News


MACHI 5, 2012
SHINYANGA
NAIBU spika wa bunge, JOB NDUGAI amewataka wazazi kuwalea vijana katika msingi bora ya  malezi ili taifa lipate  viongozi waadilifu na wenye kudumisha  amani nchini.
Ametoa wito huo mkoani Shinyanga katika tamasha la uzinduzi wa album ya Huima band ya jijini mwanza.
Amesema takwimu  za vijana  nchini zinaeleza kuwa  asilimia 70 ya vijana wenye umri wa  miaka 30 wameharibika  kimaadili.
Ndugai amesema wazazi na jamii inatakiwa kuwa makini na vijana katika suala la malezi bora ili lipatikane taifa lenye wasomi watakaojiajiri na kuajiriwa na si vinginevyo.
Amesema vijana wanachangamoto nyingi hivyo wadau wakiwamo viongozi wa dini wanapaswa kuongeza masomo ya uadilifu na uzalendo kwa vijana
Naibu spika huyo amesema  wengi wa vijana nchini wamekataa tamaa katika  mambo  mbalimbali hivyo jitihada za makusudi zinahitajika
Pamoja na mambo mengine amesema suala la ushoga  linazidi kushamiri na kuhatirisha  maadili ya nchi  hivyo amewataka wazazi na walezi kufuatilia mienendo ya vijana na kuwaelimisha madhara  ya vitendo viovu.
MOSHI
RAIS Jakaya Kikwete  hii leo amezindua  kampeni ya kupinga ukatili na matumizi ya nguvu dhidi ya wanawake.
Pia amezindua safari ya kupanda Mlima Kilimanjaro iliyopewa jina la “Kilimanjaro Speak Out, Climb Up”.
Amezindua hayo kwenye lango la hifadhi ya mlima Kilimanjaro (KINAPA),wilayani Moshi mkoani Kilimanjaro.
Mbali na kuanzisha kampeni hiyo, pia rais  atafungua mkutano wa mwaka wa maofisa waandamizi wa jeshi la polisi unaofanyika kwenye Chuo cha Polisi mjini Moshi.
Hiyo ni ziara ya kwanza ya rais Kikwete katika Mkoa wa Kilimanjaro tokea alipotembelea mkoa huo wakati wa kampeni za uchaguzi mkuu wa mwaka 2010 na aliwasili ktaika mji huo jana jioni.
KIBAHA
MAITI ya abiria waliopoteza maisha katika ajali ya mabasi mawili madogo ya abiria wilayani Kibaha wametambuliwa na baadhi wameanza kuchukuliwa na ndugu zao kwa ajili ya mazishi.
Akizungumza kwa niaba ya kamanda wa polisi mkoani Pwani, mkuu wa upelelezi wa mkoani humo Evance  Mwijage  amewataja marehemu waliotambuliwa ni:- James  Senga(49), Hadija  Abdulrhaman(25) na mtoto wake Abdallah  Juma (3 ½), Siwema Ally, (28) na mtoto wake Mariam  Ally (3)
MWIJAGE amesema majeruhi wanne kati ya 42 waliokuwa wamelazwa katika hospitali teule ya Tumbi wamehamishiwa katika hospitali  ya taifa ya Muhimbili kutokana na hali zao kuzidi kuwa mbaya.
Naye mganga mkuu wa hospitali ya Tumbi, Dk IZAACK LWALI amewataja majeruhiwa hao kuwa ni Kelvin Pius, (23), Josephat Lukio, (39), Muhsin Sonaga, (34) na Alex Masawe, (27).
Dk Lwali amesema majeruhi wengine 40 bado wanaendelea kupatiwa matibabu katika hospitali ya Tumbi na hali zao bado hazijatengemaa
Ajali hiyo ilitokea Machi 3 mwaka huu katika eneo la Kwa Mbonde Kibaha na ilihusisha gari T.986 ASF Toyota Coaster  likiendeshwa na dereva aliyejulikana kwa jina moja la babu (marehemu) ikitokea Dar es salaam kwenda mlandizi ambapo iligongana uso kwa uso na gari T318 AQY Isuzu Journey iliyokuwa kutokea Mlandizi kwenda Dar es salaam
Chanzo cha ajali hiyo ni dereva wa coaster kuyapita magari mengine kwa mwendo kasi bila kuchukua tahadhari yoyote na  kugongana uso kwa uso na Isuzu journey na kusababisa vifo vya watu sita papo hapo  na majeruhi 46.
ZANZIBAR
RAIS wa Zanzibar anatarajiwa kufunguwa mkutano wa mbegu za kilimo Afrika,  utakaofanyika Zanzibar Machi 7 hadi 8 mwaka huu.
Katibu wa Wizara ya Kilimo na Mali Asili Zanzibar, AFAN OTHMAN MAALIM, amesema mkutano huo utawakutanisha wafanyabiashara, wazalishaji, wasambazaji na wdau wengine wenye nia ya kuwekeza katika sekta ya kilimo Tanzania, pamoja na wataalamu wa sekta ya mbegu kutoka Tanzania na Afrika.
Amesema jumla ya mada nne zitajadiliwa katika mkutano huo, ikiwamo mchango wa magugu hatari kutokana na mbegu bora, changamoto za uzalishaji mbegu bora, changamoto katika biashara ya mbegu bora na maendeleo katika utafiti wa maeneo mapya ya mbegu bora.
Waziri huyo amesema mafunzo yatakayopatikana katika mkutano huo yatakuwa ni kichecheo kikubwa katika kuendeleza jitihada za Serikali mbili katika kuhakikisha kilimo kinaendeshwa kwa tija na kwa kutumia mbegu bora.
Mkutano huo ambao ni wa kwanza kufanyika Tanzania na  unatarajiwa kushirikisha  zaidi ya washiriki 200 kutoka Bara la Afrika na Ulaya, na utafungwa na waziri mkuu MIZENGO PINDA.

MACHI, 4, 2012
KAHAMA
WAZIRI wa maliasili na utalii, EZEKIEL MAIGE amewataka wananchi wilayani kahama mkoani Shinyanga kuyatumia vizuri mabonde yanayofaa kwa kilimo cha mpunga.
Amesema hatua hiyo itasaidia kupatikana kwa  chakula  cha uhakika na kingi ambacho kinaweza kulisha mkoa mzima wa Shinyanga.
Ametoa wito huo ikiwa ni siku chache  baada ya Waziri Mkuu MIZENGO PINDA kufanya ziara ya kikazi wilayani Kahama na kuyaona  mabonde yanayofaa kwa kilimo cha umwagiliaji   katika kata za Busangi, Chela, Ntobo, Ngaya, Segese, Ngogwa na Mbizi.
Pamoja na mambo mengi waziri mkuu huyo aliahidi kutuma wataalamu kutoka wizara ya kilimo na umwagiliaji kufanya utafiti kwenye maeneo hayo.
MAIGE ambaye pia ni mbunge wa jimbo  la Msalala, amewataka wananchi kuthaamini ardhi zao  ambazo amesema  zinazoweza kuwa msaada kwenye maisha ya baadaye na  familia.
Amesema kwa kutumia kilimo cha umwagiliaji, wananchi wanaweza  kuvuna na kupanda mazao mara mbili katika msimu mmoja.
BUKOMBE
WATU wanne wa familia moja waliokufa wilayani Bukombe baada ya nyumba walimokuwamo kuteketea kwa moto, wamezikwa jana majira ya saa kumi jioni katika makaburi ya AICT, ushirombo.
Watu hao walifariki papo hapo na wengine watatu   walijeruhiwa.
Tukio hilo lilitokea usiku wa kuamkia  jana  katika mtaa wa mission kata ya Igulwa Ushirombo  mjini.
Waliokufa ni  YUNIS  BLASH(31) ambaye ni mama wa watoto, GATUKULA  MWENYEJI(5), GRACE MWENYEJI(4),na  RODA MWENYEJI mwenye miezi  sita, ambao nao walikufa.
Waliojeruhiwa ni  baba wa familia hiyo MWENYEJI GATUKULA(36) na wanawe  SOFIA JAMES(22) na  Mzaire Mwenyeji (12) mwanafunzi shule ya msingi bomani ambao wamelazwa katika hospitali ya wilaya ya bukombe
Chanzo cha moto ulioteketeza  nyumba hiyo ni  mshumaa uliokuwa ukiwaka na nyumba ilianza kuungua majira ya saa nane usiku.
MUNGU AZILAZE ROHO ZA MAREHEMU MAHALA PEMA PEPONI,  AMIIN
BUKOMBE
JESHI la polisi wilayani Bukombe, mkoani Shinyanga  linawashikilia watu wawili kwa tuhuma za kuwaingilia kimwili wanafunzi wa shule ya msingi msasani wilayani humo.
Watu hao ni ROBATI SOSY(25) na MZOSI SOSY(30) ambao ni wapasua mbao katika msitu wa kigosi.
Wakiongea na redio KAHAMA FM wazazi wa  wanafunzi hao, ANTON KISABO na LUKWAJA ZAKALIA wamesema wanafunzi hao VERONICA ANTON(15) na SIWEMA LUKWAJA (13) walitumwa kufuata kuni majira ya saa TISA alasiri na walirudi saa TATU usiku.
Walipohijiwa na wazazi wao, walisema kuwa walikuwa na wanaume hao na kila mmoja alipewa ELFU 3 na kufanya nao mapenzi.
Wanafunzi hao ambao wamepelekwa hospitali ya wilaya kwa uchunguzi wamesema watuhumiwa hao waliwaangilia kimwili kwa zamu.
Watuhumiwa hao walikamatwa na SUNGUSUNGU na kufikishwa polisi na wanatarajiwa kufikishwa mahakamani uchunguzi utakapokamilika.
Afisa elimu wilyani BukombeDONALD MPANDA amethibitisha kutokea kwa tukio hilo na kwamba wote wanaofanya vitendo hivyo waache .
Pia ameiomba mahakama kuchukua hatua kali kwa watuhumiwa wanaobainika kufanya vitendo hivyo.


MACHI 3, 2012
BUKOMBE
WATU wanne wa familia moja wilayani Bukombe wamekufa papo hapo na wengine watatu   wamejeruhiwa baada ya nyumba walimokuwamo kuteketea kwa moto.
Tukio hilo limetokea usiku wa kuamkia leo katika mtaa wa mission kata ya Igulwa  Ushirombo  mjini.
Waliokufa ni  YUNIS  BLASH(31) ambaye ni mama wa watoto, GATUKULA  MWENYEJI(5), GRACE MWENYEJI(4),NA  RODA MWENYEJI mwenye miezi 6, ambao nao wamekufa.
Waliojeruhiwa ni  baba wa familia hiyo MWENYEJI GATUKULA(36) na wanawe  SOFIA JAMES(22) na  Mzaire Mwenyeji (12) mwanafunzi shule ya msingi bomani. Wote wamelazwa katika hospitali ya wilaya ya bukombe

Kamanda wa polisi mkoani Shinyanga, DIWANI ATHUMAN amesema  chanzo cha moto ulioteketeza  nyumba hiyo ni  mshumaa uliokuwa ukiwaka na kwamba nyumba ilianza kuungua majira ya saa nane usiku.
Baba wa familia hiyo MWENYEJI GATUKULA, amesema aliwasha mshumaa huo kufuatia mafuta ya taa kuisha katika taa.
Mganga mkuu wa wilaya ya  Bukombe ARCHAD RWEZAHULA amekili kupokelewa kwa maiti za  marehemu hao  na kwamba hali ya majeruhi si nzuri na wanaendelea kutibiwa.
Mbali na vifo hivyo , kumekuwapo na athara kubwa na  hadi sasa thamani yake haijajulikana,
Kufuatia tukio hilo kaimu mkuu wa wilaya ya Bukombe meja mstaafu BAHATI MATALA amewashukuru wananchi wa eneo hilo kwa jitihada za kuiokoa familia hiyo. Na ametuma  salamu za rambirambi kwa familia hiyo.
MUNGU AZILAZE ROHO ZA MAREHEMU MAHALA PEMA PEPONI,  AMIIN
SONGEA
KAMATI huru ya kuchunguza vurugu zilizotokea Songea Februari 22 mwaka huu, na kusababisha vifo vya watu wanne inatarajia kukamilisha kazi hiyo wiki ijayo badala ya jana.
Mkuu wa mkoa huo, SAIDI MWAMBUNGU ameiambia REDIO KAHAMA FM kuwa wakati ripoti hiyo ikisubiliwa, kila kata imeweka mikakati ya ulinzi shirikishi ambapo kila mkazi anapaswa kushiriki.
Amesema jitihada zinaendelea  kufanywa kwa kukutana na viongozi mbalimbali wakiwamo wa mila, dini na watu mashuhuri ili  kukemea uvumi na imani potofu ambazo amesema zinasababisha uvunjifu wa amani.
Pamoja na mambo mengine amewataka watanzania kuwa makini na kuachana na maneno ya uvumi.
Naye mwenyekiti wa kamati ya ulinzi na usalama  wilayani Songea ambaye pia ni mkuu  wilaya hiyo, THOMAS OLE SABAYA amesema anaendelea kufanya ziara kwenye kata zote 21 kwa ajili ya kuhamasisha wananchi kuweka ulinzi shirikishi kwenye maeneo wanayoishi .
Kutokana na mauaji hayo askari polisi wanne wanashikiliwa na jeshi la polisi kwa wakituhumiwa kwa mauaji hayo na raia 54 nao wamefikishwa mahakamani kwa kufanya maandamano kinyume cha sheria  na taratibu.

ARUMERU
KAMATI kuu ya CCM na ile ya CHADEMA kwa nyakati tofauti hii leo zimepitisha rasmi majina ya wagombea ubunge wa jimbo la Arumeru Mashariki, mkoani Arusha

CCM imemteua Sioi Sumari na CHADEMA imemteua Joshua Nassari na kampeni za uchaguzi zinatarajiwa kuanza Machi 9, na upigaji  kura utakuwa ni  April mosi, mwaka huu.
Akizungumza jijini Dar es Salaam jioni ya leo katibu wa itikadi na uenezi wa CCM taifa, NAPE NNAUYE amesema chama hicho  pia kimemteua rais mstaafu Benjamin Mkapa kufungua kampeni hizo na kufunga.
Pia kimemteua Katibu Fedha na Uchumi wa CCM,  LAMECK MWIGULU kuwa mratibu wa kampeni hizo.

Katika hatua nyingine Nape amesema CCM imetoa  baraka kwa Tasisi ya Kupambana na rushwa TAKUKURU kuendelea na mchakato wao wa kushughulikia watu waliokamatwa na rushwa katika kura za maoni za CCM jimboni humo.

Naye katibu mkuu wa Chadema Dk. Wilbrod Slaa akizungumza jimboni Arumeru Mashariki, amesema kwa pamoja wajumbe wote wameridhika na ushindi wa Nassari.

Mwenyekiti wa chama hicho, Freeman Mbowe amesema hadi sasa hakuna mpasuko wowote ndani ya chama hicho.

Kupitishwa kwa jina la Nassari kuna mfanya mgombea huyo kuwania jimbo hilo kwa mara ya pili baada ya mwaka 2010 kuangushwa na aliyekuwa mbunge wa jimbo hilo marehemu JEREMIA SUMARI.

Katika kura za maoni Nassari alifanikiwa kuibuka na ushindi wa kura 805  dhidi ya wajumbe 888 waliopioga kura kutoka vijiji 86 vilivyopo Jimbo la Arumeru.

Uchaguzi wa jimbo hilo unafanyika tena baada ya aliyekuwa mbunge wa jimbo hilo Jeremiah Sumari kufariki dunia hivi karibuni.

KIBAHA
JESHI la polisi mkoani Pwani linawashikIria watu  wanne  kwa tuhuma za wizi wa ng’ombe 45 wanaokadiriwa kuwa na thamani ya milioni 21.5

Kaimu kamanda wa polisi mkoani humo, SALEHE  MBAGA amesema ng’ombe hao waliibiwa walipokuwa wakirejea nyumbani kutoka malishoni katika kijiji cha madege dutumu wilayani Kibaha.
Kufuatia msako wa  jeshi la polisi, walifanikiwa kupata ng’ombe 17 kati ya 45 walioibwa na  watuhumiwa wanne wamekamatwa.
Watuhumiwa hao ni Samwel Shangwe (25), Born Subaida (25), Madege Dotto (30) na Kilabachenga Majuto (29).
Kamanda MBAGA amesema ng’ombe waliopatikana wamekabidhiwa kwa mmiliki MAJALIWA LAHALEY (66) na kwamba msako unaendelea na watuhumiwa watafikishwa mahakamani upelelezi ukikamilika.



MACHI, 2, 2012
BUKOMBE
JESHI la polisi  mkoani Shinyanga limewaondoa polisi waliokuwa wakilinda kwenye machimbo madogo ya dhahabu katika  shule ya msingi Ng’anzo wilayani Bukombe.

Na sasa  wanalinda askari wa idara ya maliasili.

Katibu tawala wa wilaya ya Bukombe, PAUL CHEYO ameiambia REDIO KAHAMA FM kuwa pamoja na hatua hiyo na baada ya mashimo ya dhahabu kufukiwa, ulinzi umeimarika na hakuna wachimbaji wanaoendelea na uchimbaji kwenye shule hiyo, baada ya kudhibitiwa na askari hao.

Amesema hatua ya kuondolewa kwa askari polisi ni kufuatia kuwapo kwa tuhuma kuwa wanaingiza watu katika machimbo hayo kinyemela.

Cheyo amesema kufuatia tuhuma  hizo kamanda wa polisi mkoani  Shinyanga,  DIWANI ATHUMANI alifikia uamuzi wa kuwaondoa katika eneo hilo.

Hatua hiyo imeelezwa kuwa itasaidia kuwaondoa wachimbaji wadogo wa dhahabu katika machimbo hayuo.

DODOMA
POLISI mkoani Dodoma inawashikilia viongozi watatu wa kijiji cha Zepissa, Kata ya Hombolo mkoani Dodoma kwa tuhuma za wizi na ubadhirifu wa fedha za mradi wa ujenzi wa zahanati.
Wanatuhumiwa kuiba milioni  3, laki tisa  na elfu kumi na tano.

Ofisa Tarafa wa Dodoma mjini  GERALD GUNINITA, amewataja viongozi hao kuwa ni mwenyekiti wa kijiji, DICKSON LUBOTE, mtendaji wa kijiji hicho,SARUJI HASSAN na mwenyekiti wa kamati ya ujenzi wa zahanati, ABIAZARI BWANZA.
GUNINITA amesema viongozi hao walikamatwa Februari 29 mwaka huu na  walighushi risiti za ununuzi wa vifaa vya ujenzi  na hati za malipo ya fundi.
Amesema tuhuma hizo zilibainika katika kikao cha kamati ya mipango miji na mazingira cha Manispaa ya Dodoma kilichofanyika Januari 11, baada ya  diwani wa kata ya Hombolo, MUSSA KAWEYA kulalamika kuwa ujenzi wa Zahanati hiyo umesimama kwa sababu kamati ya ujenzi ilikataa kupokea mifuko ya saruji 100 kwa kuwa fedha zilizotolewa zilikuwa ni za mifuko 200.


Alisema taarifa zilizopo zinaonyesha kuwa ujenzi wa zahanati hiyo hadi ulipofikia umegharimu milioni 22.7, jambo ambalo si kweli.

Diwani huyo alisema baada ya wakaguzi kufanya tathimini ya  ujenzi huo, walibaini kuwa gharama za ujenzi hazilingani na thamani ya fedha hizo.

Kamanda wa polisi mkoa wa Dodom, Zelothe Stephen alithibitisha kukamatwa kwa viongozi hao na kusema kuwa wameshahojiwa na wapo  nje kwa dhamana.
RUVUMA
Watumishi wa serikali ambao ni wanachama wa TUGHE wametakiwa kufanya kazi kwa bidii ili kutimiza wajibu wao na hatimaye waweze kupata haki ya kudai nyongeza ya maslahi kwa mwajili.
Wito huo umetolewa na katibu mkuu wa Tughe taifa ALLY KIWENGE alipokuwa akiongea na watumishi wa hospitali ya mkoa wa Ruvuma.
Amesema ili wafanyakazi waweze kuwa na sauti ya kudai hali bora ya maslahi kwa mwajili ni budi wao kwanza wakafanya kazi kwa bidii na kuzingatia taratibu.

Amezitaja taratibu kama kuwahi kazini na kuwajibika katika sehemu zao za kazi pia kuacha uzembe, uzururaji na kupiga majungu kuwa ndio nguzo za kuwa na Utendaji mzuri mahala pa kazi

Amewataka watumishi kuacha  maneno ya kejeli na uchochezi na tutumie vikao halali kuwasilisha kero na matatizo yetu kwa mwajili.
Kiwenge amesema kwa watumishi wazembe na wapika maneno sehemu za kazi Tughe haitojishughulisha kuwatetea endapo hatua za kinidhamu zitachukuliwa na waajiri.
Katika kikao hicho Kiwenge alitaja matatizo makuu manne ambayo serikali inapaswa kuyafanyia kazi kwa kipindi hiki ambayo ni nyenzo za kisasa za  kufanyia kazi katika hospitali zote nchini.

Pili, wafanyakazi kuwa na majadiliano na viongozi wao ili kuwe na ushirikiano katika kutatua kero zinazojitokeza mahala pa kazi kabla madhara hayajawafika wananchi.
Tatu, watumishi wa serikali kutoiingiza itikadi za kisiasa katika kazini.
Na nne, ni serikali kuchukua maamuzi magumu ya kuboresha maslahi ya watumishi wa umma ikiwamo kupandisha mishahara ya watumishi ili ikidhi mahitaji ya mwezi mzima..

DAR ES SALAAM
MAJADILIANO baina ya serikali na madaktari kuhusu madai yao yaliyowasababisha wagome mwezi uliopita, yameshindikana kuanza jana.
Hatua hiyo ni baada ya madaktari kutoka nje ya mkutano wakikataa kujumuishwa na makundi mengine ya watumishi wa kada nyingine za afya wanaofanya kazi nao pamoja.
Taarifa kwa vyombo vya habari iliyotolewa na ofisi ya waziri mkuu inasema baada ya hatu hiyo ya madaktari, makundi mengine yaliyobaki nayo yalikataa kuanza majadiliano bila ya kuwepo madaktari.
Madaktari hao wamesema wasingependa kufanya majadiliano hayo na serikali katika kikao kinachojumuisha kada nyingine za afya kama wauguzi, wafamasia, wanasayansi wa maabara za afya, wafiziotherapia na wataalamu wa mionzi kwa sababu wakiwa pamoja madai yao hayatopewa uzito stahiki.
Majadiliano hayo yaliitishwa na Serikali kufuatia maombi ya madaktari kwa Serikali ya kujadiliana nao kwa pamoja kuhusu utekelezaji wa madai yao baada ya Mkutano wao na Waziri Mkuu Februari 9, 2012 na kukamilika kwa kazi ya kamati iliyoundwa na Waziri Mkuu.
Akihutubia taifa  juzi , Rais JAKAYA KIKWETE alisema kamati aliyounda Waziri Mkuu kushughulikia madai ya madaktari imekamilisha kazi yake na kuwasilisha taarifa kwake na kwamba jana serikali ingeanza kuifanyia kazi taarifa hiyo na kuamua ipasavyo kulingana na uwezo uliopo.





