu pamoja na kushirikiana na vyombo vingine vya
ulinzi na usalama katika kuhakikisha wasafiri, wadau na maeneo yote ya
viwanja vya ndege yanabaki salama na vitendo vya kiuhalifu havina nafasi
katika viwanja hivyo.
Bw.
Mayongela amesema pamoja na watumishi hao kufanya kazi katika wakati
mgumu kutokana na baadhi ya abiria kuwa watata kila wanapotaka
kutekeleza wajibu wao kwa mujibu wa sheria na kanuni.
No comments:
Post a Comment