Katibu wa Itikadi na Uenezi wa CCM, Humphrey Polepole amesema wabunge wa upinzani wanaotaka kujiunga na chama hicho mwisho wa kufanya hivyo ni Disemba, 2018.
Polepole
 ametoa kauli hiyo jana Jumapili Oktoba 7, 2018 kupitia ukurasa wake wa 
mtandao wa kijamii wa twitter ambapo amesema mwaka 2018 ndio mwisho wa 
chaguzi ndogo za ubunge, wale watakaoshindwa kuhamia CCM wabaki walipo.
“Tumezingatia
 na tunaweka jitihada zetu zote katika kushughulika na utatuzi wa shida 
za watu wetu wa Tanzania. Mwaka 2018 ndiyo mwisho kwetu kufanya chaguzi 
ndogo za ubunge kwa wale wanaohama vyama vyao na kujiunga na CCM. 
Watakaoikosa raundi hii mbaki hukohuko tutakutana 2020”, ameandika Polepole.
 






No comments:
Post a Comment