MACHI 1, 2012
KAHAMA
MKUU wa wilaya ya kahama BAHATI MATALA ameagiza wanafunzi wote ambao walichaguliwa kujiunga kidato cha kwanza na hadi sasa hawajaanza masomo, kuripoti shuleni kabla ya Machi 5, mwaka huu.

Amesema yeyote atakayezembea zoezi hilo akiwamo afisa tarafa, watendaji wa kata na vijiji, watachukuliwa hatua za kinidhamu.

Agizo hilo linafuatia takwimu kuonyesha  kuwa baadhi ya wanafunzi wanaotakiwa kujiunga kidato cha kwanza bado hawajaripoti mashuleni kwa sababu mbalimbali.

Amesema pamoja na sababu hizo ni lazima wanafunzi hao waripoti shuleni na kwamba kila afisa tarafa atatakiwa kuwasilisha taarifa ya mahudhurio ya wanafunzi kwa mkono wake kabla ya Machi 7.

MATALA ambaye pia ni kaimu mkuu wa wilaya ya Bukombe mkoani Shinyanga amesema kwa mwanafunzi ambaye hajaripoti shuleni, ni lazima taarifa ieleze sababu na hatua zilizochukuliwa.
DAR ES SALAAM
RAIS Jakaya Kikwete amemuagiza mpiga chapa wa Serikali kuhakikisha vitabu vya katiba vinachapishwa kwa wingi ili wananchi waweze kuwa navyo na kuvisoma.
Amesema hatua yake hiyo ni kuhakikisha wananchi wanapata fursa pana ya kuielewa katiba iliyopo na kumuwezesha kuamua kwa usahihi anataka kupendekeza nini kiwemo katika Katiba mpya. 
Hivyo amewataka watanzania kujiweka tayari kutoa maoni yao kwenye tume na kwamba zoezi la kuunda tume hiyo  litakamilika katika muda mfupi kadri inavyowezekana, baada ya kupokea mapendekezo ya makundi. 
Amesema hayo katika hutoba yake ya kila mwisho wa mwezi.
Hata hivyo amesema pamoja na tume kuwa  itatengeneza utaratibu wa kuelimisha wananchi kuhusu katiba,  lakini amemtaka kila mtanzania aanze kuchukua hatua za kuifahamu katiba iliyopo sasa ili apate ufahamu wa maudhui muhimu ya katiba. 
Amesema tume imepangiwa kukamilisha kazi yake ndani ya miezi 18 na inaweza kuongezewa miezi miwili
Pia amesema kamati aliyoundwa kushughulikia madai ya madaktari imekamilisha kazi yake na kuanzia leo serikali itaifanyia kazi taarifa hiyo na kuamua ipasavyo kulingana na uwezo uliopo
Amesema pamoja na mgomo wa madaktari kwisha lakini  makovu yake yatabaki maisha katika kumbukumbu za historia ya taaluma ya tiba nchini.
Kuhusu maandamano ya Songea, amesema  vyombo vya usalama vinaendelea kufanya uchunguzi wa kina wa mauaji na kwamba wahusika wote watafikishwa mahakamani.
Pia amesema muda si mrefu, serikali na wadau wataanza mazungumzo kuhusu mapendekezo ya marekebisho kuhusu Bunge Maalum la katiba.
ZANZIBAR
KAMATI ya wazazi wa wanafunzi waliofutiwa matokeo ya mitihani Zanzibar imetoa muda wa siku saba kwa baraza la mitihani nchini (NECTA), kufuta adhabu ya wanafunzi hao kutofanya mitihani kwa muda wa miaka mitatu.
Agizo hilo limetolewa na wazazi hao  visiwani Zanzibar kufuatia kutoridhika na adhabu hiyo.
Katibu wa kamati hiyo SALEH MOHAMMED amesema uamuzi uliofikiwa na NECTA  ni kinyume na taratibu.
Amesema adhabu ya kuwafutia matokeo wanafunzi ilitosha na ni somo kwa wanafunzi  na kwamba hatua hiyo  ingekuwa ni faida kwa maslahi ya taifa.
Katibu huyo amesema kimsingi baraza hilo wakati linatoa hukumu hiyo halikuangalia zaidi maslahi ya taifa bali walitoa kwa utashi tu.
Hata hivyo amesema   kufanana kwa majawabu si suala la kushangaza kwa kuwa  mwalimu wa darasa  ni mmoja na wanafunzi wanasomeshwa  kitu kimoja.
Pamoja na mambo mengine kamati hiyo imeliomba baraza hilo kurejewa kwa mitihani Zanzibar, hatua ambayo itawapunguzia ubebaji wa lawama kwa kuondoa dhana ya kuvuja kwa mitihani.
ZANZIBAR
VIONGOZI wa dini nchini wametakiwa kutumia nafasi zao kuishauri serikali juu ya mambo mema ambayo yatasaidia kuiendeleza nchi kiuchumi na kuwahamasisha wananchi kulinda amani iliyopo.
Wito huo umetolewa visiwani Zanzibar na makamu wa kwanza wa rais wa Zanzibar MAALIM SEIF SHARIF HAMAD katika mazungumzo yake  na  Mufti Mkuu wa Zanzibar Sheikh SALEH OMAR QABI.
Amesema viongozi wa dini wana nafasi kubwa ya kuishauri serikali kuhusu  mambo yenye maslahi kwa taifa, na kuikosoa pale wanapoona inakwenda kinyume na maadili au misingi ya taratibu za nchi kwa maslahi ya wananchi.
Maalim Seif amempongeza Sheikh Qabi kwa kuteuliwa kushika wadhifa huo, na kwamba ana matumaini makubwa na uongozi wake kutokana na uwezo alionao kiutendaji.
Naye mufti  huyo ameupongeza uongozi wa awamu ya saba kutokana na mwamko wake wa kuondoa tofauti zilizokuwepo miongoni mwa wananchi na kuwafanya wananchi kuishi katika hali ya upendo.
Amesema mafanikio hayo yamepatikana kutokana na moyo walionao viongozi, na kuwaomba viongozi hao kuendelea kufanyakazi kwa ushirikiano na kupendana, ili kuliongoza vema taifa.

FEBRUARI, 29, 2012
KAHAMA
MKUU wa wilaya ya kahama, mkoani Shinyanga, BAHATI MATALA amewataka wakulima kung’oa mazao yaliyokauka na kupanda upya mazao yanayokomaa kwa muda mfupi na yale yanayostahamili ukame.
Pia amesema mawakala wameagizwa kuendelea kutoa pembejeo zenye ruzuku ili wakulima wakulima waweze kujinusuru na baa la njaa.
Amesema hatua hiyo ni kufuatia mvua za masika kuanza kunyesha.
MATALA ambaye pia ni kaimu mkuu wa wilaya ya Bukombe amesema mbegu za mtama na mahindi yenye kukomaa kwa muda mfupi zimesambazwa na zinaendelea kusambazwa katika maeneo mbalimbali za wilaya hiyo.
Hivyo amewataka viongozi wote wakiwamo maafisa tarafa, madiwani, watendaji kata na serikali za vijiji kuwahamasisha wakulima, kulima.
Pamoja na mambo mengine amewapongeza wakulima kwa juhudi kubwa wanazozifanya katika shughuli za kilimo.
SHINYANGA
IDARA ya uhamiaji,mkoani Shinyanga imewakamata wahammiaji haramu 255 kutoka nchi 14 ambao waliingia nchini kinyume cha taratibu huku idadi kubwa wakiwa ni Warundi na Wanyarwanda.
Mkuu wa uhamiaji mkoani  Shinynga,SELEMANI KAMEYA amesema idadi hiyo ni kubwa ikilinganisha na mwaka 2010, ambapo jumla ya wahamiaji 199 walikamatwa 
Wahamiaji hao ni 20 kutoka nchini Kenya,  40 Burundi, 36 Rwanda, Kongo 11, Bangladesh 4, Uganda 12, India 8, Urusi 1, Israel 3, China 16, Canada1, Lebanon 2 na Nigeria 3.
Kameya amesema watu hao walifikishwa kwenye vyombo vya sheria na kwamba walichukuliwa hatua mbalimbali za kisheria ikiwamo kufungwa, kutozwa faini  na wengine kurejeshwa makwao.
Pamoja na changamoto mbali mbali idara ya uhamiaji  imeweza kukusanya milioni 140 kutoka vyanzo mbalimbali vya mapato,ikiwamo uuzaji wa passport za vitabu 603, Hati za dharura 10,514, Hati za Ufuasi 184, Hati za ukaazi madaraja ABC 331 na Hati za Msamaha 18.
 Kufuatia hali hiyo amewataka wananchi kuwafichua wageni hasa wanaoingia nchini kinyume na utaratibu.
Naye mkuu wa mkoa wa Shinyanga, ALLY RUFUNGA amezitaka halmashauri zote za wilaya kutenga  bajeti maalumu ya kutoa elimu kwa wananchi kuhusu kujua sheria za uraia na uhamiaji .SONGEA
MAHAKAMA za mwanzo 47  mkoani Ruvuma zinakabiliwa na uhaba wa mahakimu na kusababisha kuwapo kwa mrundikano wa kesi katika mahakama hizo.
Msajiri wa mahakama kanda ya Songea, WILFRED DYANSOBERA amesema  mkoa  huo una jumla ya  mahakimu 25 wa mahakama za mwazo tu.
Amesema kutokana na upugufu huo, mahakimu  hulazimika kufanya kazi katika zaidi ya mahakama mbili tofauti.
DYANSOBERA amesema mahakimu wanalazimika kufanya hivyo ili kupunguza mrundikano wa kesi na kwamba wanafanya kazi katika mazingira magumu ikiwamo kujigharamia wenyewe usafiri kwenda katika mahakama nyingine.
Amesema hakimu wa mahakama ya mwanzo wa Mfaranyaki  iliyopo Songea mjini analazimika kwenda kufanya kazi kwenye mahakama nyingine zilizopo  katika vijiji vya Gumbiro, Mahanje na Likuyufusi.
Amesema wilaya ya Tunduru ina mahakama za mwanzo 11,  mahakimu 4, wilaya ya  Mbinga ina mahakama za mwanzo 15 mahakimu  9, wilaya ya Namtumbo ina mahakama 10 na mahakimu  5 na wilaya ya Songea ina mahakama 11 na  mahakimu waliopo ni 7.
DAR ES SALAAM
WAZIRI mkuu MIZENGO PINDA amesema ili nchi iweze kunufaika na maliasili ilizonazo, kuna haja ya kutumia wawekezaji wa ndani na kama itashindikana, utumike mfumo wa ubia katika utafutaji wa maliasili hizo.
Ameyasema  hayo jijini Dar es Salaam katika  ufunguzi wa majadiliano ya jinsi ya kutumia vema maliasili na kuhakikisha zinalitajirisha bara la Afrika.
Amesema mikutano ya majadiliano kama hiyo inapaswa kusaidia kutoa mafunzo kwa Watanzania ili wajue namna ya kusimamia vizuri zaidi maliasili za nchi.
PINDA amesema ni lazima watanzania wafundishwe na kujengewa uwezo wa jinsi ya kuwekeza katika utaalamu, mitaji, mitambo na kwenye teknolojia ili tuache kutegemea vyanzo  kutoka nje ya nchi.
Amesema kinyume na hivyo nchi itaendelea kutonufaika  na maliasili zetu ikiwamo almasi, mafuta, gesi na dhahabu.
Waziri mkuu huyo amesema balaa ama laana ya kutonufaika na rasilmali imezikumba nchi nyingi za Afrika, na kwamba nyingi  zimekumbwa na vita  vya wenyewe kwa wenyewe, vita baina ya nchi.
Pia amesema nchi zimepoteza  fedha nyingi,  maisha ya watu wengi wasio na hatia hasa wanawake na watoto na wengine wamebakia vilema kutokana na vita hivyo.
Amesema Tanzania iko tayari kushirikiana na wabia wa maendeleo, taasisi za kimataifa, sekta binafsi au watu binafsi ili kuhakikisha inawajengea uwezo wananchi wake katika maeneo tofauti yakiwemo ya utafutaji, uongezaji thamani na uuzaji wa maliasili tulizonazo.
 ZANZIBAR
MAKAMU wa kwanza wa rais visiwani Zanzibar Maalim Seif Sharif Hamad amesema serikali inalizingatia kwa umakini suala la kuwaenzi wastaafu ili kulinda heshima yao.
 Amesema wastaafu wengi baada ya kustaafu wanafanya kazi zisizoendana na taaluma zao na kwamba serikali inalitafutia ufumbuzi suala hilo.
Ameyasema hayo visiwani zanzibar alipokuwa akizungumza na viongozi wa umoja wa wanamaji wastaafu Zanzibar.
Pamoja na mambo mengine  amewapongeza kwa kuanzisha umoja huo ambao utawasaidia kukabiliana na kero zinazowakabili.
Mwenyekiti wa umoja huo, LALI MFAMAU  amesema wafanyakazi wengi wa vikosi wanastaafu wakiwa bado wana uwezo wa kufanya kazi, hivyo wameamua kuanzisha umoja huo kwa lengo la kuwaunganisha na kuangalia namna ya kukabiliana na tatizo la ajira kwa wafanyakazi hao baada ya kustaafu.
Amesema  wastaafu hao wapatao 242 wako tayari kushirikiana na serikali katika kutumia ujuzi wao ikiwa ni pamoja na kukabiliana na maafa wakati yanapotokea.



FEBRUARI, 28, 2012
SHINYANGA
WAZIRI mkuu MIZENGO PINDA amewataka watanzania kujitokeza kwa wingi   katika  utoaji maoni ya uundwaji wa katiba mpya  na katika  zoezi la  sensa la  kutambua idadi halisi ya watanzania.
Ametoa wito huo katika kiwanja cha shycom mjini shinyanga alipokuwa akihitimisha  ziara yake ya kikazi katika wilaya zote za mkoa wa shinyanga.
Amewataka wananchi  kujitokeza bila ya kujali itikadi za kidini wala chama chochote.

Pinda amesema wananchi wanatakiwa kujitokeza kwa wingi katika kushiriki kwenye sensa itakayoanza mwezi Agosti  ili kujua idadi ya watanzania bila ya kuwa na hofu yoyote.

Amesema mkoa wa shinyanga wwenye  ukumbwa wa km ELFU 55, unajumla ya wakazi million 4.1, idadi ambayo ni  kumbwa na mkoa unakabiliwa na  changamoto nyingi na kwamba ndio maana serikali imefikia uamuzi wa kuugawanya na kuwa mikoa miwili Shinyanga na Simiyu ili kuongeza chachu ya maendeleo nchini.

Hivyo amewataka wananchi wa wilaya ya Bariadi na Maswa kuacha kugombania mahala pa kuwapo makao makuu na kwamba busara na hekima itumike  katika kupata muafaka wa suala hilo.
Katika hatua nyingine amesema zaidi ya asilimia 80 ya wakulima katika  mkoa wa shinyanga hawana elimu ya kilimo hivyo serikali imeweka mpango mkakati wa kutoa elimu hiyo ili kilimo kiwe na tija.

DODOMA
CHAMA cha walimu (CWT) mkoani  Dodoma kimeitaka serikali kumuwajibisha diwani wa Kata ya Chahwa, JOSEPH CHAHONZA kwa kitendo chake cha  kuwatishia walimu na kusababisha kuikimbia shule ya msingi Chahwa.

Mwenyekiti wa CWT mkoani humo, LUKAS LUHOMBA amesema kitendo kilichofanywa na diwani huyo ni cha kinyama na udhalilishaji kwa walimu na kwamba kisipofanyiwa kazi kinaweza kudidimiza elimu katika kata hiyo.
Amesema mgogoro wa Chahwa ni wa muda mrefu na hadi sasa bado haujapatiwa ufumbuzi hali inayopelekea kila mwalimu anapelekwa shuleni hapo, baada  ya muda kukimbia kutokana na kupewa vitisho.
Pia kutokana na hali hiyo, manispaa imelazimika kuwahamisha walimu kwa mkupuo na kwamba itawapeleka walimu hadi kutakapokuwapo usalama.

Hata hivyo diwani huyo amekanusha madai hayo na kueleza kuwa kilichotokea ni hali ya kutoelewana kati walimu na wanakijiji kutokana na baadhi ya walimu kuwa na mahusiano ya kimapenzi na wasichana shuleni na kijijini hapo.

MBEYA
WAMILIKI wa shule binafsi wameitaka serikali kutobadili  mitaala ya vitabu mara kwa mara na kwamba hali hiyo inachangia  wanafunzi kutofanya vizuri  katika mitihani ya kuhitimu elimu ya msingi na  kidato cha nne.
Ombi hilo limetolewa mkoani Mbeya na makamu mwenyekiti wa wamiliki wa shule binafsi   kutoka mikoa ya Nyanda za juu kusini (TAMOSCO) MBOKA MWAMBUSI  wakati akifungua semina inayoshilikisha  viongozi kutoka serikalini, wakuu wa shule na wamiliki.
Amesema ni wakati muafaka  serikali kukaa meza moja na wamiliki wa shule binafsi ili kupata njia sahihi za kukabiliana na  changamoto mbalimbali katika sekta ya elimu ikiwamo wanafunzi wanaokosa nafasi za kujiunga na shule za serikali.
MWAMBUSI amesema kutofanya vizuri kwa wanafunzi nchini ni moja ya chanamoto kubwa ambayo inatakiwa kupatia ufumbuzi wa haraka na uliomakini.
Pamoja na mambo mengine ametaka kuwapo kwa ushirikiano  wa kishule ikiwamo shule binafsi na za serikali ili kuwajengea uwezo wanafunzi wa kubadilisha matirio ya kimasomo.

DAR ES SALAAM
KAMATI kuu ya CCM imeamua upigaji kura za maoni kumpata mgombea wake katika uchaguzi mdogo jimbo la Arumeru Mashariki urudiwe.
Leo jijini Dar es Salaam katibu wa, Itikadi na Uenezi wa CCM taifa, Nape Nnauye amesema, kikao hicho chini ya mwenyekiti wa CCM, Rais Jakaya Kikwete kimeamua upigaji kura huo urudiwe kwa kuwa katika matokeo ya upigaji kura uliopita, hakuna mgombea aliyepata kura zinazovuka asilimia 50 ya kura zote.
Amewataja watakaochuana kwenye marudio hayo kuwa ni, Wiliam Sarakikya na Sioi Solomon.
Katika kura za maoni zilizopita, Sioi aliongoza kwa kura 361 wakati Sarakikya aliyeshika nafasi ya pili alipata kura 259 huku Elishilia Kaaya aliyeshika nafasi ya tatu alipata kura 176.
Nape amesema uchaguzi huo wa kura za maoni utarudiwa Machi 1, mwaka huu na wapigakura wale wa  mkutano mkuu wa jimbo  hilo.
Amesema, uchaguzi huo utasimamiwa na Makamu Mwenyekiti wa CCM (Bara) Pius Msekwa , Naibu Katibu Mkuu wa CCM (Bara) Kapteni Mstaafu, John Chiligati na Mwenyekiti wa CCM mkoa wa Kagera, Costancia Buhiye.

Nape amesema siku itakayofuata  ya Machi 2, kamati ya siasa ya wilaya itapitisha majina ya wagombea hao na baadaye siku hiyo hiyo jioni kamati ya siasa ya mkoa itapitia mapendekezo ya wilaya kabla Kamati Kuu kupitisha rasmi jina la mgombea Machi 3.
Kwa mujibu wa Tume ya Taifa ya Uchaguzi(NEC), uchaguzi mdogo jimbo la Arumeru Mashariki utafanyika Aprili Mosi mwaka huu, baada ya vyama vitakavyoshiriki kwenye uchaguzi huo kuchuana katika kampeni ambazo zitaanza  rasmi Machi 9, mwaka huu.
Uchaguzi huo unafanyika kufuatia jimbo hilo kubaki wazi baada ya aliyekuwa mbunge wa jimbo hilo, JEREMIAH SUMARI kufariki dunia hivi karibuni.


FEBRUARI, 27, 2012
SHINYANGA
VIONGOZI wa vyama vya wafanyakazi mkoani Shinyanga wametakiwa kuacha kuibiana  wanachama na kwamba wawe mstari wa mbele kutetea haki za wafanyakazi na wajiepusha na vitendo vya rushwa.
Wito huo umetolewa na naibu katibu mkuu wa shirikisho la vyama vya wafanyakazi nchini (TUCTA) HEZRON KAAYA katika mkutano mkuu wa kuchagua viongozi wa  shirikisho  hilo mkoani Shinyanga.
Amesema viongozi wa vyama vyote vya wafanyakazi wanatakiwa washikamane na kusimama kidete katika kutetea haki za wafanyakazi nchini na kuwasaliti.
Katika uchaguzi huo ESTER ODARI amechaguliwa kuwa mwakilisha wa wanawake wa mkoa na nafasi ya mratibu imechukuliwa na Tabu Mambo ambaye  hakuwa na mpinzani.
Nafasi ya mwenyekiti wa shirikisho hilo imechukuliwa na FUEL MLINDOKO ambaye ametetea kiti hicho kwa kupata kura zote.

Baada ya kutetea kiti chake hicho, amewataka wafanyakazi nchini kote kushirikiana na kuwa kitu kimoja katika kutetea maslahi yao na kwamba kusalitiana  kutokana na kupewa rushwa ni sawa na kulaaniwa.

MBEYA
NEEMA EDSON ( 19) mkazi wa Namtanga Swaya jijini Mbeya amefikishwa katika mahakama ya mkoa kwa kosa la kumuua mtoto wake akiwa mchanga.


Akisoma shitaka hilo mbele ya hakimu mkazi mfawizi MONIKA NDYEKOBOLA mwanasheria wa serikari EMA MSOFE amesema mshtakiwa alitenda kosa hilo Januari 3 mwaka huu maeneo ya namtanga jijini  humo.

MSOFE amesema  pindi mahakama itakaporidhika na ushahidi itoe  adhabu kali kwa mtuhumiwa ili iwe fundisho kwa wengine

Amemtaja mtoto aliyeuawa kuwa ni STEVEN CHINGA aliyekuwa na umri chini ya miezi kumi na miwili kinyume na kifungu cha sheria namba 199 sura ya 16 kama kilivyofanyiwa marekebisho mwaka 2002.

Hata hivyo mshtakiwa hakutakiwa kujibu lolote na kwamba kesi hiyo itaanza kusomwa upya februari 6 mwaka huu katika mahakama kuu.

ARUSHA
WAZIRI wa Ujenzi  Dk JOHN MAGUFULI amesema Tanzania inakabiliwa na changamoto kubwa ya tatizo la makazi ya wananchi na watumishi wa umma
Ametoa kauli hiyo mjini Arusha alipokuwa akiweka jiwe la msingi wa majengo mawili ya ghorofa 10 yanayojengwa na serikali kupitia wakala wa Majengo (TBA) mkoani humo.
Majengo hayo yanatarajia kugharimu zaidi ya bilioni 10.2 hadi kukamilika na hadi sasa yamekwishagharimu bilioni 5.2
Waziri Magufuli amesema kati ya asilimia 70 hadi 75 ya wananchi nchini  wanaishi katika makazi holela na kwamba nchi inamahitaji ya  zaidi ya nyumba milioni tatu katika maeneo mbalimbali.
Amesema tangu nchi ipate uhuru  mwaka 1961, serikali imekuwa ikumudu kutoa  huduma ya makazi kwa watumishi wake kwa asilimia 3 tu, hatua ambayo imesababisha kuwepo na mahitaji makubwa ya nyumba kwa watumishi wake

Hata hivyo amesema wakala wa majengo inatarajia kujenga nyumba zaidi ya 10,000 kwa ajili ya makazi ya watu wakiwemo watumishi wa umma katika mwaka huu wa feha 2011 / 2012
DAR ES SALAAM
MKAGUZI mkuu wa ndani wa serikali, MOHAMED MTONGA ameagiza wakaguzi wote wa ndani kuhakikisha wanasimamia rasilimali za nchi vizuri kwa niaba ya wananchi ili miradi ilinganishwe na thamani ya fedha iliyoombewa.
Ametoa agizo hilo jijini Dar es salaam alipokuwa  akifungua mkutano wa siku tatu wa wakaguzi wa ndani wa halmashauri za serikali za mitaa na Sekretarieti za mikoa
Amesema inasikitisha kuona ubadhirifu wa mali za umma ikiwamo ujenzi wa madarasa yasiyokidhi  viwango unatokea mita chache kutoka ilipo ofisi ya mkaguzi wa ndani au mtaa anaoishi bila kuchukua hatua zinazostahili za kuhakiki kama kweli mradi huo unalingana na fedha zilizotolewa na serikali.
Pia MTONGA amewaagiza wakaguzi  hao kuwa wabunifu ili wawe wasimamizi wazuri wa rasilimali na fedha za umma kwa niaba ya wananchi bila kujali kuwa wanavifaa vya kutosha au hawana .
Pia amewaonya kuepukana na  mitandao inayowafanya kikiuka sheria na taratibu za fedha na kupelekea  kutoa taarifa zisizosahihi za ukaguzi wa ndani na hivyo kusababisha upotevu wa fedha za umma.
Katika hatua nyingine  amesema  ofisi yake inaandaa mwongozo utakaowasaidia wakaguzi wa ndani kukagua  bajeti na kuangalia utekelezaji wake.
Amesema  hatua hiyo inalenga kuhakikisha kunakuwapo na uwazi na uwajibikaji kwa watendaji na wananchi.


FEBRUARI, 26, 2012
BUKOMBE 
WAZIRI MKUU Mizengo  Pinda ameshitushwa na kasi ya ongezeko la asilimia 7.4 la  idadi ya watu kuzaana wilayani Bukombe ambapo kila kaya inawastani wa watu saba.
Amesema pamoja na kwamba   kuzaliana huko kwa kasi ni neema lakini ni mzigo kwa familia na kwa taifa pia.
Kufuatia hali hiyo waziri Pinda ameagiza kutolewa  kwa elimu ya uzazi wa mpango kwa wananchi wilayani humo.
Pia ameagiza kupambana na kudhibiti ongezeko la maambukizi ya ukimwi  kufuatia wilaya hiyo kukumbwa na  asilimia 6.6 ya maambukizi.
Wakati huo huo, waziri mkuu amesema serikali ipo katika hatua ya kujenga soko la kisasa katika kanda ya ziwa ikiwamo kiwanda na machinjio ya kisasa ili kuwasaidia wafugaji kuuza mifugo yao

Amesema  hatua hiyo itawasaidia wafugaji hao kujiongezea  kipato  kwa kuwa watakuwa na soko karibu.


Waziri mkuu Pinda  Amesema kwa sasa watakaa na viongozi wa mikoa ya kanda hiyo kwa ajili ya kupanga namna ya kujenga soko hilo pamoja na kupanga namna ya kuwapatia wafugaji elimu  ya ufugaji wa kisasa

Amesema bila wananchi kupatiwa elimu  soka hilo halitawasaidia  na kwamba    migodi mingi katika  ukanda huo inanunua nyama toka nje ya mikoa hiyo  na kwamba ili kuwarudisha  lazima wajenge  viwanda na  machinjio ya kisasa
Pia amesema tatizo kubwa la wafugaji wa mifugo kuendelea kuwa na maisha duni  inatokana na  kuwa na uelewa mdogo  juu ya kufuga ambapo hufuga  mifugo mingi ambayo huwasumbua kuitunza.
Amesema  wakati  umefika kwa wafugaji kupewa  utaalamu wa kupunguza mifugo  na kufuga  kisasa.
KONGWA
SERIKALI imetakiwa kuliangalia kwa mtazamo maalumu na wa kipekee kundi la vijana ili kuendelea kujenga  taifa imara, lenya amani na utulivu.
Wito huo umetolewa na mwenyekiti wa umoja wa vijana wa CCM mkoani  Dodoma ANTON MAVUNDE, alipokuwa akifungua tawi la vijana wa Shule za Sekondari kata ya Sejeli wilayani Kongwa.
Amesema vijana ndio nguvu kazi inayotegemewa na taifa lolote duniani hivyo lisipoangaliwa kwa umakini litahatarisha amani ya nchi.
Pamoja na mambo mengine amevitaka vyama vya siasa navyo kuwasaidia vijana katika kufikia malengo mbalimbali.
Amesema hata wanasiasa ni vema wakaacha ubinafsi usiokuwa na maana na wajikite kwa dhati kuwasaidia vijana kwa mustakabali mzuri wa nchi.

MAVUNDE amesema utulivu na amani ya nchi inaweza isiwepo  endapo vijana wataendelea  kukosa kazi za kufanya kwa kujiajiri au kuajiriwa.

Hata hivyo amewataka vijana  kuacha kunung’unika kwa kila jambo na kwamba  watimize wajibu wao kikamilifu ikiwamo kukubali kukaa katika vikundi ili waweze kufikiwa kwa urahisi.
Kuhusu uchaguzi wa CCM na jumuiya zake, amewataka vijana kujitokeza kwa wingi bila kuogopa, kugombea katika nafasi mbalimbali.

CHUNYA
ZAIDI ya wanafunzi  400 wa shule ya msingi  Gua katika kijiji cha Gua Wilayani Chunya wameshindwa kuendelea na masomo kwa ukosefu wa vyoo.
Kaimu mkuu wa shule  hiyo, EFEDI TWEVE amesema  uongozi wa shule umelazimika kuwasimamisha kuendelea na masomo wanafunzi kuanzia chekechea, hadi darasa la  tano .
Amesema kutokana na hali hiyo wanafunzi  wataendelea kukaa nyumbani hadi hapo ujenzi utakapokamilika na kwamba ujenzi huo unasuasua  kutokana na wananchi kutokuwa na mwamko wa kuchangia fedha za miradi ya maendeleo ikiwamo ujenzi wa  madarasa.
TWEVE amesema hali hiyo itachangia kwa kiasi kikubwa wanafunzi kuwa nyuma kimasomo  hasa wa darasa la nne na saba na ikizingatiwa kuwa  shule hiyo inaupungufu wa walimu
Mwanafunzi CATHERINI JOSEPHAT wa darasa la saba amesema wapo katika wakati mgumu na wanalazimika  kujisaidia katika vyoo vya zahanati na vichakani.
Hata hivyo mzazi SALOME MWAIKALA amesema wananchi wamekwua wakichangia ujenzi wa vyumba vya madarasa na vyoo lakini kikwazo kikubwa ni viongozi wa vijiji na kata kushindwa kusimamia kikamilifu miradi hiyo na kwamba wanaitumia michango kwa  maslai  binafsi.

Hivyo ameiomba serikali kuingilia kati suala hilo na kwamba maendeleo wilaya ya chunya yanakwamishwa na  viongozi wa vijiji na kata.
MBINGA
MWANAFUNZI Vaileth Tweve (14)  wa kidato cha kwanza katika shule ya Sekondari Depaul amekufa papo hapo na wengine 16 wamejeruhiwa baada ya kupigwa na radi.
Tukio hilo limetokea katika kijiji cha  Mbangamawe wilayani mbinga mkoani Ruvuma,  majira ya saa saba mchana wakati wanafunzi hao na wengine wakisubili chakula cha mchana
Kamanda wa polisi wa mkoani Ruvuma MACHAEL KAMUHANDA  amesema majeruhi wamelazwa katika hospitali ya wilaya hiyo na hali zao zinaendelea vizuri
Amesema radi hiyo imetokea wakati kukiwa hakuna mvua na jua lilikuwa linawaka.


FEBRUARI, 24,  2012
KAHAMA
WAZIRI mkuu MIZENGO PINDA  leo  Ijumaa  ameanza ziara ya siku mbili wilayani kahama ikiwa ni sehemu ya ziara yake ya siku nane mkoani Shinyanga kukagua shughuli za maendeleo katika wilaya zote saba za mkoa huo.
Ziara yake hiyo iliyoanza Jumatatu wiki hii ilianzia  wilayani  Maswa, Bariadi, Meatu, Kishapu.
Baadaye hii leo atakwenda wilayani  Bukombe, na kisha kurejea Kahama, na keshokutwa  atakwenda Shinyanga Vijijini na kumalizia Shinyanga Mjini.
Katika wilaya zote hizo, waziri mkuu amehutubia mikutano ya hadhara na kusalimiana na wananchi kwenye baadhi ya miradi atakayoikagua.
Wilayani  kahama ataweka jiwe la msingi katika  mradi wa umwagiliaji maji huko Chela, na kwenye karakana ya kilimo iliyoko Kahama mjini. wilayani Bukombe atakagua shamba la uzalishaji mbegu bora za mihogo katika gereza la Kanegele
Akiwa wilayani Meatu amekagua josho la mifugo la Mwamihanza, shamba darasa la pamba, na kukagua mradi wa umeme vijijini katika kijiji cha Mwandoya
Wilayani Kishapu amekagua shamba la mbegu bora la mtama katika kijiji cha Mwamashele.
Akiwa Shinyanga, waziri mkuu atafungua ghala la mazao la kijiji cha Lyabusalu na kukagua hospitali ya wilaya ya Shinyanga iliyoko ISELAMAGAZI.
Pia atakagua kiwanda cha nyama kilichopo Old Shinyanga na kuzindua Chuo cha VETA Shinyanga.
Jumatatu ijayo ya Februari 27, atafanya majumuisho ya ziara yake katika mkoa huo kwenye ukumbi wa mikutano wa NSSF na kurejea jijini Dar es Salaam mchana huo huo.
 BUKOMBE
IMEELEZWA kuwa vita dhidi ya rushwa nchini haiwezi kufanikiwa kwa kutegemea sheria pekee na kwamba inahitajika mabadiliko ya  tabia na mwamko mpya wa  maadili ikiwamo uchamungu.
Hayo yamesemwa  na mkuu wa taasisi ya kuzuia na kupambana na rushwa  (TAKUKURU) wilayani Bukombe, CASIUS  KYARO kwenye warsha ya siku moja mjini ushirombo ya kujadili mbinu mbadala ya kutokomeza vitendo vya rushwa, iliyowakutanisha maimamu na wachungaji .
KYARO amesema rushwa ni haramu na ni sumu katika jamii kwa kuwa athali zake  zinazorotesha haki, utawala bora, mfumo mzima wa utawala na hivyo kudumaza maendeleo binafsi na ya nchi.
Pamoja na mambo mengine amesema  miongoni mwa sababu za kuwapo kwa rushwa ni mmomonyoko wa maadili, tamaa, na ubinafsi.
Hivyo amewaomba viongozi wa dini na wadau wengine kutumia nafasi zao kuhakikisha vitendo vya rushwa vinatokomezwa na kujenga jamii yenye maadili mema.
Warsha hiyo iliandaliwa ili kuwajengea uwezo viongozi wa dini katika kukabilina na kudhibiti vitendo vya rushwa.
ARUSHA
TANZANIA ipo katika mchakato wa kutengeneza sera ya makuzi na malezi  ya mtoto kwa kutoa elimu ya awali  nchini.
Kufuatia mpango huo kila shule itatakiwa kuwa na shule ya awali na kwamba  maandalizi ya kupata walimu umekamilika.
Hayo yamesemwa mkoani Arusha  na waziri wa elimu na mafunzo ya ufundi stadi Dk SHUKURU KAWAMBWA katika jukwaa la kwanza la kitaifa linalojadili utungwaji sera ya makuzi na malezi ya awali ya mtoto.
Amesema sera hiyo inalenga kujali, kuthamini na kugundua vipaji vya watoto na kwamba huko ndiko  kujenga msingi wa awali wa mtoto ili anapoanza elimu ya msingi anakuwa na msingi imara.
Pia amesema sera hiyo itazingatia umuhimu wa serikali kutoa chakula mashuleni.
DAR ES SALAAM
MAMLAKA ya Chakula na Dawa (TFDA) imetahadharisha kuwapo kwa dawa bandia ya kutibu ugonjwa wa Malaria nchini .
Dawa hiyo inaitwa Eloquine (Quinine Sulphate 300mg U.S.P) na ipo katika makopo ya vidonge elfu moja kila moja.
Maelezo yaliyopo katika lebo  yanaonesha kuwa dawa hiyo imetengenezwa na kiwanda cha Elys Chemical Industries Ltd cha nchini Kenya. 
Hata hivyo, TFDA imebaini kuwa kiwanda cha Elys Chemical Industries Ltd hakitengenezi dawa yenye jina la biashara la ‘ELOQUINE’.
TFDA imesema kiwanda cha Elys Chemical Industries Ltd kimebainisha tofauti mbalimbali zilizopo katika lebo ya dawa bandia ikilinganishwa na dawa halisi inayotengenezwa na kiwanda hicho iliyosajiliwa na TFDA na hivyo kuthibitisha kuwa kiwanda hicho hakitengenezi dawa hiyo.
Uchunguzi wa dawa bandia katika maabara umebaini kuwa vidonge hivyo havina kiambato hai cha Quinine Sulphate kwa ajili ya kutibu ugonjwa wa Malaria, hivyo matumizi yake ni hatari kwa afya ya binadamu.
Katika kudhibiti usambazaji wa dawa hiyo nchini, hadi sasa TFDA imekamata jumla ya makopo 155 ya dawa hiyo bandia ya Eloquine jijini Dar Es Salaam yaliyokuwa yakisubiri kusambazwa.
Pia kopo moja lenye vidonge 115 limekamatwa Moshi, Kilimanjaro na mtuhumiwa mmoja amefikishwa  mahakamani na  wasambazaji wa dawa hiyo wanaendelea kwa kushirikiana na Jeshi la Polisi.
ZANZIBAR
SERIKALI ya Msumbiji imeiomba Tanzania kufikiria uwamuzi wa kurejeshwa tena   utaratibu wa kuwa  na vikao vya pamoja kati ya pande hizo mbili ambao ulilenga zaidi kuimarisha ujirani mwema.
Ombi hilo limetolewa na balozi wa Msumbiji nchini ZAKARIA KUPELLA katika  mazungumzo yake na makamu wa pili wa rais  visiwani Zanzibar, Balozi SEIF ALI IDDI.
KUPELA amesema Tanzania ilikuwa mstari wa mbele katika kusaidia ukombozi wa mataifa ya Afrika ikiwamo Msumbiji, hivyo ni vyema vikao vya ushirikiano vikafufuliwa kwa nia ya kulinda umoja na udugu wa sehemu hizi mbili.
Amesema yapo maeneo mengi ambayo wananchi wa pande hizo mbili wamekuwa wakishirikiana kwa pamoja hasa ikizingatiwa nchi hizo zimepakana.
Amesema itapendeza iwapo utaandaliwa utaratibu wa  kuyaunganisha makundi ya vijana wa pande hizo mbili na nchi zikafaidika  kwa pamoja katika kutumia rasilimali zilizomo.
Naye Balozi Seif  Iddi amesema uhusiano wa pande hizo mbili hivi sasa inafaa uelekezwe zaidi katika uchumi badala ya Siasa.

FEBRUARI, 23, 2012

KAHAMA
WAKRISTO nchini wametakiwa kujitoa kwa moyo kuwasaidia maskini na  wasiojiweza hasa katika kipindi  hiki cha kwa lezima.

Wito huo umetolewa na padri ROGATUS MALULU katika ibada ya  misa maalumu ya kipindi cha kwalezma iliyofanyika  katika kanisa kuu la katoliki jimbo la kahama mjini.

Amesema wakati wote wananchi   wanatakiwa kuacha mambo yasiyompendeza MUNGU, wawe na matendo  mema ikiwamo  kuwasaidia maskini na wasiojiweza na wanaoteseka kwa kukosa misaada

Pamoja na mambo mengine padri MALULU amewataka waumini wa dini ya kikristo  kutubia ipasavyo  makosa na kuombana  msamaha ili  kujenga  imani ya kweli yenye kumpendeza MWENYEZI MUNGU. 
SHINYANGA
WAZIRI mkuu MIZENGO PINDA  kesho  Ijumaa  anaanza ziara ya siku mbili wilayani kahama ikiwa ni sehemu ya ziara yake ya siku nane mkoani Shinyanga kukagua shughuli za maendeleo katika wilaya zote saba za mkoa huo.
Ziara yake hiyo iliyoanza Jumatatu wiki hii ilianzia  wilayani  Maswa, Bariadi, Meatu, Kishapu.
Akifika kahama atakweda wilayani  Bukombe, na kisha kurejea Kahama, na keshokutwa  atakwenda Shinyanga Vijijini na kumalizia Shinyanga Mjini.
Katika wilaya zote hizo, waziri mkuu atahutubia mikutano ya hadhara na kusalimiana na wananchi kwenye baadhi ya miradi atakayoikagua.
Wilayani  kahama ataweka jiwe la msingi katika  mradi wa umwagiliaji maji huko Chela, na kwenye karakana ya kilimo iliyoko Kahama mjini. wilayani Bukombe atakagua shamba la uzalishaji mbegu bora za mihogo katika gereza la Kanegele
Akiwa wilayani Meatu amekagua josho la mifugo la Mwamihanza, shamba darasa la pamba, na kukagua mradi wa umeme vijijini katika kijiji cha Mwandoya
Wilayani Kishapu amekagua shamba la mbegu bora la mtama katika kijiji cha Mwamashele.
Akiwa Shinyanga, waziri mkuu atafungua ghala la mazao la kijiji cha Lyabusalu na kukagua hospitali ya wilaya ya Shinyanga iliyoko ISELAMAGAZI.
Pia atakagua kiwanda cha nyama kilichopo Old Shinyanga na kuzindua Chuo cha VETA Shinyanga.
Jumatatu ijayo ya Februari 27, atafanya majumuisho ya ziara yake katika mkoa huo kwenye ukumbi wa mikutano wa NSSF na kurejea jijini Dar es Salaam mchana huo huo.

SHINYANGA
WAFANYABIASHARA  wa soko kuu la manispaa ya Shinyanga wamegoma kulipa ushuru wa soko na kutishia  kufanya maandamano kwenda kuonana na mkuu wa mkoa  huo.
Hatua hiyo ni  kupinga  kuamishwa kwa kituo cha magari madogo yanayosafirisha abiria kwenda katika miji ya Maganzo, Korandoto na Mhunze.
Mmoja wa wafanyabiashara katika soko hilo, ERICK GENZABUKE amesema baada ya mkuu wa mkoa wa Shinyanga, ALLY RUFUNGA kuagiza kuondolewa kwa magari madogo katika kituo cha mabasi cha zamani, biashara katika soko hilo imepungua na wafanyabiashara hasa wa matunda wameanza kupata hasara.
Amesema wamesikitishwa na kitendo cha uongozi wa mkoa kupingana na maamuzi ya awali yaliyokataza kuamishwa kwa kituo hicho.
GENZABUKE amesema  makubaliano yalikuwa ni  kuhamishwa kwa kituo cha mabasi cha stendi mpya kwenda eneo la soko la IBINZAMATA na si kuamishwa kwa kituo cha soko kuu.
Hivi karibuni mkuu huyo wa mkoa alitangaza uamuzi wa kuhamishwa kwa kituo cha magari madogo katika eneo hilo la soko kuu kwa sababu ya kupanua mji.
KIBAHA
WIZARA ya elimu na mafunzo ya ufundi stadi  imetakiwa kuendeleza vipaji vya uchoraji kwa watoto wa shule za msingi ili kuwawezesha ikiwamo  kujipatia ajira.

Wito huo umetolewa  wilayani Kibaha, mkoani Pwani na mratibu wa shirika lisilo la kiserikali la International Youth Development Programme (IYDP) FLORA KALINGA katika maonyesho ya michoro ya watoto yenye ujumbe wa miaka 50 ya Uhuru ambapo michoro 400 imeonyeshwa.

Amesema wizara ya elimu haina mpango mkakati wa namna ya kusaidia watoto wenye vipaji vya uchoraji nchini.

Hivyo amesema mpango mkakati wa IYDP ni kuendeleza vipaji hivyo  kwa lengo la kuwaandaa vijana kujiajiri.

Mkurugenzi wa maendeleo ya utamaduni wa wizara hiyo professa HERMAS MWANSOKO amepongeza jitihada za shirika  hilo la  kuibua vipaji vya uchoraji na kwamba nchi itaweza kupata  maendeleo ya haraka.

Mshindi wa kwanza wa  uchoraji kutoka shule ya msingi Ruvu JKT, JUMA MASANJA ameomba serikali kuweka somo la maalumu la uchoraji na kwamba kwa sasa wanajisomea na kujifunza wenyewe bila kuwapo kwa vipindi wala mwalimu

Amesema kuwapo kwa somo hilo kutaongeza ufanisi  wa fani hiyo.





FEBRUARI, 22, 2012
SHINYANGA
KIPATO kidogo cha wazazi ni mojawapo ya sababu ya wanafunzi kufeli masomo na kwamba hulazimika kujiingiza katika biashara ndogondogo ili kumudu mahitaji yao.
Sababu nyingine  ni wazazi kutofuatilia mienendo ya watoto ikiwamo kama  wamefika shuleni na kuandika au la.
Hayo yamesemwa mkoani Shinyanga  katika mdahalo wa kampeni ya kupunguza utoro wa wanafunzi wa shule za msingi ulioandaliwa na asasi isiyo ya serikali ya YHDA.
Imeelezwa wengi wa wanafunzi wanalazimika kuacha kusoma na kwenda  kufanya biashara ndogo ndogo  kwa kukosa chakula nyumbani.
JULIUS THOMAS amesema watoto wengi wamekuwa wakidanganya wanakwenda shule lakini hawafiki na wengine wanajificha vichakani
YHDA imesema baadhi ya wanafunzi waliohojiwa wamesema  wanashindwa kuingia darasani kwa kuwa wanafikiria  kurudi nyumbani kuuza matunda ili kupata fedha za kununulia chakula.
Pamoja na mambo mengine, wazazi na walezi wametakiwa kubadilika kwa kuacha kuwaangiza wanafunzi kufanya biashara.
Pia wametakiwa kutenga muda wa kufuatilia mienendo ya watoto ili kuwajenga  katika maadili na tabia njema.

ZANZIBAR
SERIKALI ya Oman imekubali kusaidia kutoa matibabu ya moyo kwa watoto kuanzia mwaka mmoja hadi miaka 16.
Waziri wa wizara ya Afya visiwani Zanzibar, JUMA DUNI HAJI amesema kila mtoto  atagharamiwa kwa dola za kimarekani kati ya ELFU 4 na ELFU 5.
Amesema huduma za matibabu hayo zinatarajiwa kuanza mwanzoni mwa mwezi ujao ambapo kwa kuanzia watapelekwa watoto 10 hadi 20.
Waziri DUNI amesema matibabu hayo yatakuwa yakifanyika nchini India katika Hospitali ya Nara.
Amesema kwa sasa wataalamu kutoka India wapo Kisiwani Pemba wakiendelea na uchunguzi ambapo tayari watoto 73 wamegundulikana kuwa na matatizo hayo kwa Unguja pekee.
Waziri huyo amesema mpango huo ni wa kudumu na kwamba idadi ya wagonjwa itaongezeka maradufu.

MWANZA
MKUU  wa mkoa wa Mwanza mhandisi EVARIST NDIKILO amewataka watendaji wa kata na vijiji wanaoshindwa kutoa taarifa ya  mapato na matumizi ya michango ya miradi mbalimbali ya maendeleo, kujiuzulu nafasi hizo kabla hawajafukuzwa na kuchukuliwa hatua za kisheria.
Ametoa agizo hilo jana katika mkutano wa hadhara uliofanyika katika kijiji cha Nyehunge wilayani SENGEREMA ambapo pamoja na mambo mengine ametembelea miradi mbalimbali ya maendeleo.
Amesema watendaji hao wamekuwa na bidii kubwa kuwachangisha wananchi michango mbalimbali lakini mapato na matumizi  haifahamiki.
Kufuatia agizo hilo amewataka maofisa tarafa kusimamia suala hilo kwa  kuhakikisha kila baada ya miezi mitatu wananchi wanawasomea taarifa ya mapato na matumizi.
Hata hivyo amewaonya maofisa tarafa kuwa wakipuuzia agizo lake hilo  hatua za kinidhamu ikiwamo kusimamishwa kazi zitachukuliwa.
Katika hatua nyingine amemtaka mhandisi wa ujenzi wilayani Sengerema MOHAMED KABELWA kuacha ubabaishaji katika kazi zake kutokana na miradi iliyochini yake kujengwa chini ya kiwango na kulalamikiwa na wananchi.
 Amesema hata taarifa ya mkaguzi na mdhibiti mkuu wa hesabu za serikali (CAG), imebaini miradi mingi ya ujenzi imejengwa  chini ya kiwango
Pamoja na mambo mengine amesema wilaya nyingi mkoani Mwanza zinatuhumiwa kujihusisha na ubadhirifu mkubwa na ndio maana zimepata hati za masahaka kutoka  kwa CAG.
MBEYA
WAZAZI na walezi wametakiwa kutowafungia ndani watoto wenye ulemavu na wawapatie huduma muhimu ikiwamo ya kwenda shule ili waweze kujitegemea hapo baadae. 
Wito huo umetolewa  na mwenyekiti wa asasi isiyo ya kiserikali inayoshughulikia vitendo vya ukatili na unyanyasaji wa wanawake na watoto mkoani Mbeya, IMANUEL SIMONI.
Amesema watoto wenye ulemavu wamekuwa wakinyimwa haki zao za msingi hali inayowapelekea kudumaa kifikra, kiafya na kielimu na hatma yao kuwa  ni ombaomba.
SIMON amesema tabia hiyo si nzuri na ni ubaguzi na kwamba watoto wote wana haki sawa.
Kuhusu utupaji wa watoto, amesema  moja ya sababu  ni  wanaume kukataa mimba, kutelekeza wake zao na ugumu wa maisha ambao umekuwa ukiwakabili baadhi ya wanawake  kutokana na sababu mbalimbali.
Hata hivyo amewataka wanawake wanaopata ujauzito  wasiutoe wala kutupa watoto na wawe wavumilivu  kwa kuwa kwa namna moja ama nyingine watoto watakuja kuwasaidia.



FEBRUARI, 21, 2012
SHINYANGA
WAZIRI mkuu MIZENGO PINDA  Ijumaa wiki  hii  anaanza ziara ya siku mbili wilayani kahama ikiwa ni sehemu ya ziara yake ya siku nane mkoani Shinyanga kukagua shughuli za maendeleo katika wilaya zote saba za mkoa huo.
Ziara yake hiyo iliyoanza Jumatatu wiki hii ilianzia  wilayani  Maswa, Bariadi, Meatu, Kishapu. Akifika kahama atakweda wilayani  Bukombe, na kisha kurejea Kahama, na keshokutwa  atakwenda Shinyanga Vijijini na kumalizia Shinyanga Mjini.
Katika wilaya zote hizo, waziri mkuu atahutubia mikutano ya hadhara na kusalimiana na wananchi kwenye baadhi ya miradi atakayoikagua.
Wilayani  kahama ataweka jiwe la msingi katika  mradi wa umwagiliaji maji huko Chela, na kwenye karakana ya kilimo iliyoko Kahama mjini. wilayani Bukombe atakagua shamba la uzalishaji mbegu bora za mihogo katika gereza la Kanegele
Akiwa wilayani Meatu amekagua josho la mifugo la Mwamihanza, shamba darasa la pamba, na kukagua mradi wa umeme vijijini katika kijiji cha Mwandoya
Wilayani Kishapu amekagua shamba la mbegu bora la mtama katika kijiji cha Mwamashele.
Akiwa Shinyanga, waziri mkuu atafungua ghala la mazao la kijiji cha Lyabusalu na kukagua hospitali ya wilaya ya Shinyanga iliyoko ISELAMAGAZI.
Pia atakagua kiwanda cha nyama kilichopo Old Shinyanga na kuzindua Chuo cha VETA Shinyanga.
Jumatatu ijayo ya Februari 27, atafanya majumuisho ya ziara yake katika mkoa huo kwenye ukumbi wa mikutano wa NSSF na kurejea jijini Dar es Salaam mchana huo huo.
 CHUNYA
NAIBU waziri wa elimu na mafunzo ya ufundi stadi, PHILIPO MULUGO na wananchi wa  kijiji cha mwajuni wilayani chunya mkoani mbeya  wamewakataa wajumbe watatu wa halmashauri ya kijiji hicho akiwamo afisa mtendaji wa kijiji SADICK KAHULULU (44).
Wamewakataa   kwa tuhuma za matumizi mabaya  ya fedha za michango ya maendeleo na wanachangia kukwamisha shughuli za maendeleo.
Kwa pamoja  wamemtaka mkurugenzi wa halmashauri hiyo  MAURICE SAPANJO  kumuondoa haraka kabla ya athari mbaya hazijatokea.
Uamuzi huo ilifikiwa jana jioni katika mkutano wa hadhara uliofanyika katika kijiji hicho. Waziri MULUGO pia ni mbunge wa jimbo  hilo.
Wamesema wamechoshwa na watendaji hao kwa kuwa wananchi wanachangia michango mbalimbali ya maendeleo lakini wanakatishwa tamaa na watendaji hao  kwa kutotoa mapato na matumizi ya michango hiyo.
Kufuatia hali hiyo Waziri MULUGO  ameiagiza halmashauri  hiyo kuunda tume maalum, itakayosimamia  michango ya wananchi.
Amesema atahakikisha watuhumiwa hao wanafikishwa mahakamani na haki inatendeka.
Hivyo ameziagiza halmashauri zote nchini kuunda tume maalumu zitakazokuwa zikisimamia na kufuatilia mwenendo mzima wa michango ya wananchi na kuhakikisha wanapewa taarifa sahihi za mapato na matumizi.
Februari 19 watuhumiwa hao walishikiliwa na jeshi la polisi kwa tuhuma za ubadhilifu wa milioni 10 zilizotolewa na wananchi na  leo wanafikishwa mahakamani.
 MOROGORO
WAFUGAJI wilayani Ulanga, mkoani Morogoro, wameanza kupunguza idadi ya mifugo na kubaki na michache ili  kufuga kisasa.
Hatua hiyo ni kuitikia wito wa serikali na wameanza kuiuza huku fedha wanazopata wanazitumia kuwekeza katika vitega uchumi mbalimbali ikiwamo ujenzi wa nyumba za biashara  na ununuzi wa matrekta kwa ajili ya shughuli za kilimo.
Pia  wameamua kuandaa bajeti maalum ili waweze kwenda nchini Botswana kujifunza mbinu za ufugaji wa kisasa na wenye tija.
Mwenyekiti wa chama cha kuweka na kukopa cha wakulima na wafugaji Ulanga (IFALIA SACCOS) MICHAEL PAWA, na kwamba wafugaji  wameamua kubadilika baada ya kupewa elimu ya mabadiliko kutoka kwa daktari wa mifugo wa wilaya ya Ulanga Dk Fredrick Sagamiko.
Pia hatua hiyo imechangiwa kwa kiasi kikubwa agizo la waziri mkuu Mizengo Pinda kuwa wafugaji wote waliovamia bonde oevu la Kilombero ifikapo  mwezi Agosti mwaka huu lazima watoke eneo hilo .

Kupitia chama chao wafugaji hao wanatarajia kukusanya milioni 10 kwa ajili ya kwenda Botswana na mwezi Machi  wafugaji wanne ndio watakaoanza kwenda nchini humo.
Mkuu wa mkoa wa Morogoro JOEL BENDERA amewataka wafugaji nchini kote kuiga mfano huo.
Amesema kulingana na dunia ya sasa ni lazima wananchi wabadilike ili kwenda na karne ya sayansi na teknolojia na ni lazima  wafugaji  wafuge kisasa.
Pamoja namambo mengine amewataka wafugaji kuhakikisha wanawapeleka shuleni watoto wao.
ZANZIBAR
SERIKALI imetakiwa kuongeza kasi ya ujenzi wa nyumba za walimu vijijini ili kuwaondolea tatizo la makazi
Wito huo umetolewa na katibu mkuu wa chama cha  walimu Zanzibar (ZATU) MUSSA OMAR  katika  kongamano la kutimiza miaka 10 ya chama hicho.
Amesema ukosefu wa nyumba za walimu unachangia kwa kiasi kikubwa kudumaza maendeleo ya elimu ikiwamo muda wa kufundisha kupungua.
Akizungumza katika kongamano hilo makamu wa pili wa rais  visiwani Zanzibar BALOZI SEIF ALI IDDI amesema pamoja na mambo mengine serikali itaendelea kuboresha maslahi  ya walimu, kwa kadri mapato yatakavyoruhusu.
Hata hivyo amesema vyama  vya wafanyakazi vinatakiwa kupata haki na fursa zote zinazostahiki na kuruhusiwa kufanya kazi zake kikamilifu, bila ya bugudha, ili kuendeleza maendeleo ya wanachama wao.
Kuhusu wanafunzi wa kidato cha nne kufutiwa matokea yao, Balozi Seif amesema  hatua hiyo ni changamoto kwa walimu ili kuwa makini  katika ufundishaji na usimamizi wa mitihani.
Amesema fahari ya mwalimu ni wanafunzi kufanya vizuri masomo, kinyume na hapo ni fedhea.
Pamoja na mambo mengine amesema kamati iliyoundwa kuchunguza tatizo la  hilo ndio itakayotoa mwelekeo wa utatuzi wa suala hilo.


FEBRUARI,20, 2012
SHINYANGA
WAZIRI mkuu MIZENGO PINDA   leo  Jumatatu, ameanza ziara ya siku nane mkoani Shinyanga kukagua shughuli za maendeleo katika wilaya zote saba za mkoa huo.
Ziara yake hiyo imeanzia wilayani  Maswa, na itaendelea katika wilaya ya Bariadi, Meatu, Kishapu, Bukombe, Kahama, Shinyanga Vijijini na kumalizia Shinyanga Mjini.
Katika wilaya zote hizo, waziri mkuu atahutubia mikutano ya hadhara na kusalimiana na wananchi kwenye baadhi ya miradi atakayoikagua.
Miongoni mwa shughuli atakazozifanya ni kukagua josho la mifugo la Mwamihanza, shamba darasa la pamba, na kukagua mradi wa umeme vijijini katika kijiji cha Mwandoya wilayani Meatu.
Pia , atakagua shamba la mbegu bora la mtama katika kijiji cha Mwamashele, wilayani Kishapu na shamba la uzalishaji mbegu bora za mihogo katika gereza la Kanegele wilayani Bukombe.
Wilayani  kahama ataweka jiwe la msingi katika  mradi wa umwagiliaji maji huko Chela, na kwenye karakana ya kilimo iliyoko Kahama mjini.
Akiwa Shinyanga, waziri mkuu atafungua ghala la mazao la kijiji cha Lyabusalu na kukagua hospitali ya wilaya ya Shinyanga iliyoko ISELAMAGAZI.
Pia atakagua kiwanda cha nyama kilichopo Old Shinyanga na kuzindua Chuo cha VETA Shinyanga.
Jumatatu ijayo  ya Februari 27, atafanya majumuisho ya ziara yake katika mkoa huo kwenye ukumbi wa mikutano wa NSSF na kurejea jijini Dar es Salaam mchana huo huo.

DODOMA
WAKAZI wa vijijini wametakiwa kujitoa muhanga katika kufuatilia miradi mbalimbali inayosimamiwa na viongozi wao ili kuepusha  tatizo la ‘uchakachuaji’.
Wito huo umetolewa na mwenyekiti wa taasisi isiyo ya kiserikali ya Better Life,  ASIA SULEIMAN.
Amesema kitendo cha watu kuogopa na wakati mwingine kukata tamaa katika kufuatilia miradi ya maendeleo  ndio chanzo kikuu cha ufujaji wa fedha za umma.
Hata hivyo amesema wakazi wengi wa vijijini  hawajui bajeti na hata wakijua ni vigumu kufuatilia kwa kuwa hawajui  mahali pa kufuatilia.
Amesema suala hilo linaendelea kuota mizizi na kwamba  wanaoendelea kutafuna fedha za umma ni wenye mishahara ya uhakika ambao wamekabidhiwa dhamana ya kusimamia mali za watanzania.
Pia amewataka wananchi kuwa makini  na vishawishi na vitisho kutoka kwa watendaji  na watumishi wa serikali.
Amesema wengi wa watendaji hutoa vitisho na vishawishi kwa watu wanaofuatilia mwenendo wa miradi ya maendeleo, wakiamini wanawakosesha ulaji.
Pamoja na mambo mengine amewataka wananchi kujifunza  misingi ya uandaaji wa bajeti, ufuatiliaji, pamoja na usimamizi katika matumizi hadi mwisho wa mradi husika na kutolea taarifa.

IRINGA
NAIBU waziri wa TAMISEMI AGRREY MWANRI amemuagiza mhandisi wa ujenzi wa Halmashauri ya wilaya ya Kilolo mkoani Iringa,  ATU MWAIPYANA kuwasilisha vyeti vyake vya elimu kuanzia elimu ya sekondari  hadi chuo alichosomea taaluma hiyo kabla ya kuwajibishwa kwa kuisababishia hasara kubwa halmashauri hiyo katika miradi ya ujenzi.

Pia amekosoa utendaji mbovu wa wahandisi wa ujenzi katika Halmashauri ya Manispaa ya Iringa, Iringa vijijini, Ludewa, Njombe, Kilolo na Makete.
Amesema pamoja na kukutana na wahandisi wenye mapungufu katika halmashauri mbalimbali  lakini  si kwa mhandisi wa wilaya ya Kilolo na kwamba ameonyesha kutofahamu vema wajibu wa kazi yake.
Katika maujumuisho ya ziara yake, MWANRI amesema majibu aliyoyapata kutoka kwa mhandisi huyo wakati akihoji usimamiaji mbaya wa miradi ya ujenzi ndio yaliyomfanya kuingia wasiwasi na elimu  yake .
Pia amemtaka mhandisi  wa ujenzi wa wilaya ya LUDEWA kuwajibika kufuatia nyumba tatu kati ya kumi zilizojengwa kwa ajili ya watumishi wa umma, kujengwa chini ya kiwango.Wengine waliotakiwa kuwajibika kwa uzembe ni mhandisi wa wilaya ya Makete na Njombe

Katika hatua nyingine, amewaagiza wakurugenzi wa Halmashauri zote za wilaya isipokuwa ya  Mufindi kutolea majibu kwa mapungufu yaliyokutwa katika miradi ya ujenzi katika maeneo yao.

FEBRUARI 19, 2012
BUKOMBE
WATU wasiojulikana wamebomoa na kuiba katika nyumba ya kulala wageni mjini Ushirombo baada ya kumpa madawa ya kulevya mlizi.
Mmiliki kwa nyumba hiyo SOSPETER KADAMA ameiambia REDIO KAHAMA FM kuwa wezi hao walipanga katika nyumba hiyo na walijiandikisha kwa majina ya ABDU MASANJA  na  FURAHA HANSI wote wakazi wa jijini Mwanza.
Amesema ilipofika usiku walimpa mlizi ndizi mbili zilizokuwa zimewekwa madawa ya kulevya na baada ya kuzila alisinzia  fofofo.
Ndipo walipofanikiwa kuchimba na kuingia ndani ya chumba cha duka la madawa kilichopo katika  nyumba hiyo na kuiba mali ambazo hadi sasa thamani yake haijafahamika.
Mlinzi huyo amepelekwa hospitali na jeshi la polisi limechukua mabaki ya ndizi  zenye madawa hayo kwa ajili ya kufanyia uchunguzi.
Kufuatia tukio hilo, kaimu mkuu wa wilaya ya Bukombe, BAHATI MATALA amewataka wamiliki kuajili walinzi waliopitia jeshi la mgambo ua wastaafu wa jeshi.
Amesema wengi wao wanambinu za kumtambua jambazi.
Pamoja na mambo mengine amewataka wananchi kushirikiana na vyombo vya dora ili kuwatia mbaroni watuhumiwa hao.
MOSHI
WAHITIMU wa fani mbalimbali nchini, wametakiwa kutambua ugumu wa upatikanaji wa ajira, na kwamba wawe na mikakati mbadala wa kumudu ushindani wa soko la ajira.
Wito huo umetolewa mkuu wa mkoa wa Kilimanjaro, LEONIDUS GAMA,  katika mahafali ya kidato cha sita katika shule ya sekondari  Bendela, mjini Moshi
Amesema licha ya serikali kuwa na jukumu la kutengeneza ajira mbalimbali lakini juhudi binafsi zinahijika katika kujipatia ajira hasa za kujiajiri.
Mkuu huyo wa mkoa amesema kulingana  na ongezeko kubwa la  wahitimu wa vyuo vikuu ndio maana ajira zinakuwa ngumu.
Pia amesema hali hiyo imesababishwa na  dhana ya  wengi wa wanaohitimu fani mbalimbali  kutegemea kuajiriwa.
Kutokana na changamoto hizo amewataka wasomi kubuni njia mbadala ya kujipatia ajira kwa kutumia fani walizozisomea.
Naye ,kuu wa shule hiyo Fatha Meles Mlingi, amesema pamoja na mafanikio  ya kitaaluma tangu ilipozinduliwa na rais Jakaya Kikwete mwaka 2004, inakabiliwa na changamoto ya upanuzi wa miundombinu ili kukidhi mahitaji ya wanafunzi wanaotaka kusoma shuleni hapo.
Katika hatua nyingine mkuu huyo wa mkoa amepongeza hatua zinazoendelea kuchukuliwa na wadau wa sekta ya elimu mkoani humo, zenye lengo la kuhakikisha kiwango cha elimu kinaongezeka.
NJOMBE
MAWAKALA wa usambazaji wa pembejeo  wamesema   chanzo cha kusuasua kwa zoezi la ugawaji wa vocha za pembejeo za ruzuku katika maeneo mbalimbali  nchini ni kutoka na serikali kutowalipa  malipo ya msimu uliopita.
Kufuatia tatizo hilo wameitaka serikali  kupitia wizara ya kilimo, chakula na ushirika  iharakishe kulipa fedha hizo ili wakulima wapate pembejeo katika muda muafaka.
Hayo yamesemwa na viongozi  wa chama cha mawakala wa pembejeo wilayani Njombe, mkoani Iringa  na kwamba ndio maana awamu ya nne ya mfumo wa vocha za ruzuku haukufanikiwa ikilinganishwa na awamu ya tatu.
Mwenyekiti  wa chama hicho, ANDREA SANGA amesema katika misimu iliyopita hakukuwa na tatizo la upatikanaji wa pembejeo kutokana na serikali kuwahisha malipo ya mawakala.
Naye muhasibu wa chama hicho, SERGIUS MLOWE amesema mawakala wapo katika hali ngumu ya kifedha kufuatia  taasisi nyingi za kifedha kukataa kuwakopesha fedha baada ya kufahamu serikali haijatoa fedha kwa mawakala hao.

FEBRUARI 18, 2012
DAR ES SALAAM
NAIBU wa Waziri wa Ujenzi, Dk Harrison Mwakyembea amelijibu jeshi la polisi kuwa anachougua, kimesababishwa na kunyweshwa sumu.
Hatua yake hiyo inafuatia  tamko lililotolewa jana na mkurugenzi wa makosa ya jinai DCI Robert Manumba  kuwa Dk Mwakyembe hakunyweshwa sumu na kuwa unaumwa ugonjwa wa ngozi  bila ya kufafanua, ulisababishwa na  nini.
Katika taarifa yake aliyoitoa kwa vyombo vya habari hii leo, Dk Mwakyembe ameendelea kusisitiza kuwa kuna kundi  linalijihusisha na mauaji lilikuwa limeelekezwa kumuua kwa kutumia sumu.
Amesema pamoja na kutoa taarifa hiyo  katika jeshi la Polisi lakini  ni karibu mwaka mzima polisi hawakutaka kuifuatilia kwa sababu wanazozijua wenyewe.
Amesema hadi sasa hajwahi kuhojiwa na jeshi la Polisi kutaka kujua kama alipewa sumu au la kwamba  wamekurupuka  kutoa tamko hata kabla ya kumchunguza alivyo.
Pia amesema si kweli kama jeshi la polisi  limeongea na hata kuwahoji  madaktari bingwa wa Kihindi wanaonifanyia uchunguzi,  katika hospitali ya Apolo.
Amesema hadi sasa madaktari hao bingwa wanatafuta kitu kwenye mifupa yake ambayo wanaangaika kukijua, kukidhibiti na kukiondoa ambacho ndicho kinachomletea madaha
Aidha napata taabu kuamini kama DCI Manumba na wenzake waliisoma taarifa halisi ya matatibabu yangu au walisoma taarifa “nyingine”, na kama waliisoma taarifa hiyo wenyewe au “walisomewa”! Nasema hivyo kwa kuwa alichokisema DCI Manumba kwa wandishi wa habari hakifanani kabisa na picha iliyo kwenye taarifa halisi ya Apollo ambayo inatamka wazi kuwa kuna kitu kwenye mifupa yangu
KISHAPU
MADIWANI wa  halmashauri ya wilaya ya Kishapu mkoani Shinyanga wamepanga kukutana na waziri mkuu, MIZENGO PINDA atakapokuwa  ziarani mkoani humo ili kumweleza matatizo yanayochangia ubadhirifu mkubwa wa fedha katika halmashauri hiyo.
Pia wametaka wananchi nao wapeswe nafasi kueleza wanachokijua kuhusu halmashauri hiyo.
Madiwani hao wamesema kwa kipindi kirefu  halmashauri ya kishapu imekuwa ikikabiliwa na tatizo la ubadhirifu wa fedha za umma na hivyo ni wakati muafaka kila kitu kikawekwa wazi kwa waziri mkuu.
Wamesema  hatua yao hiyo ni kufuatia ratiba  ya ziara ya waziri mkuu, kutowapa nafasi ya kukutana naye ana kwa ana na kwamba hiyo imepangwa makusudi ili asijue ukweli wa  yanayoendelea katika halmashauri hiyo. 
Wamesema katika kuficha ukweli wa mambo mkurugenzi mtendaji wa halmashauri hiyo THEONAS NYAMUHANGA amewaandikia barua yenye kumb. Na. KDC/M.20/1/6 ya Februari 15, mwaka huu ikiwataka kwenda katika kikao cha majumuisho kitakachofanyika mjini Shinyanga badala ya kukutana naye kwanza wilayani Kishapu.

Diwani wa kata ya Mondo, JOHN NDAMA amesema kutokana na kitendo hicho, wanaendelea na msimamo wao wa kumkataa mkurugenzi mtendaji huyo na kwamba ameshindwa kusimamia shughuli za maendeleo.
Hivi karibuni waziri mkuu anatarajia kuwa na ziara ya kikazi mkoani Shinyanga na katika wilaya ya kishapu, atafungua jengo jipya la halmashauri hiyo.

CHAMWINO
WALEMAVU nchini wemetakiwa kujenga tabia ya ujasiri katika kuhoji na kutetea haki zao na si kukaa kimya  wakisubiri kuhurumiwa.
Pia halmashauri za wilaya, miji na manispaa zimetakiwa kutenga katika bajeti zao mafungu ya kutosha kwa ajili ya vitendea kazi kwa ulemavu na kuwapa nafasi ya kujiendeleza.
Wito huo umetolewa na afisa elimu wilayani  Chamwino mkoani Dodoma, SCOLASTIKA KAPINGA alipokuwa akifungua semina kuhusu sheria namba 9 ya mwaka 2010 kwa walimu wenye ulemavu.
Amesema kitendo cha baadhi ya walemavu kuzijua sheria za kazi pamoja na mahitaji yao lakini wananyamaza bila ya kupasa sauti zao, ni sawa na taa iliyowashwa na ikafunikwa.
Bi KAPINGA amesema wakati umefika  kwa kila kundi kujitetea na kujisimamia katika kutafuta haki.
Amesema walemavu ni miongoni kwa makundi ambayo yamebahatika kuwa na watu wenye uelewa mpana kuliko makundi mengine hivyo hawana sababu yakuogopa kudai haki zao za msingi.

Mratibu wa semina hiyo OMARY LUBUVA amesema pamoja na mambo mengine  walemavu wanakabiliwa na changamoto nyingi ikiwamo ukosefu wa miundombinu maalumu kwa ajili yao
MBEYA
WATU wawili  wilayani Kyela mkoani Mbeya  wamenusurika kufa baada ya kuchomwa moto na wananchi wakituhumiwa kuiba mabomba katika josho la kuogeshea ng’ombe.

Pamoja na kujeruhiwa  vibaya na moto lakini walinusurika  baada ya kuokolewa na wasamalia wema kabla ya jeshi la polisi kufika na kuwapeleka  hospitali kwa matibabu.

Kamanda wa polisi mkoani humo,  ADVOCATE NYOMBI amesema tukio hilo lilitokea katika kijiji cha Sinyanga wilayani Kyela  na kwamba watuhumiwa hao waliiba mabomba 27 yenye thamani ya  milioni 4, Laki 3 na Elfu 20, mali ya kijiji hicho.

Amewataja watuhumiwa hao kuwa ni KASTO MWAIJEGA (40) mkazi wa kijiji cha Shinyanga ambaye ni mfanyabiashara  na ZAILE MWANGONDA (30) mkulima na mkazi wa kijiji cha Ipande wilayani humo.

Amesema watuhumiwa walikamatwa wakiwa na pikipiki aina ya T-BETTER yenye namba za usajili T981TDP,  waliyotaka kuitumia kubebea mabomba hayo.


Kamanda  NYOMBI amesema baada ya kuzingirwa na wananchi watuhumiwa hao walikiri kutaka kuiba mabomba hayo  na ndipo waliposhambuliwa na  kuchomwa moto  kabla ya kuokolewa.

Watuhumiwa hao wamelazwa katika hospitali ya rufaa ya Mbeya na watafikishwa  mahakamani upelelezi ukikamilika.

ZANZIBAR
SERIKALI ya  Zanzibar imesema haitapiga marufuku uingizaji wa vitu vilivyotumika 'Used' na kwamba  inadaa mpango madhubuti wa usimamizi na uhakiki wa uingiaji wa vitu hivyo  kama  vina viwango bora na vinafaida kwa watumiaji.
Msimamo huo umetangazwa na waziri wa nchi, ofisi ya makamu wa kwanza wa rais, FATMA ABDULAHABIB FEREJI  alipokuwa akizungumzia, changamoto, mipango  na mafanikio ya  wizara hiyo.
Amesema serikali inafahamu  vitu vilivyotumika vinanunuliwa sana na wananchi wenye hali ya chini kiuchumi  kwa kuwa hawana uwezo wa kununua vitu vipya.
Hivyo serikali imelenga kuangalia njia mbadala ya upatikanaji wa vitu hivyo katika  ubora na si kuwakomoa wananchi.
Vitu vingi vinavyoingizwa nchi ambavyo vimetumika kutoka nchi za nje ni vifaa vya electronic ikiwamo TV, friji na makuka pamoja na nguo za mitumba.


FEBRUARI 17, 2012
SHINYANGA
MKAZI wa kijiji cha Bunonga, mkoani Shinyanga NDALO DOKEZO (28) ameuwawa kwa kupigwa mawe na kisha mwili wake kuchomwa moto baada ya kutuhumiwa kuiba debe moja la mahindi.
Kamanda wa polisi  mkoani  Shinyanga, DIWANI ATHUMANI amesema tukio hilo limetokea jana  majira ya saa moja asubuhi katika kijiji cha Bugogo wilayani Shinyanga.
Amesema DOKEZO aliuwawa baada ya kutuhumiwa kuiba mahindi mabichi kiasi cha debe moja hata hivyo mmiliki wa mahindi hayo  hajafahamika.

Jeshi la polisi linawasaka watu waliohusika na mauaji hayo Kamanda ATHUMANI amewataka wananchi kuacha tabia ya kujichukulia sheria mkononi.

Katika tukio lingine polisi inawashikilia wakazi wawili wa kata ya Kitangiri manispaa ya Shinyanga wakituhumiwa kwa kosa la kupatikana na mtambo wa kutengenezea pombe haramu ya gongo.

Kamanda Athumani amewataja watuhumiwa hao kuwa ni MARGARETH NYANGIDO (50) na HELLENA TENGE (50) watuhumiwa hao wanatarajiwa kufikishwa mahakamani.

MBINGA
MAKAMU wa rais Dk MOHAMED GHALIB BILAL amesema serikali inafanya jitihada za kipekee kuhakikisha madini ya makaa ya mawe yanachimbwa na kuzalisha ili kuondoa  tatizo la umeme nchini.
Amesema hayo  alipotembelea mradi wa makaa ya mawe wa ngaka, wilayani Mbinga mkoani Ruvuma na kwamba umeme wa uhakika utainufaisha nchi zaidi.
Dk BILAL amesema kutokana na wingi wa makaa hayo, umeme unaweza kuzalishwa kwa zaidi ya miaka mia mbili.
Awali akitoa taarifa ya mradi huo mkurugenzi wa shirika la maendeleo la taifa (NDC) GIDEON NASALI amesema  upatikanaji wa  leseni kwa kampuni ya TANCOAL  ili kutekeleza mpango wa kuzalisha megawati 400 za umeme, umekuwa mgumu.
Kwa sasa makaa ya mawe yanayozalishwa katika mgodi wa Ngaka yanatumika na viwanda vya saruji vya Mbeya na Tanga na pia madini husika yanauzwa nchini Malawi.
Katika mradi huo serikali kupitia NDC inamiliki asilimia 30 na kampuni ya Intra Energy ya Singapole ina hisa asilimia 70.
MBEYA
WATU wawili wamefariki dunia katika matukio mawili tofauti mkoani Mbeya likiwamo la mwanaume mmoja kunyongwa shingo hadi kufa na mwili wake kutupwa mtoni.
Kamanda wa polisi mkoani Mbeya,  ADVOCATE NYOMBI amesema tukio la  kunyongwa kwa ZUBERI MWANJELEBA (20) limetokea katika kijiji cha Ibumba-Ibungu  wilayani Rungwe.
Amesema aliuwawa majira ya saa mbili usiku  jana na mwili wake ulikutwa unaelea katika mto Kang’eng’ele.
 Katika tukio lingine, binti asiyefahamika  jina  amekufa baada ya kugongwa na pikipiki katika maeneo ya Ilomba  barabara ya Mbeya- Iringa.
Kamanda Nyombi  amesema binti huyo  anayekadiriwa kuwa na umri kati ya miaka 10 hadi 18 aligongwa na kufa papo hapo, majira ya saa kumi na mbili jioni na kwamba baada ya ajali mwendesha pikipiki  alikimbia.
Mwili wa marehemu umehifadhiwa katika hospitali ya rufaa ya Mbeya.
Kamanda huyo amesema upelelezi wa matukio yote mawili yanaendelea na kwamba hakuna mtu yeyote aliyekamatwa kuhusiana na matukio hayo.
ZANZIBAR
WANANCHI kutokuwa na tabia ya kuchukua risiti baada ya kununua bidhaa linaikosesha  serikali mapato mengi.
Pia  baadhi ya wafanyabiashara wanafanya udanganyifu kwa kuwa na  vitabu viwili tofauti vya risiti.
Hayo yamesemwa na waziri wa nchi ofisi ya rais, fedha na mipango ya maendeleo visiwani Zanzibar, OMAR YUSSUF MZEE.
Kutokana na hali hiyo ameitaka mamlaka ya mapato (TRA) na  ile ya Zanzibar (ZRB), kutoa elimu ya kutosha kwa wananchi ili kufahamu umuhimu wa kudai risiti watakaponunua bidhaa.
Hata hivyo amesema mamlaka hizo zimeonesha mwamko mzuri katika ukusanyaji wa kodi  kwa kipindi cha miezi sita kuanzia June 2011 hadi Januari 2012.
Amesema katika kipindi hicho ZRB imekusanya bilioni 53.4 kati ya bilioni 55.3 walizopangiwa kukusanya na kila mwezi wanakusanya takriban  bilioni 10 badala ya bilioni nane.
Katika kipindi hicho TRA imekusanya bilioni 41.9 kati ya bilioni 59.4 walizopangiwa kukusanya huku kwa mwezi inakusanya takribani bilioni nane kutoka bilioni sita.
Amesema TRA imekuwa na upungufu mkubwa katika ukusanyaji mapato  kutokana na kuwa bado hawajaingia katika ukataji wa kodi kwa wafanyakazi wa muungano.
Kuhusu mfumuko wa bei amesema umepanda kwa kiasi kikubwa na kufikia asilimia 14.7 kutoka asilimia 6.1, sababu ikiwa ni ongezeko la thamani ya dola, kupanda kwa mafuta, na kushuka kwa uzalishaji wa chakula hasa mchele.
Katika kukabiliana na hali hiyo amesema serikali imeweka kipaumbele cha kuimarisha kilimo  hasa cha umwagiliaji maji ili kuondokana na utegemezi wa kuagiza chakula kutoka nje.

FEBRUARI, 16, 2012
KAHAMA
MBUNGE wa jimbo la Kahama JAMES LEMBELI amewapongeza wananchi wa kijiji cha BULIMA kata ya mpunze wilayani  humo kwa kuanzisha mfuko maalum  wa kuwasaidia watoto yatima na wanaoishi katika mazingira magumu.


Ametoa pongezi hizi alipokuwa akikabidhi sare za shule kwa watoto 24 ambao ni yatima na wasio na uwezo.

Akizungumza na mamia ya wananchi wa kijiji hicho, amesema kuwalea watoto yatima na wanaoishi kwenye mazingira magumu si la serikali pekee na kwamba uamuzi wa wananchi wa Bulima kuunda kamati ya kufuatilia maisha ya watoto hao ni mfano wa kuigwa.

Pamoja na mambo mengine amewataka wananchi kuendelea na moyo wa kuwachangia wenzao  ambao hawana uwezo.


Awali afisa mtendaji wa kijiji hicho alisema, kijiji  hicho kina kinakabiliwa na changamoto nyingi ikiwamo  ukosefu wa zahanati na  madarasa  katika shule ya msingi.

Kufuatia matatizo hayo, mbunge LEMBELI amechangia jumla ya milioni 6, zitakazotumika  katika maendeleo ya kijiji hicho.

Amesema milioni 2 zitatumika kwa ajijli ya ujenzi wa zahanati, milioni 2 kwa ajili ya kuezeka madarasa mawili ya shule ya msingi na laki 5 kwa ajili ya kuwalipia ada wanafunzi 4 ambao ni  watoto yatima.


Pia ameahidi kununua sola pawa kwa ajili ya shule ya sekondari ya kata ya Mpunze yenye thamani ya shilingi  milioni 1 na NUSU.
SHINYANGA
KATIBU mkuu wa wizara ya maji, mhandisi  CHRISTOPHER SAYI amesema utekelezwaji wa awamu ya pili ya mradi wa utunzaji ziwa  victoria utagharimu dola za kimarekani milioni 35 kwa kipindi cha miaka minne.
Ameyasema hayo katika ziara yake mkoani Shinyanga na  kwamba mradi huo unatekelezwa kwa  ushirikiano wa Tanzania na nchi za jumuiya ya Afrika Mashariki.

Mradi huo unaoendeshwa na nchi tano wanachama wa Jumuiya ya Afrika ya Mashariki unatarajia kuijengea uwezo jamii, taasisi za kiserikali na zisizo za kiserikali kulinda na kusimamia rasilimali za majini na nchi kavu. 
Mradi huo ulioanza Septemba mosi, mwaka  2009 umelenga kuishirikisha jamii katika kusimamia rasilimali za majini na nchi kavu na  kuzifanya kuwa  endelevu kwa vizazi vya sasa na vijavyo.
Lengo lingine ni kupunguza matatizo na kasi ya uharibifu wa mazingira katika bonde la ziwa victoria na kuongeza utunzaji wa bonde na mito inayotiririsha maji yanayoingia katika  ziwa hilo.
Kudhibiti  uchafuzi  wa mazingira katika vyanzo vya maji na kuhamasisha matumizi ya teknolojia ya kuhifadhi majitaka kwa vyombo vinavyosafiri katika ziwa hilo.
Miradi  60 ya kijamii ambayo itagharimu kiasi cha bilioni 2 itaibuliwa na  hivyo kuongeza kipato kwa jamii husika baada ya kukamilika.
Miradi hiyo ya kijamii inatekelezwa katika wilaya ya Bariadi, Kwimba, Magu, Maswa, Chato, Musoma vijijini, Manispaa ya Bukoba na Bukoba vijijini.

HAI
TATHMINI iliyofanywa na kituo cha utafiti wa zao la kahawa nchini (TaCRI), imebaini mahitaji makubwa ya miche ya kahawa kwa ajili ya wakulima wa zao hilo, hususani katika wilaya mpya zilizoanzishwa  nchini.
Mwenyekiti wa bodi ya TaCRI,  VEDASTUS NGAIZA  amesema mahitaji ya miche ya kahawa inayozalishwa  haikidhi mahitaji yaliyopo.
Kutokana na hali hiyo mkurugenzi wa TaCRI, profesa JAMES TERI, amesema  mahitaji hayo ni mojawapo ya changamoto kubwa watayoitatua mwaka huu.
Naye naibu mwidhinishaji wa fedha za umoja wa Ulaya kutoka wizara ya fedha, SAMWEL MARWA amesema serikali inaridhishwa na matumizi sahihi ya fedha zilizoinishwa kwa ajili ya kuboresha kazi za utafiti na uimarishaji wa miundombinu sehemu zinazosimamiwa na TaCRI.
MOROGORO
CHAMA cha walimu mkoani morogoro (CWT) kimetoa muda wa wiki moja kwa uongozi wa serikali ya mkoa  huo  kulipa madai ya walimu la sivyo watagoma na kufanya maandamano ya amani kushinikiza malipo hayo.
Pia CWT imeimtaka  mkuu wa mkoa huo, JOEL BENDELA kuitisha kikao cha dharura na wakurugenzi wa wilaya ambazo hazijawalipa walimu, maafisa elimu,TSD ili kutafuta ufumbuzi wa kero hiyo.
Katibu wa CWT mkoani  humo, ISSA NGAYAMA, amesema hatua hiyo ni kufuatia  walimu wa wilaya Ulanga, Kilombero, Kilosa  kutolipwa  fedha zao  ili hali mkoa huo umepokea bilioni 1.6 lakini ni bilioni 1.2 ndizo zilizolipwa.
Amesema zaidi ya  milioni 369, hazijalipwa  kwa walimu wapatao 211 wa wilaya hizo na kwamba baadhi ya malipo ya walimu yanaonyesha yamelipwa  huku wahusika wakiwa hawajapata fedha hizo.
Hivyo wanahisi kuna  vitendo vya uchakachuaji wa fedha  hizo.
Amesema kwa mujibu barua ya  katibu  tawala wa mkoa huo ya Januari 10, mwaka huu imewataka wakurugenzi wa Halmashauri za wilaya na Manispaa kulipa madai ya walimu wote lakini baadhi yao hawajalipwa  kwa madai ya vielelezo vimepotea.
Katika hatua nyingine katibu huyo ameitaka serikali kufanya marekebisho ya mishahara na malimbikizo  kwa walimu waliopanda vyeo tangu mwaka 2008 hadi 2011 ambao  ni 1987 na wanaodai malimbikizo  ni 1233.
Amesema  hali hiyo inawavunja moyo  walimu katika utendaji wao na kwamba wamechoka kuvumilia.



FEBRUARI, 15, 2012
BUKOMBE
WATANZANIA  wametakiwa kuomba na kushiriki ipasavyo katika mchakato mzima wa uundwaji wa katiba mpya.
Wito huo umetolewa na mchungaji wa kanisa la FPCT la Ushirombo wilayani Bukombe mkoani Shinyanga,  EDWARD  NGAI.

Amesema haitoshi kuomba  tu na kwamba  wajitokeze kwa wingi kutoa maoni na ushauri katika uundaji wa katiba mpya pindi zoezi hilo litakapoanza.
Pamoja na mambo mengine amesema ni vema kila  mtanzania ajisikie  huru na fahari  katika kutoa maoni yake.
Mchungaji huyo amesema  katika kipindi hiki kila mtanzania anapaswa kuisoma na kuielewa ipasavyo katiba iliyopo ili  kujua mapungufu yaliyopo.

Amesema watanzania wahakikishe wanamuomba MUNGU  ili zoezi  la uundwaji wa katiba mpya lifanyike kwa salama na amani na katiba iwe ya watanzania wote.
DODOMA
MTUHUMIWA wa uporaji wa fedha za jumuiya ya vijana ya CCM wilaya ya simanjiro mkoani  Manyara, OMARY KARIATI, amekiri kuondoka na fedha za vijana hao na kwamba amezitunza.
KARIATI ambaye ni diwani wa kata ya Kwadero wilayani Kondoa, amesema ugomvi wa mbunge wa Simanjiro CHRISTOPHER OLE SENDEKA na mwenyekiti wa vijana mkoa wa Arusha, JAMES OLE MILLYA ndio uliomfanya aondoke na fedha hizo.
Amesema anamilioni 2 za umoja huo zilizopatikana katika harambee na kwamba  anasubiri hali itulie ili azipeleke kwa vijana hao.
Amesema ahadi nyingine za fedha zilizotolewa hadi hii leo bado hazijachangwa.
Diwani huyo amejitokeza kufuatia moja ya gazeti  kuandika kiongozi mmoja wa uvccm wilaya ya Simajiro ameondoka na milioni 26 ambazo alichangisha katika harambee ya mfuko wa vijana.

Amesema  katika harambee hiyo  fedha taslimu milioni  4 zilitumika katika kulipia ukumbi  na chakula kwa wageni.

Pamoja na mambo mengine KARIATI amewahi kuwa katibu wa uhamasishaji wa vijana mkoa wa Dodoma kabla ya kuteuliwa kuwa katibu wa vijana Bukoba mjini na kisha wilaya ya Simanjiro.
 ARUSHA
MAKAMPUNI 100 ya kilimo na nafaka kutoka nchi kumi  barani Afrika , yanatarajiwa kushiriki katika maonyesho ya kilimo na biashara yanayotarajiwa kufanyika jijini Arusha.
Nchi hizo ni  za wanachama wa baraza la nafaka la kanda ya Afrika Mashariki(EAGC).
Pamoja na mambo mengine maonyesho hayo yatalenga zaidi kutoa mafunzo kwa wakulima kuhusu kilimo ,biashara na  jinsi wakulima watakavyoweza kupata masoko ya ndani na nje .
Hayo yamesemwa na mkurugenzi mkuu wa baraza hilo, Gerald Masika na kwamba maonyesho yamelenga kumpa kipaumbele mkulima na yatagharimu takriban dola za kimarekani elfu 90.
Amesema maonyesho hayo yatasaidia kupata utatuzi wa changamoto inayowakabili wakulima ikiwamo jinsi ya kukabiliana na mbegu feki.

Amewataka wakulima nchini kujitokeza kwa wingi kushiriki katika maonyesho hayo ili pamoja na mambo mengine waweze kubadilisha   uzoefu na maarifa  na wakulima wenzao.

DODOMA
HALMASHAURI kuu ya CCM (Nec) imeshindwa kufikia muafaka kuhusu ukomo wa ubunge, uwakilishi na udiwani wa viti maalumu kwa wanawake wa chama hicho.
Pia katibu mkuu wa CCM, WILLSON MUKAMA amesema suala la mwenyekiti wa umoja wa wanawake wa chama hicho (UWT) SOPHIA SIMBA kupewa nafasi ya ubunge ikiwa atashinda uenyekiti, licha ya kuwa ameshatumikia vipindi viwili ni haki yake.
MUKAMA alitoa kauli hiyo alipokuwa akitoa salamu za chama katika kikao cha baraza kuu la wanawake wa UWT mjini Dodoma.
Hata hivyo wajumbe wa UWT wamepinga  msimamo wa chama, wakisema ni lazima kila nafasi iwe na ukomo.
UWT ilipendekeza kuwapo kwa ukomo wa vipindi  viwili kwa wabunge, wawakilishi na madiwani wa viti maalum lakini MUKAMA amesema kamati ya wabunge wa CCM imepinga uamuzi huo.
Hivyo NEC ya CCM imelazimika kurirudisha suala hilo  kwa baraza la wanawake, lijadiliwe upya.

MUKAMA amesema  hoja za wabunge ni kuwa  ukomo wa vipindi viwili  hautoshi na kwamba utawapa nafasi watu wasio na uzoefu kuingia katika nafasi hiyo nyeti.

Katika ufunguzi huo, mwenyekiti wa UWT Sophia Simba aliwakumbusha wanawake kuwa makini katika kipindi cha uchaguzi ndani ya Jumuiya hiyo na kwamba kuna mapandikizi kutoka vyama vya upinzani.
ZANZIBAR
WIZARA ya Afya  Zanzibar imeandaa mfumo mpya wa uchangiaji huduma za afya ili wananchi waweze kushiriki  kikamilifu.
Hatua hiyo imefikiwa kufuatia  mfumo uliopo wa uchangiaji huduma za afya kutokuwa wazi.
Hayo yamesemwa na waziri wa wizara hiyo, JUMA DUNI HAJI na kwamba  huo ni mpango mkakati wa kutekeleza sera mbalimbali za wizara hiyo.
Amesema mfumo  huo mpya upo katika hatua ya mwisho na utekelezaji wake utaanza wakati wowote.

Waziri Duni amesema  mfumo huo utakaoitwa afya ya jamii  utakuwa na kamati  maalumu katika kila ngazi.

Pamoja na mambo mengine amesema wananchi wataendelea  kukabiliwa na magonjwa tofauti ikiwamo ya miripuko kama mipango madhubuti ya kiafya haitowekwa.

Amesema elimu ya afya ndio msingi wa kinga, ambayo inahitajika kutolewa kikamilifu kwa jamii ili kuweza kuielewa.

Katika hatua nyingine amesema wizara ya afaya  bado inakabiliwa  na changamoto  nyingi ikiwamo ya upungufu wa wafanyakazi dawa, vifaa, ongezeko la wagonjwa katika hospitali na wanaohitaji kupatiwa matibabu  nje ya nchi.

Changamoto nyingine ni muamko mdogo wa wananchi katika  kukabiliana na magonjwa ya kuambukiza na yasiyoambukiza.



FEBRUARI 14, 2012
KAHAMA
WANANCHI  mkoani shinyanga wametakiwa kuondokana na hisia na dhana potofu  kwa wazee na  kuacha  vitendo vya mauaji  dhidi ya wazee na maalbino.
 Wito huo umetolewa  hii leo na mkurugenzi wa wilaya ya kahama Bi ELIZA BWANA kwa niaba ya mkuu wa mkoa wa Shinyanga, ALLY  RUFUNGA  katika semina ya kongamano ya kujadili  hali ya mauaji ya wazee  kwa imani ya kishirikina.
Meneja mradi wa shirika la SHIDEPH  PLASI kahama, VENAS MUZIKA amesema wananchi wanapaswa kutambua haki za msingi za  wazee ikiwamo ya kuishi bila kubuguziwa.
Pia ametaka kuboreshwa kwa makazi  na usalama kwa wazee ili kuwaepusha na mauaji ambayo yamekuwa yakiongezeka kila siku.
Naye Meneja mradi wa shirika la  HELP AGE INTERNATIONAL, LEONARD NDAMGOBA amewataka wananchi kuwa na ushirikiano na vyombo vya usalama ili kutokomeza mauaji ya wazee.
Amesema mahala penye ushirikiano mzuri kati ya wananachi na   vyombo  vya usalama hakuwezi kuwa na vitendo viovu.
Kuanzia mwaka 2007 hadi mwaka 2011 jumla ya wazee 149 wameuwawa  wilayani kahama  huku wilayani Bukombe  idadi ikiwa ni  94.
Miongoni mwa sababu za kuuwawa kwa wazee hao ni  watoto  kuharakisha kurithi  mali pamoja na imani za kishirikina.
Semina hiyo ya siku mbili inayofanyika wilayani kahama imewakutanisha wadau mbalimbali ikiwamo kamati ya ulinzi na usalama ya mkoa wa shinyanga.
DODOMA
WANANCHI waishio vijijini wametakiwa kuzijua ipasavyo bajeti za serikali za vijiji na kata zao  na kufuatilia shughuli za maendeleo yao.
Wito huo umetolewa na mratibu wa Better Life, HIDAYA MIDEGA alipokuwa akifungua  mafunzo kwa viongozi wa vijiji na kata ya Chihanga Manispaa ya Dodoma.
Mafunzo hayo yaliyofadhiliwa na shirika la Civil Society Foundation, pamoja na mambo mengine wataunda timu za ufuatiliaji wa mali za umma.
MIDEGA amesema wananchi kuendelea kuwalalamikia viongozi wa serikali wanatumia ovyo fedha  za umma bila ya kuijua bajeti yao ni sawa na  kutwanga maji kwenye kinu.
Amesema ili kudhibiti  vitendo hivyo ni lazima wanakijiji waijue bajeti na  namna ya kuhoji matumizi ya fedha  ikiwamo walizochanga katika michango mbalimbali.
Midega amesema wananchi wanapaswa  kuwa na ujasiri wa kuhoji mapato na matumizi  na pia viongozi wao wanatakiwa kujua namna bora ya uandaaji wa bajeti.
Pamoja na mambo mengine  amewataka wananchi kutambua namna ya kujenga utawala bora hadi vijijini  na kwamba  tafiti nyingi zinaeleza  kuwa hali za wananchi hasa wa vijijini  ni duni  na hilo linachangiwa zaidi na kutojua jinsi ya  kuhoji matumizi na mapato.
SONGEA
MVUA kubwa iliyoambatana na upepo mkali imebomoa zaidi ya nyumba 13 katika kata ya Ruvuma manispaa ya Songea mkoani Ruvuma.
Pia mvua hiyo iliyonyesha jana kwa saa moja  imeathiri mazao,miti na miundombinu mbalimbali.
Mvua hiyo iliyonyesha majira ya saa tisa jioni hadi saa kumi imeleta athari katika kata ya Mshangano  ,Bombambili ,Mfaranyaki, Lizaboni, Ruhuwiko, Majengo, Subira na Ruvuma.
Mkuu wa wilaya  ya songea  THOMAS OLE  SABAYA amesema  tathimini ya athari  iliyojitokeza bado haijajulikana na kwamba wakazi wa kata hizo wanahitaji msaada wa haraka.
Amesema pamoja na mambo mengine, wakazi hao wanahitaji mahala pa kuishi, chakula na mahitaji mengine muhimu ya binadamu.

MBEYA
MKAZI  wa kitongoji cha Busungo kijiji cha Mpakani wilayani Rungwe Mkoani Mbeya, ameuawa kwa kupigwa na watu kwa tuhuma za wizi wa mahindi.
Kamanda wa polisi mkoani humo, Advocate Nyombi amemtaja marehemu kuwa ni IVO MWAMPOLE (70) ambaye ni mkulima na mkazi wa kijiji cha Busale wilayani Kyela.
Amesema tukio hilo limetokea jana majira ya saa mbili usiku na kwamba marehemu huyo alikutwa akiiba mahindi kwenye shamba la YOHANE KAMENDU (35) mkulima na mkazi wa kijiji cha Busongo wilayani humo.
Mwili wa marehemu umehifadhiwa katika hospitali ya Makandana wilayani humo na upelelezi wa tukio hilo unaendelea ili kuwabaini waliohusika na mauaji hayo.
Wakati huo huo Jeshi la polisi linamshikilia BERNAD TIKSON (19) mkazi na mkulima wa kijiji cha Izilya wilayani Ileje kwa tuhuma za kukutwa na miche ya bangi nyumbani kwake.

kamanda NYOMBI amesema  mtuhumiwa  huyo pia ni muuzaji na mvutaji wa bangi na atafikishwa mahakamani upelelezi  utakapokamilika.



FEBRUARI,13, 2012
KAHAMA
MKAZI wa Nyasubi wilayani kahama, mkoani Shinyanga, SALUM MRISHO, aliyejimwagia mafuta ya petrol na kujiwasha moto, amefariki dunia.
Amefariki katika hospitali ya wilaya ya kahama, wodi namba moja ambayo zamani ilikuwa ni wodi namba nane alikokuwa akipatiwa matibabu  baada ya  sehemu kubwa ya mwili wake kuungua moto.

Marehemu huyo mwenye umri  zaidi ya miaka 45, alijimwagia  mafuta na kujichoma  jana majira ya mchana nyumbani  kwake.

Mmoja wa ndugu wa MRISHO, aliiambia REDIO KAHAMA FM kuwa miongoni mwa sababu za mwanaume huyo kujimwagia mafuta ya petrol na kujichoma ni  migogoro ya kifamilia pamoja na  familia yake kutomsikiliza.

Amesema kabla ya kufanya tukio hilo, aliaga anakwenda Shinyanga mjini lakini baada ya muda arirudi akiwa amebeba mafuta na kuingia chumbani kwake na kujifungia.

Baada ya hapo waliona moto ukiwaka chumbani na ndipo majirani walifanikiwa kuvunja dirisha na kumuokoa.

Marehemu MRISHO anatarajiwa kuzikwa hii leo,

Mungu ailaze roho ya marehemu mahala pema peponi.
DODOMA
HALMASHAURI kuu ya CCM(NEC) imeiagiza serikali kukamilisha mchakato wa kumaliza kabisa mgogoro wa madaktari nchini na kuhakikisha migogoro ya namna hiyo inashughulikiwa mapema ili isiwe na madhara makubwa kwa wananchi.
Pia NEC imeridhishwa na jinsi mchakato wa upatikanaji wa katiba mpya unavyoendelea na kuipongeza serikali kwa jinsi inavyolisimamia swala hilo.
Katibu wa Itakadi na Uenezi wa CCM, NAPE NNAUYE amesema chama hicho kimewataka wananchi wote kushiriki  katika mchakato huo na  huku wakizingatia kutunza amani na utulivu uliopo nchini.
Katika hatua nyingine, NEC chini ya mwenyekiti wa taifa  Jakaya Kikwete, pamoja na mambo mengine imetoa ratiba ya mchakato wa kumpata mgombea wa CCM katika uchaguzi mdogo wa jimbo la Arumeru Mashariki.
Pia imetoa ratiba ya mchakato wa kuwapata wagombea udiwani kwa tiketi ya CCM kwenye kata nane zilizotangazwa na tume ya taifa ya uchaguzi.
NNAPE amesema katika nafasi ya Ubunge kwa Arumeru Mashariki, utaratibu utakaotumika ni wa upigaji  kura za maoni kwenye mkutano mkuu wa Jimbo na kwamba  uchukuaji  na urejeshaji fomu  utanza leo Februari 13 hadi Februari 18 na Februari 27, NEC itafanya uteuzi wa mgombea huyo.

Kuhusu nafasi ya udiwani katika kata 8 za Tanzania Bara kura za maoni zitapigwa kwenye mikutano mikuu ya matawi na uchukuaji  na urejeshaji fomu  utanza leo Februari 13 hadi Februari 16.
MOROGORO
BARAZA la madiwani wa halmashauri ya wilaya ya Kilombero limekataa kuipokea taarifa ya kamati ya Uchumi, Ujenzi na Mazingira kutokana na idara za kamati hiyo kubakiwa na kiasi kikubwa cha fedha huku miradi mingi ikiwa haijatekelezwa.

Hatua hiyo imefuatia baada ya kuwapo kwa mapugufu ya utekelezaji wa miradi mingi iliyokuwa chini ya kamati ya uchumi,ujenzi na mazingira.
Kamati hiyo katika kipindi cha kuanzia Oktoba hadi Disemba mwaka jana ilipangiwa kutumia bilioni 3, lakini ikatumia milioni 614.5 tu huku miradi mingi ikiwa haijakamilika na mingine haijakithi viwango.
Diwani wa viti maalum kata ya Kidatu JANETH UGOBA amesema ni vigumu kwa kiwango hicho cha fedha kubakia ili hali zahanati, madaraja na barabara nyingi zinamatatizo.

Naye diwani wa  kata ya Mofu, SAMSON NGWILA ameitaka halmashauri kuwachukulia hatua kali watendaji wanaokwamisha miradi ya maendeleo na pia kuweka vikwazo  kwa miradi kukaguliwa.
Pia ametaka  makandarasi wote wabovu wanyang’anywe zabuni


. ZANZIBAR
WAZIRI wa Katiba na Sheria  visiwani Zanzibar,  Abubakar Khamis amesema wizara yake inakabiliwa na changamoto nyingi ikiwamo  vitendo vya rushwa.

Pia amesema  vitendo vya rushwa kwa namna moja ama nyingine vimeathiri utendaji wa mahakama pamoja na idara nyingine za serikali.

Ameyasema hayo alipokuwa akizungumzia mipango mikakati ya wizara yake  na jinsi ya  kufikia malengo waliyojiwekea.

Waziri huyo amesema wameanza kutatua hali hiyo na kwamba  kuna sheria zinapaswa kufanyiwa marekebisho na  nyingine  kutungwa upya ili kuendana na wakati.

Hivyo amewataka wananchi kutoa maoni yao kuhusu sheria mbalimbali na kwamba yatafanyiwa kazi.

Pamoja na mambo mengine amesema idara ya mahakama inakabiliwa na changamoto nyingi  ikiwamo upungufu wa majengo, vitendea kazi, uhaba wa mahakimu na kwamba vinachangia kwa kiasi kikubwa kuzorotesha shughuli za utendaji ikiwamo mrundikano wa kesi

FEBRUARI 12, 2012

KISHAPU

MADIWANI wilayani Kishapu mkoani Shinyanga wamemlalamikia mkurugenzi wa halmashauri hiyo, THEONAS NYAMHANGA kwa kutowapatia taarifa ya kuuza magari chakavu manne likiwamo gari STK 843 Mitsubish Dabo kibini ya mwaka 2005, iliyouzwa  kwa shilingi millioni 1.5.
Wakizungumza kwenye kikao cha baraza hilo madiwani hao wamesema  magari hayo yameuzwa bila ya kuwapo zabuni yoyote iliyotangazwa.
Kufuatia hali hiyo wamesema  wanadharauliwa na  watendaji wa halmashauri hiyo na  kwa pamoja wametaka magari hayo yarudishwe.
Diwani wa viti maalumu, JUKE ANDREW amesema kamwe hawawezi kuruhusu  mambo kama hayo yafanyike tena na amewataka madiwani wenzake kuacha huruma katika kusimamia  utendaji wa halmashauri hiyo .

Kutokana na  kubanwa ipasavyo mkurugenzi wa halmashauri hiyo aliomba msamaha na kwamba hatorudia kufanya maamuzi bila  kupata baraka za  baraza la madiwani

SHINYANGA
JESHI la polisi mkoani Shinyanga limewatahadhalisha wananchi kujihadhari na matapeli wa madini  na noti bandia ambao wametapakaa katika maeneo ya migodi

Tahadhari hiyo imetolewa na kamanda wa polisi  mkoani humo, DIWANI ATHUMAN  kufuatia mama mmoja mkazi wa mjini Kahama kuibiwa kwa kutapeliwa milioni 10 taslimu kwa kuuziwa madini ya mabandia.
Amesema mama huyo  ni mtumishi mstaafu wa idara ya afya na alitapeliwa  majira ya asubuhi mwishoni mwa wiki  hii.
Kamanda  huyo wa polisi amewataka wananchi kuwafichua matapeli hao  ili sheria ichukue mkondo wake.
Amesema madini ya dhahabu na almasi ni yenye thamani na hayauzwi ovyo na mitaani.
Wakati huo huo  jeshi la polisi wilayani Kahama inawashikilia watu wanne, wanaume wawili na wanawake  wawili kwa kukutwa na noti badia za shilingi elfu kumi.
 Kamanda ATHUMAN amesema watu hao walikamatwa jana  Jumamosi majira ya mchana katika eneo la Majengo Kahama mjini.
Amesema kukamatwa kwa watu hao ni kufuatia taarifa  kutoka kwa  wasamalia wema hivyo ameomba ushirikiano zaidi.


ZANZIBAR
WIZARA ya afya Zanzibar inatarajia kutunga sheria itakayotoa adhabu kwa wananchi wanaotupa na kuhifadhi ovyo  uchafu kwenye makazi.

Hatua  hiyo imelenga kupunguza uchafu na  mazalia ya mbu ili kutokomeza ugonjwa wa malaria.
Hayo yamesemwa na waziri wa wizara hiyo JUMA DUNI HAJI katika uzinduzi wa kampeni ya ugawaji vyandarua bure kwa wanachi wa Zanzibar itakayoanza mwezi ujao.
Amesema kabla ya kufikia hatua hiyo wizara itaanza kutoa elimu ya kinga ya afya  kwa wananchi na wale watakaokaidi watachukuliwa hatua za kisheria.
waziri Duni amesema kuuondoa kabisa ugonjwa wa malaria inawezekani, na kinachohitajika ni wananchi kubadili tabia  kwa kuishi katika  mazingira safi yasiyo na mazalia ya  mbu.
Kuhusu kampeni ya ugawaji wa vyandarua vyenye dawa ya muda mrefu amesema kila familia itapata vyandarua vitatu.

Hata hivyo  meneja mkuu wa kitengo cha Malaria Zanzibar SULEIMAN ABDALLAH amesema  kuumaliza ugonjwa wa malaria utachukua muda na kwamba idadi ya wagonjwa imepungua.

Zaidi ya vyandarua laki saba vyenye thamani ya dola za Marekani milioni 3.5 vinatarajiwa kugawiwa kwa wananchi bila ya malipo visiwani Zanzibar.




FEBRUARI 11, 2012
DODOMA

SERIKALI imeifunga shule ya Zamzam English Medium ya mjini Dodoma kufuatia kwenda kinyume na sheria na kanuni za nchi.
Hatua hiyo ni kufuatia ziara ya gafla iliyofanywa na  naibu waziri  wa elimu na mafunzo stadi, Philipo Mulugo katika shule kadhaa za mjini Dodoma.
Pia amekemea tabia ya walimu na wanafunzi wa shule ya YOUNG JAI ya kutovaa viatu kwa madai ya masharti ya mmliki wa shule hiyo.
Kufuatia hali hiyo amemuagiza  ofisa elimu mkoa wa Dodoma kuwasiliana na kamanda wa polisi mkoani humo  na vyombo vya usalama kuhakikisha shule hiyo haipokei wanafunzi  wengine.
Amesema shule hiyo  kuendelea kupokea wanafunzi ili hali haijasajiliwa ni kutokuwatendea haki wanafunzi na wazazi wa watoto wanaosoma katika shule hiyo na kwamba walimu na wanafunzi kutovaa  viatu wakiwa shuleni hapo ni  kinyume na utamaduni  wa nchi.
Ameuagiza uongozi  wa shule hiyo kuanzia Jumatatu  ya kesho kutwa  walimu na wanafunzi kuvaa viatu vinginevyo hatua kali za kisheria zitachukuliwa.
Pia waziri  MULUGO alishangazwa na  hatua ya walimu kuchapwa viboko kwa kisingizio cha kutokufundisha kwa kiwango kinachotakiwa na shule hiyo.

Mkurugenzi wa shule hiyo YOUNG  MICHA amesema tabia ya kutokuvaa viatu kwa wanafunzi na walimu ni utaratibu wa nchini kwao Korea na amekubali  kubadili mfumo wa uendeshaji kufuatana na mazingira ya Tanzania.
MOROGORO
WATANZANIA wametakiwa kuachana na mila na desturi zilizopitwa ili kuwawezesha watoto hasa wa kike kupata elimu bora kwa manufaa yao na taifa kwa ujumla.
Wito huo umetolewa mkoani morogoro na mlezi wa Elimu ya Sekondari katika Wilaya ya Morogoro, KASSIMU KISEGEYU.
Pamoja na mambo mengine ametaka kuwachukulia  hatua kali ikiwamo kuwafikisha mahakamani na kuwatangaza hadharani watakaobainika kuwapa mimba wanafunzi ili iwe fundisho kwao na kwa wengine wenye kuendekeza vitendo hivyo.
Amesema pamoja na jitihada za serikali kupambana na  tatizo la mimba kwa wanafunzi lakini  linaendelea kushamiri.
KISEGEYU amesema wanafunzi wengi wanashindwa kuendelea ma masomo na kwamba watu wanaowabebesha ujauzito, hawachukuliwi hatua kutokana na wazazi kutotoa taarifa kwa vyombo vya dola.
Mkuu wa shule kata ya Mikese Gaudence Mhoha amesema idadi ya wanafunzi wanaomaliza kidato cha nne shuleni hapo inapungua kutokana na sababu mbalimbali ikiwamo  ujauzito na utoro.
Naye mwenyekiti wa bodi ya shule  hiyo, SAID SAID amewaonya wazazi watakaobainika kuwaozesha watoto wao na  kuwakatisha masomo kuwa watachukuliwa hatua kali za kisheria.
ZANZIBAR
TUME ya uchaguzi Zanzibar(ZEC) imesema matayarisho kwa ajili ya uchaguzi mdogo wa jimbo la Uzini utakaofanyika kesho  Jumapili yamekamilika
Akizungumza na wandishi wa habari mara baada ya kukabidhi vifaa vya kupiga kura msimamizi wa uchaguzi wilaya ya kati Mussa Haji Juma amesema vifaa vyote vimekamilika na hakuna upungufu uliojitokeza.
Pamoja na mambo mengine msimamizi huyo amewataka wananchi wa jimbo  hilo wenye sifa za kupiga kura kujitokeza kwa wingi  kuchagua mgombea wanayemtaka.
Mwenyekiti wa chama cha wakulima (AFP) SAID SOUD amewahimiza wasimamizi wa uchaguzi ikiwamo jeshi la  polisi kudumisha nidhamu  ili uchaguzi ufanyike kwa amani na utulivu.
Naye katibu wa Chama cha CUF Wilaya kati, HAJI JUMA amesifu uendeshaji wa kampeni za kistaarabu katika jimbo hilo bila malumbano ya kisiasa na kupigana.
Amesema iwapo mgombea wa chama hicho atashindwa chama kitayakubali  matokeo .
Uchaguzi mdogo wa jimbo la uzini unaofanyika kesho Jumapili unakipambanisha  chama cha   CCM, CHADEMA, CUF, TADEA na AFP.
Katika hatua nyingine, chama cha AFP kinatarajia kumfikisha mahakamani mgombea wa CCM jimbo la Uzini Mohammed Raza,  hata kama atashinda katika uchaguzi huo.
Hatua  hiyo ni kutokana na uhalali wa uraia wa Raza kikidai mgombea huyo anamiliki hati mbili za kusafiria ambapo ni kinyume na sheria za nchi .
Mgombea uwakilishi wa jimbo hilo kupitia AFP, RASHID MSHENGA amesema a mwanasheria wa chama  hicho anaandaa utaratibu wa kumfikisha Raza mahakamani.

FEBRUARI 10,2012
SHINYANGA
MIUNDOMBINU hafifu ikiwamo kukaa chini darasani  inachangia kwa kiasi kikubwa kufeli kwa wanafunzi  hasa wa kike.
Hayo  yamesemwa kwenye mdahalo na afisa wa idara ya elimu mkoani Shinyanga, Bi BEATRICE MAMBONEA na kwamba wanafunzi wasichana wanashindwa kwenda shule wakiwa katika siku zao kwa kuhofia kunyanyuliwa kira mara.
Amesema kutokana na kukaa chini  huko wengi wa wasichana  uathirika  kisaikolojia ikiwamo  kuumwa migongo  na kupelekea  kutoelewa  ipasavyo  masomo.

Afisa huyo amesema  pamoja na  juhudi za makusudi za serikali kutaka kumnyanyua mwanamke, juhudi hizo zinaweza kukwama kutokana na kutokuwapo kwa ushirikiano
Pamoja na mambo mengine amewataka wazazi kuchangia madawati ili kuepusha hali hiyo.
Mdahalo huo uliandaliwa na  shirika la kutokomeza utoro wa wanafunzi mkoani shinyanga(YHDA)kwa ufadhili wa shirika la Foundation for Civil Society.

DODOMA
SERIKALI imesema mishahara ya walimu imekuwa ikipanda kwa kiasi kikubwa kuliko watumishi wengine nchini.
Waziri wa nchi, ofisi ya rais menejimenti ya utumishi wa umma HAWA GHASIA amesema mishahara ya walimu imekuwa ikipanda kila mwaka.
Amesema katika kipindi cha mwaka 2005 hadi mwaka 2011, kiwango cha upandaji wa mishahara kwa walimu kimekuwa kwa asilimia 12 na 12.4 kwa mwaka wakati kada zingine mishahara iliongezeka kwa asilimia 5 hadi 12.6 kwa mwaka.
Alikuwa akijibu swali la msingi la mbunge wa  jimbo la Kisarawe (CCM)  SELEMAN JAFU aliyetaka kujua serikali ina mpango gani wa kushughulikia tatizo la mishahara kwa walimu ambayo imekuwa haipandi mara kwa mara na kufanya walimu wawe na ugumu wa maisha.
Waziri GHASIA amesema mwaka 2005, mwalimu wa daraja la tatu A’  alianza na mshahara wa Sh 74,570 ambapo kwa sasa mwalimu huyo anaanza na mshahara wa sh 244,400 kwa mwezi.
Amesema walimu wa Stashaha walianza na mshahara wa Sh 108,800 na sasa wanaanza na Sh 325,700 wakati walimu wa shahada walikuwa wakianza na mshahara wa Sh 140,000 lakini kwa sasa wanaanza na mshahara wa Sh 449,200 kwa mwezi ambalo ni ongezeko la asimilia 235.14.
Kuhusu posho za walimu za kujikimu pamoja na usafiri kwa walimu wanaokwenda katika mazingira magumu, amesema serikali imeboresha mazingira yake ikiwamo kuwapaa mikopo kulingana na mishahara yao.
MOROGORO
WATANZANIA wametakiwa kutoidharau elimu ya ufundi stadi  na kuiona  kama  sehemu ya kuwapeleka vijana wasio na uwezo, waliofanya vibaya kitaaluma au kukosa fursa za kujiendeleza katika maeneo mengine.
Wito huo umetolewa  na mkuu wa chuo cha Mafunzo ya Ufundi Stadi VETA, MKUMI  CRISTOPHER, na kwamba kama mafunzo ya ufundi stadi yatadharauliwa kuna hatari  ya kukosekana kwa watenda kazi wenye ujuzi.

Pamoja na mambo mengine amesema VETA katika kukabiliana na changamoto mbalimbali  imeanzisha maabara maalum ya lugha ya kiswahili, kiingereza na kifaransa pamoja na kituo cha maelekezo ya utalii.
Mkuu huyo  wa VETA amewataka watanzania kuondokana na mtazamo wa kuajiriwa pekee na kujiajiri ndio mtazamo mpya katika mataifa mbalimbali na kwamba elimu ya ufundi ina fursa pana zaidi  katika  hilo na maisha kwa ujumla.

SONGEA
DIWANI wa kata ya Mletele CCM, katika Halmashauri ya manispaa ya Songea mkoani Ruvuma,  FLAVIAN TAMAAMBELE  amefariki dunia.

 katika hospitali ya mkoa Songea kutokana na kusumbuliwa na ugonjwa wa Malaria .

Mstahiki Meya wa  halmashauri  hiyo, CHARLES MHAGAMA amesema diwani huyo amefariki katika hospitali ya  Songea  kwa ugonjwa wa malaria.

Amesema hadi umauti unamkuta jana asubuhi, alikuwa amelazwa kwa muda wa siku 14.

Meya huyo amesema maziko ya diwani huyo yatafanyika kesho  februari 11 mwaka huu majira ya saa saba mchana kijijini kwao  Mletele.

TAMAAMBELE ambaye amekuwa diwani wa kata hiyo kwa awamu mbili  amefariki dunia akiwa na umri wa miaka 69 na ameacha mjane na watoto .
MUNGU ailaze roho ya marehemu mahala pema peponi amin



FEBRUARI 9, 2012
KAHAMA
JESHI la polisi wilayani  kahama  hii leo limewatanya kwa mabomu yenye vishindo wananchi wa kijiji cha nyakato kata ya Nyasubi, waliokuwa wameifunga barabara kuu ya  kwenda nchi jirani .
Katika tukio hilo watu 11 wamekamatwa na jeshi la polisi
Hatua hiyo ya polisi ni kufuatia wananchi hao kuifunga barabara hiyo kwa saa kadhaa m,ajira ya mchana, wakishinikiza kuzungumza na mkuu wa wilaya hiyo, Bahati Matala.

Hapo jana  wananchi hao pia waliifunga barabara hiyo majira ya jioni kushinikiza kujengwa kwa matuta ili  kupunguza ajali.

Tukio la jana lilifuatia baada ya mtu mmoja kugongwa na gari na kufariki dunia.

Diwani wa kata hiyo, LEONARD MAYALA amewataka wananchi kuwa na subira na kwamba mkuu wa wilaya hiyo, atafanya mkutano na wananchi ili kutatua kero hiyo.

Hata hivyo amesema  katika wiki moja na nusu takribani watu watatu wamekufa na kwamba tangu aingie madarakani miaka miwili iliyopita  zaidi ya ajali 18 zimetokea katika eneo hilo.

KISHAPU
MADIWANI wa halmshauri ya Kishapu mkoani Shinyanga wamemkataa mkurugenzi mtendaji wao, THEONAS NYAMHANGA kutokana na halmashauri hiyo  kupata hati chafu na kusababisha ubadhilifu wa fedha nyingi.

Wametoa msimamo huo hii leo mbele ya mkuu wa Mkoa wa Shinyanga Ally Rufunga kwenye  kikao cha baraza  la madiwani.
Wameitaka serikali imuondoe mkurugenzi huyo na kwamba ni kikwazo cha  maendeleo katika Halmashauri hiyo.
Wamesema hati chafu na vitendo vya ubadhilifu ni kufuatia mtendaji huyo kutowajibika ipasavyo ikiwamo kusimamia mapato ma matumizi.

Kufuatia hali hiyo mwenyekiti wa Halmashauri  hiyo, JUSTINE SHEKA alihairisha baraza hilo kutokana na kukosekana kwa taarifa ya yatokanayo
DODOMA
MKAGUZI na Mdhibiti Mkuu wa Hesabu za Serikali (CAG) Ludovick Utouh amesema serikali inafanya madudu katika matumizi yake pamoja na kuanzisha mamlaka bila ya kuwa na mipango kamili.

Hii leo mjini Dodoma, CAG amesema  kuwa amebaini ubadhilifu mkubwa wa fedha katika wilaya ya Kishapu, Rombo na Kilosa na kwamba  sehemu zote fedha nyingi zimetumika bila ya mipango.

Pia amesema ubadhilifu mwinge wa fedha za umma unafanyika katika matengenzo ya magari ya serikali.

Amesema wilaya ya Kishapu imeanzishwa pasipokuwa na mipango maalumu na kwamba kwa miaka mitatu imeipa serikali hasara ya zaidi ya  bilioni  6.7 bilioni.
UTOUH amesema serikali inashindwa kuwadhibiti watumishi wake na kwamba  katika  miaka minne  wilaya ya Kishapu imekuwa na wakurugenzi wanne na waweka hazina wanne.

Amesema si kishapu pekee bali hata wilaya nyingine zina matatizo kama hayo.

Kuhusu ubadhirifu wa fedha katika matengenezo ya magari ya serikali amesema  magari yaliyopo ni mengi na gharama za matengenezo wakati mwingine zinazidi hata gharama za manunuzi
CAG amesema wizara ya Ujenzi haina mipango mizuri wala mwongozo wa matengenezo ya magari ya serikali na kuwa malip[o hufanyika bila hata ya magari kuharibika.

Mwenyekiti wa kamati ya hesabu za serikali mitaa Agostino Mrema ameilaumu serikali kwa kupuuzia ripoti za CAG na inawalinda watuhumiwa wa ufujaji wa fedha za umma.
SONGEA
WATU  wawili kati ya wanne wamekufa papo hapo kufuatia  kuchomwa moto na wananchi wenye hasira kali katika eneo la Ruhuwiko Manispaa ya Songea Mkoani Ruvuma.
Kamanda wa polisi mkoani humo, MICHAEL KAMUHANDA amesema  tukio hilo limetokea jana  majira ya saa 4 asubuhi.
Amesema watu hao wanne walikuwa wamepakizana katika pikipiki mbili tofauti na kwamba walipofika katika eneo hilo, walitiliwa shaka na wananchi na walipohojiwa, wawili walikimbia.
Kupigwa hadi kuchomwa moto ni kufuatia wawili waliobaki kukiri kuhusika  na matukio matatu ya mauwaji ya wasichana  yaliyo tokea katika kipindi cha mwezi mmoja uliopita.
Kamanda huyo amesema wasichana wanapouwawa hukatwa sehemu zao za siri na kwamba hudaiwa kutumika katika kuchimbia madini.
Pamoja na mambo mengine amesema jeshi la polisi  linamshikilia mwanamke mmoja kwa mahojiano zaidi na amewataka wananchi kutojichukulia hatua mkononi.
Miili ya marehemu hao imehifadhiwa katika hospitali ya mkoa wa  Ruvuma.

DAR ES SALAAM
SERIKALI  imemsimamisha kazi katibu mkuu wa wizara ya afya na ustawi wa jamii Bi.BLANDINA NYONI na mganga mkuu wa Serikali Dk DEO MTASIWA ili kupisha uchunguzi dhidi ya malalamiko ya madaktari.
          
Pia serikali imekubali kuongeza posho kutoka ELFU 10 hadi elfu 25 kwa madaktari bingwa na Elfu 20 kwa madaktari wa kawaida katika kipindi cha mpito na kwenye bajeti mpya masuala ya mafao ya madaktari yataangaliwa upya.

Pia imeagiza madaktari wapewe nyumba na Green cards.

Hata hivyo suala la waziri wa afya, Dk HAJI MPONDA na naibu wake, Dk LUCY NKYA limeachwa kwa rais JAKAYA KIKWETE kwa kuwa ndiye mwenye dhamana na viongozi hao.
         
Uamuzi huo umetangzwa  hii leo  jijini Dar es Salaam na waziri mkuu MIZENGO PINDA alipokuwa akizungumza na makundi kadhaa ya madaktari katika Hospitali ya Taifa Muhimbili ikiwa ni sehemu ya jitihada za kumaliza mgomo wa madaktari.
          
PINDA amesema vyombo vya dola kwa sasa vinafanya kazi ya uchunguzi ili kubaini ukweli wa malalamiko hayo wakati watumishi hao wakiwa nje ya ofisi na kwamba atateuliwa kaimu mganga mkuu na kaimu katibu mkuu kuanzia sasa ili kushika nafasi hizo.
          
Wakati huo huo, Bunge limepokea taarifa ya kamati yake ya Huduma za Jamii ambayo ina mapendekezo kadhaa kuhusu hatua za kuchukua ili kumaliza mgogoro unaoendelea kati ya madaktari na serikali.



FEBRUARI, 8, 2012
DAR ES SALAAM,
BARAZA la mitihani  nchini (NACTE)  limetangaza matokeo ya kidato cha nne huku likiwafutia matokeo wanafunzi zaidi ya Elfu-3 kutokana na kufanya udanganyifu katika chumba cha Mitihani.
Katika matokeo hayo zaidi ya wanafunzi Laki Mbili sawa na asilimia 53 wamefaulu Mtihani huo wa kidato cha Nne ambapo ufaulu kwa mwaka huo umeongezeka kwa asilimia 2.63.
Akitangaza matokeo hayo leo mbele ya waandishi wa habari jijini Dar es Salaam Katibu Mtendaji a Baraza hilo Dk JOYCE NDALICHAKO amesema watahiniwa zaidi ya Laki Nne walifanya  mtihani huo mwaka jana
Amesema wanafunzi waliofutiwa matokeo hayo hawataruhusiwa tena kufanya mitihani ndani ya miaka mitano huku wanafunzi walioandika matusi katika karatasi za kujibia maswali watachukuliwa hatua kali za kisheria.
Kuhusu wanafunzi kuandika mashairi ya nyimbo za Bongo Fleva katika karatasi za kujibia maswali nao watachukuliwa hatua kali pindi uchunguzi utakapokamilika ili iwe fundisho kwa wanafunzi wengine.
Udanganyifu huo unatokana na wanafunzi kukutwa na majibu katika simu za mikononi kwenye chumba cha Mitihani, wanafunzi kufanyiwa mitihani na watu wengine pamoja na kubainika na mfano wa majibu usio wa kawaida.
DAR ES SALAAM
WANAHARAKATI  jijini Dar es salaam hii leo wameandamana kuishinikiza serikali kuchukua hatua na kutatua mgogoro wa mgomo wa madaktari.
Hata hivyo, jeshi la polisi kanda maalumu ya Dar es salaam limewatawanya wanaharakati hao  waliokuwa wamefunga Barabara ya Ali Hasan Mwinyi katika Daraja la Salender jijini Dar es saalam na kusababisha msongamano mkubwa wa magari.
Miongoni mwa wanaharakati hao ni kutoka Chama Cha Waandishi wa Habari Wanawake-TAMWA na Kituo Cha Haki za Binadamu ambao pamoja na mambo mengine wanataka Waziri wa Afya na Ustawi wa Jamii Dk HAJI MPONDA kujiuzulu pamoja na katibu mkuu wake 
BLANDINA NYONI.
Wakati huo huo, Kamati ya Uongozi ya Bunge leo imekutana Bungeni mjini Dodoma katika kikao cha kuangalia namna ya Bunge kutoa tamko kuhusu mgogoro unaoendelea kati ya Madaktari na serikali hususani mgomo wa Madaktari katika Hospitali ya Taifa Muhimbili jijini Dar es salaam.
Kamati hiyo imekutana kufuatia Naibu Spika wa Bunge JOB NDUGAI kuagiza hivyo baada ya Wabunge Sita kutoa hoja kwa Bunge kuacha shughuli zake na badala yake lijadili mgomo huo unaoendelea katika baadhi ya Hospitali za serikali.
Mapema Jana, Hospitali ya Taifa Muhimbili imetangaza kusitisha huduma za kawaida isipokuwa zile tu za dharura kutokana na mgomo huo wa Madaktari kwa kuwa inakabiliwa na upungufu mkubwa wa Madaktari.KAHAMA
JUMLA ya kaya 96 zilizoathiriwa na  mvua iliombatana na upepo mkali mwezi uliopita katika vijiji vitatu vya kata ya Mwendakulima, zimepewa msaada wa vyakula kutoka mfuko wa maafa wa wilaya ya kahama.
 Mkuu wa wilaya ya kahama,meja mstaafu, BAHATI MATALA ametaja  msaada huo kuwa ni gunia kumi za mahindi, mchele  na kilo mia  nne za maharage.
Amesema katika msaada huo mgodi wa Buzwagi umetoa gunia kumi za mchele na kilo mia mbili za maharage na  mfuko wa maafa wa wilaya ya Kahama umetoa  gunia kumi za mahindi na kilo mia mbili za maharage na kwamba zimegawanywa katika  kaya  96  zilizopo katika kijiji cha  Mwime, Chapurwa na Mwendakulima.
 Pamoja na msaada huo wananchi hao bado wana changamoto kubwa za maisha yao kutokana na kukosa mahali pa kuishi  hivyo  mkuu huyo wa wilaya amewataka wasamaria wema kuendelea kuwasaidia.
Pia amewataka wananchi kupanda miti kwa wingi ili kuepukana na madhara ya mvua, upepo na ukame.
KAHAMA
MKUU wa wilaya ya Kahama, mkoani Shinyanga meja mstaafu BAHATI MATALA ameitaka Halmashauri ya wilaya kutoa upendeleo kwa shule za sekondari za kata zinazofanya vizuri kitaaluma kwa kuzipa walimu wa kutosha wa masomo ya sayansi.
Amesema hatua hiyo itaongeza  changamoto kwa  shule nyingine kufanya vizuri kama ilivyo kwa shule binafsi
Amesema hayo katika makabidhiano ya shule ya sekondari ya kata ya mwendakulima iliyojengwa mgodi wa dhahabu wa Buzwagi.
 MATALA amesema ni vigumu kuziwezesha shule zote  kwa pamoja na kwamba  ni vigumu kwa shule zenye walimu wawili au watatu zikafanya vizuri, kitaaluma.
Meneja mgodi huo BOYD TIMLER amesema pamoja na mengine kinachotakiwa ni kutolewa kwa elimu bora.

Mkuu wa shule hiyo iliyogharimu bilioni 1.2, DIANA KUBOJA amesema baadhi ya watu wasiojulikana wameanza kuiba miundombinu ikiwamo masinki ya choo na vitu vingine vyenye thamani, hivyo amewataka wananchi kuimarisha ulinzi.
 DODOMA
SERIKALI imesema  itawanyanganya wamiliki wote wenye mashamba makubwa ambayo hawayatumii.

Waziri wa Ardhi na Maendeleo ya Makazi, profesa  ANNA TIBAIJUKA amesema serikali inaendelea na sensa kubaini mashamba hayo.

Amesema  wote watakaobainika kuwa na mashamba ambayo hawayatumii na kukodisha kwa  wengine  watanyang’anywa na kugawiwa  watu wengine watakaomba ikiwamo vijana.

Alikuwa akijibu swali la nyongeza la ESTER BULAYA (Viti Maalumu-CCM) aliyetaka kujua Wizara hiyo ina mipango gani ya kuwapatia vijana ardhi.

Akijibu swali la msingi, waziri Tibaijuka amesema Serikali inakamilisha utayarishaji wa program ya kitaifa ya kupima mashamba ya wanakijiji na kutoa hatimiliki za kimila kwa kutumia uzoefu uliopatikana kutoka wilaya ya Babati,Mbozi na Manyoni.

Waziri huyo amesema ni wakati wa vijana kujiunga katika makundi kwa ajili ya kuomba viwanja ili wajenge  nyumba za kuishi.
Hata hivyo amesema miaka mitatu baada ya kupewa  viwanja hivyo  na havikuendelezwa, wamiliki watanyanganywa na kupewa wengine.

Pamoja na mambo mengine waziri  huyo amezitaka halmashauri za miji na wilaya kufanya maandalizi ya kutekeleza program ya kitaifa ya kupima mashamba na kutoa hatimiliki za kimila.

DAR ES SALAAM
TUME ya taifa ya uchaguzi(NEC) imetangaza kuwa  uchaguzi mdogo wa ubunge katika jimbo la Arumeru Mashariki mkoani Arusha, utafanyika April mosi mwaka huu.
Uchaguzi huo utafanyika baada ya jimbo hilo kuwa wazi kutokana na kifo cha aliyekuwa mbunge wa jimbo hilo JEREMIA SUMARI kufariki dunia Januari 19 mwaka huu.
NEC imesema pamoja na uchaguzi huo mdogo pia kutakuwepo na chaguzi ndogo za madiwani katika kata za Halmashauri mbalimbali nchini.
 Katika uchaguzi mdogo wa ubunge kwenye jimbo la Arumeru Mashariki uteuzi wa wagombea utafanyika Machi 8, na kampeni zitaanza Machi 9 hadi 31 mwaka huu.

Tume hiyo itafanya chaguzi ndogo za madiwani katika kata nane zilizoko katika halmashauri mbalimbali nchini kufuatia kuwepo wazi kwa nafasi za viti vya madiwani ambazo zimetokana na vifo vya madiwani husika.
Katika chaguzi ndogo za madiwani uteuzi wa wagombea utafanyika Machi 5 na kampeni zitaanza Machi 6 hadi 31 mwaka huu.

Kata  hizo ni  vijibweni-Temeke, Kiwanga-Bagamoyo, Kirumba-Mwanza, Logangabilili-Bariadi, Chan’gombe-Dodoma, Kiwira-Rungwe, Lizaboni-Songea na Msambweni-Tanga.
Mwenyekiti wa NEC,  jaji DAMIAN LUBUVA amesema  hakutakuwa na kuandikisha wapiga kura  wapya na kwamba daftari la kudumu la wapiga kura lililotumika wakati wa uchaguzi mkuu uliopita litatumika.

Tume  hiyo imewata wananchi kujitokeza kwa wingi kushiriki katika  chaguzi hizo  na kwamba vituo vya kupigia kura vitafunguliwa saa 1 asubuhi na kufungwa saa 10 alasiri
ZANZIBAR
RAIS wa Zanzibar, Dk Ali Mohammed Shein amezitaka taasisi zinazosimamia haki kutoa elimu ya athari na hatua za kuchukua kukabiliana na  vitendo vya rushwa.
 
Ametoa wito huo alipokuwa alipokuwa akizungumza na majaji, mahakimu, mawakili, na wadau mbalimbali wa sheria katika maadhimisho ya siku ya sheria visiwani Zanzibar

Amesema elimu ya madhara ya vitendo vya rushwa ikitolewa ipasavyo,  tatizo hilo litapungua.

Rais SHEIN amesema katika kukabiliana na tatizo hilo  serikali itasimamia ipasavyo sheria ya kupambana na rushwa na kwamba  hatua za sheria zitachukuliwa  kwa wote wanaojihusisha na vitendo hivyo.

Naye jaji mkuu wa Zanzibar,  OMAR OTHMAN MAKUNGU amesema taasisi yake inakabiliwa na   changamoto nyingi ikiwamo ikiwamo  uchache wa  ofisi, maslahi madogo na utashi mbovu wa watendaji.

Amesema watendaji wawili waandamizi wa mahakama wamechukuliwa hatua za kisheria kutokana na kuvunja maadili ya kazi.


JANUARI, 7, 2012
KAHAMA
MBUNGE wa Jimbo la Kahama, mkoani Shinyanga JAMES LEMBELI amewataka wanawake kujiunga kwenye shughuli za uzalishaji mali ili kukabiliana na hali ngumu ya kiuchumi inayoikabili taifa.
Ametoa wito huo katika hafla ya chama cha wanawake wilayani Kahama CHAWAKA

Pamoja na mambo mengine amewataka  kuacha makundi yenye lengo la kurudisha nyuma maendeleo yao na kwamba  wawe na malengo ya kujiongezea kipato na aliwachangia milioni 2.5 zitakazowasaidia kuimarisha mfuko wao.

Pia mkuu wilaya hiyo meja mstafu, BAHATI MATALA lichangia  laki tano, mkurugenzi wa Halmashauri ya Wilaya ya kahama, BI ELIZA BWANA  alichangia laki tatu na mbunge wa jimbo la Meatu (CHADEMA) Meshack Opurukwa alichangia laki tano 

Naye mwenyekiti wa CHAWAKA ANNA MAGESA amesema  chama hicho kina miaka minne na kimeweza kutatua kero mbalimbali za kiuchumi kwa wanachama wake..

Katika hatua nyingine mbunge LEMBELI ameendelea kukazia uamuzi wake wa kugombea  nafasi ya uenyekiti wa CCM, mkoa wa Shinyanga.

Amewataka  wananchi kuachana na kauli za wanasiasa uchwara ambao hawajawahi kuchangia shughuli zozote za maendeleo.

Hivi karibuni alipotangza uamuzi wa kugombea nafasi hiyo  ilizua marumbano kati yake na viongozi walioko madarakani wa CCM.

SHINYANGA
SERIKALI kuu imeombwa kuanza ujenzi wa hospitali mpya ya mkoa wa Shinyanga ili kupunguza  msongamano mkubwa wa wagonjwa katika hospitali iliyopo.

Ombi hilo limetolewa na mwenyekiti  wa CCM mkoani Shinyanga HAMISI MGEJA katika maadhimisho ya sherehe ya  CCM kutimizia miaka 35 ya kuzaliwa zilizofanyika katika kata ya Mwawaza manispaa ya Shinyanga.

Amesema hospitali ya mkoa ambayo ni ya rufaa imezidiwa kwa wagonjwa,  wengi wao wakitokea wilaya ya Kishapu na Shinyanga.

Pia amesema hospitali hiyo hailingani na hadhi ya kuwa hospitali ya mkoa na  rufaa kufuatia kukumbwa na uhaba wa vifaa, na watendaji ikiwamo madaktari bingwa.

Naye mlezi wa CCM mkoani  Shinyanga, kapteni mstaafu JOHN CHILIGATI amesema atalifikisha suala hilo kwa wahusika ili kupatiwa ufumbuzi.

Pamoja na mambo mengine, CHILIGATI amewataka wanaCCM wote kujitokeza kugombea nafasi mbalimbali za uongozi ndani ya chama hicho ambao kwa ngazi ya mashina unatarajiwa kuanza mwezi huu.

DODOMA
WIZARA ya Elimu na Mafunzo ya Ufundi imetangaza  kuwa Februari 28 mwaka huu ni siku itakayotumika kwa ajili ya kuwapima wanafunzi waliojiunga na kidato cha kwanza mwaka huu kama wanajua kusoma au la.

Hayo yamesema hii leo BUNGENI naibu waziri wa elimu na mafunzo ya ufundi PHILIPO MULUGO alipokuwa akijibu swali la nyongeza la mbunge wa Viti maalum(Chadema)  CHRISTOWAJA MTINDA, aliyetaka kujua hatma ya wanafunzi wa kidato cha kwanza wasio jua kusoma na kuandika

Mbunge huyo  ambaye ni msemaji wa Kambi ya upinzani kuhusu masuala ya elimu alitaka serikali itoe ufafanuzi wa namna itakavyoweza kuwasaidia wanafunzi hao ambao wengi watakuwa wamekosa nafasi za kuendelea na elimu ya sekondari.

Katika swali la msingi mbunge wa viti maalumu CCM, ZARINA MADABIBA  alitaka kujua serikali ina mpango gani wa kuangalia upya mitaala ya shule na vyuo ili kuingiza masomo ya usimamizi wa biashara na ujasiliamali ili elimu hiyo iwasaidie vijana katika shughuli za kujitegemea.

Waziri MULUGO amesema kuanzia wanafunzi wa darasa la kwanza hadi vyuo vikuu wamekuwa wakifundishwa somo la stadi za kazi au ujasiliamali  kutegemea na ngazi husika.

Kuhusu wanafunzi wa sekondari ambao watabainika kutojua kusoma na  kuandika, waziri huyo amesema serikali itawaandalia mfumo usio rasmi ikiwamo  kuwapeleka katika vyuo vya Veta kulingana na uwezo wao.
ZANZIBAR
JUMLA ya wanafunzi 11,968 wamefaulu elimu ya msingi na sekondari katika mitihani iliyofanyika mwaka jana, visiwani Zanzibar.

Akitangaza matokeo hayo Waziri wa Elimu na Mafunzo ya Amali, Ramadhan Abdallah Shaaban amesema wanafunzi  11,041,  wasichana  6,066 na wavulana 4,975 watajiunga na kidato cha tatu.

Idadi hiyo ni sawa na asilimia 56.1 ya wanafunzi 19,666 waliofanya mitihani wa kidato cha pili  visiwani humo.

Kwa upande wa darasa la saba, Waziri SHAABAN amesema wanafunzi 843 wamechaguliwa kujiunga na sekondari na kwamba 84 wamechaguliwa katika shule maalumu za vipaji.


Wanafunzi 22 wamefutiwa matokeo  kutokana na kubainika kufanya udanganyifu katika mitihani yao.

Shule zilizofanya  vizuri ni  Mwanakwerekwe B, Nyerere Sekondari na Michakaini huku wilaya za mjini, Magharibi na Kati zikiibuka  wilaya bora kwa upande wa mtihani wa kidato cha pili.

Shule zilizofanya vibaya ni Bububu Sekondari  iliyopo wilaya ya Magharibi, Uzi iliyopo wilaya ya Kati na Kinyasini ya wilaya ya Kaskazini A Unguja.

Pamoja na mambo mengine waziri SHAABAN amesema sababu ya wanafunzi wengi kufeli  ni  wengi wao kutegemea mitihani  iliyovujishwa



JANUARI 6, 2012
KAHAMA
KAIMU mkuu wa wilaya ya Bukombe, mkoani Shinyanga  meja mstaafu BAHATI MATALA amewataka watumishi wa idara ya mahakama, polisi, afya kuacha kuwanyanyasa na kuwaomba rushwa wananchi.
Amesema malalamiko mengi anayopata kutoka kwa wananchi ni utendaji wa idara hizo katika kuwahudumia wananchi na kwamba zinafanya kazi kibabe na haziwathamini wananchi.
Matala ambaye pia ni mkuu wa wilaya ya kahama amesema kibaya zaidi ni kwa idara hizo nyeti
kuwaomba wananchi rushwa  ili wahudumiwe au kutendewa haki.
Amesema hali hiyo inasikitisha  na haivumiliki hasa katika nchi yenye misingi ya utawala bora na demokrasia.
Pia amesema matendo hayo ni kinyume na maadili ya utumishi wa umma
Pamoja na mambo mengine MATALA amesema hatua za kinidhamu na za kisheria zitachukuliwa dhidi ya mtumishi atakayebainika kuwanyanyasa na kuomba rushwa kwa wananchi.
MOSHI
JUMUIYA ya wazazi ya CCM, mkoani Kilimanjaro, imelitaka  bunge na mamlaka nyingine za kiserikali, kuchukua hatua za makusudi  kufuta posho ambazo ni  kero kwa wananchi.

Wito huo umetolewa na mwenyekiti wa jumuiya hiyo,
THOMAS NGAWAIYA alipokuwa  akiwahutubia wananchi  kwenye kilele cha maadhimisho ya miaka 35 ya kuzaliwa kwa CCM.
Ngawaiya aliyekuwa mgeni rasmi kwenye maadhimisho hayo yaliyofanyika kiwilaya Moshi mjini, amesema  kufutwa kwa posho, itapunguza kwa kiasi kikubwa  migomo na mivutano  inayoendelea nchini.
Amesema kwa kuanzia ni lazima Bunge kuridhia kufutwa  kwa nyongeza ya posho iliyoongezwa kwa wabunge na kwamba itakuwa chachu ya kumaliza migomo na mivutano iliyopo.
Katika hatua nyingine, amewataka watanzania na wanaCCM  kujali  demokrasia  katika medani ya siasa na kujiepusha na vitendo vya uvunjifu wa amani.
Naye katibu wa CCM, Moshi mjini Aluu Segamba, amesema pamoja na mambo mengine CCM imejipanga kulinda heshima yake, katika misingi ya uwazi na ukweli na utendaji wenye tija.

SHINYANGA
WATU wawili wameuwawa kwa kupingwa na mawe na kisha kuchomwa moto na wananchi kwa tuhuma za kuiba ng’ombe wawili mkoani Shinyanga.
Kamanda wa polisi mkoani Shinyanga DIWANI OTHUMAN amesema  tukio hilo limetokea katika kijiji cha Mwawaza kata ya Masekelo, majira ya saa kumi na mbili na nusu jioni jana.
Amesema kabla ya kuuwawa, marehemu walikamatwa na wananchi wakiwa njiani kwenda kuwachinja ng’ombe hao.
Amewataja waliouwawa kuwa ni MAYUYA KAPONGO mwenye umri wa miaka 33, na mwingine aliyejulikana kwa jina moja la JOHN.
Pamoja na mambo mengine kamanda ATHUMAN amewataka wananchi kuacha  tabia ya kujichukulia sheria mikononi na wafuate sheria kwa kuwafikisha watuhumiwa katika vituo vya polisi. Jeshi la polisi linaendelea  kuwatafuta wananchi waliohusika na tukio hilo.
 DODOMA
SERIKALI imeonya kuwafutia leseni na kusimamisha biashara za  wanunuzi wa zao la korosho nchini iwapo watashindwa kununua zao hilo katika muda muafaka.
Hayo yamesemwa leo BUNGENI  Dodoma na naibu waziri kilimo,chakula na ushirika, injinia. CHRISTOPHER CHIZA.
Amesema kushuka kwa soko la korosho nchini ni kufuatia asilimia kubwa ya wanunuzi wa zao hilo, kutonunua zao hilo katika muda muafaka na kupelekea zao hilo  kuharibika.
Pamoja na mambo mengine naibu waziri huyo amesema serikali haiko tayari kuvumilia hasara wanazozipata wakulima wa zao hilo na kwamba  inakwamisha maendeleo ya wakulima wa zao hilo
 DODOMA
NAIBU waziri ofisi ya waziri mkuu tawala za mikoa na serikali za mitaa, KASSIMU MAJALIWA ameshindwa kulieleza Bunge, lini serikali itatoa jibu la ukaguzi wa kampuni ya usafirishaji Dar es Salaam (UDA).
Hatua hiyo inafuati baada ya kuulizwa swali la nyongeza na Mbunge wa Kigoma Kaskazini ZITTO KABWE aliyetaka kujua  lini serikali atatoa majibu hadharani ili kurusuhu kamati ya bunge ya Mashirika ya Umma iweze kufanya kazi yake.
Majaliwa amesema kuwa serikali kupitia Ofisi ya Waziri Mkuu inajaribu kwa kila liwezekanalo kuona namna itakavyoweza kuleta haraka majibu hayo ambayo yanategemewa kutoka kwa mkaguzi na mdhibiti mkuu wa hesabu za serikali(CAG).
Katika swali la msingi PHILIPA MTURANO (Viti Maalum- Chadema) alitaka kujua serikali ina mkakati gani wa kufufua mradi wa usafiri wa mabasi ya wanafunzi katika miji mbalimbali.
Waziri MAJALIWA amesema serikali inatambua tatizo la usafiri kwa  wanafunzi katika miji mingi ikiwamo Dar es Salaam na kwamba serikali inashirikiana na sekta binafsi ili kutatua tatizo hilo.
Pamoja na mambo mengine amesema serikali haifanyi biashara hivyo inasimamia na kupanga viwango vya nauli kupitia mamlaka zake  husika.
 ZANZIBAR
VIJANA walioachana na matumizi ya madawa ya kulevya wametakiwa kuepukana na vishawishi  vitakavyo warejesha  katika utumiaji wa madawa hayo.
Wito huo umetolewa na mratibu wa idara ya madawa ya kulevya Zanzibar, MAHMOUD MUSSA katika hafla maalumu za kuwatunuku vyeti baadhi ya vijana waliotimiza mwaka mmoja  hadi mitatu bila ya kutumia madawa hayo.
Amesema hatua hiyo  si ndogo na inapaswa kuigwa na kwamba waendelea na msimamo huo na si kurejea katika matumizi ya  madawa hayo.
MUSA amesema hadi kufikia Disemba mwaka jana idadi ya vijana waliopata nafuu katika utumiaji wa madawa hayo imefikia 1,138.
 Naye mkurugenzi wa idara ya kupambana na madawa ya kulevya kutoka ofisi ya makamu wa kwanza wa rais. AHMED AWADHI amesema serikali inawaunga mkono wadau wote wanaopambana na matumizi ya madawa ya kulevya.



FEBRUARI, 5, 2012
SHINYANGA
CHAMA cha mkopo manispaa ya shinyanga (SACCOS) kimewavua madaraka mwenyekiti wake, ASHA MBWANA  na   mweka hazina DEVOTA BALTAZAR , kwa tuhuma za kuchukua  milion 23.8 za chama hicho.


Pia wanachama na  bodi ya chama hicho imewataka  kurejesha fedha hizo  kabla ya  hatua za kisheria hazijachukuliwa.

Uamuzi huo umetangazwa hii leo katika  kikao chao kilichofanyika, mazingira centre  shinyanga mjini.

Watuhumiwa hao wamepewa  miezi miwili  kurejesha  fedha hizo na kwamba ikishindikana watauza mali  zinazomilikiwa na  viongozi hao.


Mwenyekiti ya kamati ya usimamizi  wa saccos hiyo, Thecla  Bogoye amesema  uzembe ndio umepelekea kuliwa kwa fedha  hizo.

Amesema walijipatia fedha hizo nje ya utaratibu wa mikopo na kwamba   MBWANA alichukua million moja, BALTAZAR milion 17, MAJALIWA KATONGA milioni 3 na  Mrisho  milion 2.5 
Naye afisa ushirika mkoani humo, HAMISI MDOMA ametaka kuwapo kwa ushirikiano mzuri kati ya bodi na wanachama.   Chama hicho kinawanachama 142.
DODOMA
SERIKALI  imetahadhalishwa kuwa inaweza kuanguka wakati wowote kama haitatimiza mahitaji na madai ya walimu ambayo yamekuwa mengi kupita kiasi.

Pia watumishi wa wizara ya elimu wote wametakiwa kujihuzuru  kutokana na kushindwa  kumaliza kero za walimu.

Onyo hilo limetolewa   hii leo mkoani Dodoma  na umoja wa maafisa elimu nchini (UMET) na kwamba wapo tayari kwa lolote lile.

Wamesema wapo tayari kufa kwa ajili ya kudai haki yao na kwamba chama cha walimu (CWT) kimeshindwa kutatua  matatizo yao  licha ya kuwakata fedha nyingi katika mishahara yao.

Mwenyekiti wa umoja huo MESHACK KAPANGE amesema  CWT imeshindwa kumaliza matatizo yao na ndio maana wamejitokeza ili kuyapigania.

Amesema CWT imeshindwa  kupigania  malimbikizo ya mishahara, kupandishwa  vyeo kwa walimu na namna bora ya kuboresha utumishi wao na kwamba  hadi sasa hawajui wameajiliwa na wizara  gani.

Hata hivyo amesema katika kudai haki zao, hawatogoma na kwamba kufanya hivyo ni sawa na kuwaumiza watoto wa walalahoi.
Naye makamu mwenyekiti wa mtandao huo, Edmund Nditi amesema kilio chao ni cha muda mrefu na kwamba wameamua kujitoa muhanga kupambana na serikali.

HAI
VIFO vingi vya wanawake  vinavyotokana na saratani ya mlango wa kizazi ni kutokana na kuchelewa kupata  matibabu sahihi.

Shirika la kimataifa lilisilo la kiserikali la Grounds for Healthy la nchini Marekani,  lililofanya utafiti wa tatizo hilo nchini,  limesema tatizo hilo linaweza kupatiwa ufumbuzi wa haraka.

Mkurugenzi mtendaji wa shirika hilo nchini Dk
Hellen Stari, amesema kati ya  wanawake 6,000, wanaougua  ugonjwa   wa saratani ya mlango wa kizazi 7,500,  hufariki  dunia.

Amesema mikakati  madhubuti ya  kukabilina na tatizo hilo inahitajika  ili  kuepusha vifo hivyo.

Kufuatia tatizo hilo shirika hilo limezindua mpango wa miaka mitatu wa kinga ya ugonjwa huo

Naye afisa wa  wizara ya afya na ustawi wa jamii Marry Ngowi, amesema serikali ipo kwenye mchakato wa kutoa huduma hiyo na  itaanza  na wanafunzi wa darasa la nne katika shule za msingi.
KIBAHA
MAKAMU wa rais Dk Mohamed  Ghalib Bilali amemuagiza mkuu wa mkoa wa Pwani MWANTUMU MAHIZA  kuwasimamia ipasavyo watendaji wa idara ya afya ili kukabiliana na maambukizi mapya  ya Ukimwi

Pia amewataka  viongozi na watendaji  kutokuwa na  haya wanapozungumzia  athari za  ugonjwa wa Ukimwi  na wametakiwa kutoe elimu zaidi  ya kujikinga na virusi vinavyosababisha  maradhi ya ukimwi.


Ametoa  agizo hilo  wilayani Kibaha mkoani Pwani alipokuwa akifanya majumuisho  ya ziara yake.

Amesema mkoa wa Pwani ni mojawapo ya mikoa nchini  yenye idadi kubwa ya maambukizi  ya  ugonjwa wa ukimwi.


Makamu huyo amesema  hali hiyo si nzuri na inahitaji juhudi za makusudi kukabiliana na tatizo hilo na kwamba  wilaya ya  kisarawe na kibaha mkoani Pwani zinaongoza kwa maambukizi hayo.
Pamoja na mambo mengine amesema, mkoa wa Pwani  unakabiliwa na changamoto ya uharibifu wa mazingira hasa kutokana na kuongezeka kwa shughuli za ujenzi na matumizi ya nishati ya mkaa ndani ya mkoa na jiji la Dar es Salaam.

Amesema ukataji wa miti uendane na kupanda mipya na  ni muhimu kuhakikisha  mazingira ya mazalia ya samaki katika bahari ya hindi yanatunzwa.

Katika hatua nyingine, ameitaka  kamati ya ulinzi na usalama mkoani humo kujipanga  vema katika kukabilina na  wavuvi haramu, wanaotumia  mabomu na sumu  kwa lengo la  kulinda na kutunza rasilimali za mkoa huo.

FEBRUARI 4, 2012
SHINYANGA
MAHAKAMA zimeshauri kutoa elimu ya sheria ya ardhi mara tu inapomaliza kutoa hukumu mbalimbali.

Hatua hiyo imeelezwa kuwa itachangia kwa kiasi kikubwa  kupunguza vifo vinavyotokana migogoro ya ardhi  mkoani Shinyanga.  Wito huo imetolewa  na katibu tawala mkoani Shinyanga, Mwamvua Jirumbi  katika  siku  ya sheria duniani.

Amesema mogogoro mingi ya ardhi inatokea kufuatia wananchi kutojua sheria na kwamba wanasheria wanalazimika kufanya kazi ya ziada kuelimisha umma katika suala hilo.

Pamoja na mambo mengine , katibu tawala huyo amewataka wanasheria kubadilika kutokana na kashfa waliyonayo ya kupenda kupokea rushwa  na wafanye kazi wa uaminifu ili kuondoa migongano katika jamii.

Hakimu mfawidhi wa mkoa wa shinyanga, John Chaba amewataka mahakimu kutofanya kazi kwa mazoea na kutenda haki kwa kila mwananchi.

Pia amewataka mahakimu kupunguza malalamiko ya watu kukaa mahabusu kwa muda mrefu kutokana na kutokamilika kwa upelelezi wa kesi zao vizuri kwa kuzingatia kifungu cha 225 cha sheria ya makosa ya jinai.

Amesema umefika wakati wa kutumia busara zaidi katika kutoa maauzi hasa ya makosa madogo, ikiwamo ya kupigana, kutoleana lugha ya matusi au wizi wa kuku.

Hakimu huyo amesema adhabu mbadala ni mojawapo ya njia ya kupunguza malalalimiko ya mahabusu.

Pia amesema adhabu mbadala inaipunguzia  serikali gharama ya kuwahudumia wafungwa kwenye magereza.
BAGAMOYO
MAHAKAMA ya Hakimu mkazi mfawidhi  wilayani Bagamoyo imemrudisha rumande msichana Eva Abdalah(19), kwa kosa la kukojolea kitabu kitakatifu cha kiislamu Quaraan na kukitumbukiza chooni.

Akitoa uamuzi huo mbele ya maelfu ya wakazi ya Bagamoyo, Hakimu mkazi mfawidhi Said Mkasiwa amesema uamuzi wake huo unatokana na ombi la mwendesha mashtaka wa serikali, William Mwantela.

Mwendesha mashtaka  huyo  ametaka mshtakiwa asipewe dhamana kufuatia  kosa alilofanya linavutia hisia za waumini wa dini ya kiislamu hivyo anaweza kudhurika akiwa nje.

Pia mshtakiwa mwenyewe amekubali kukaa rumande  akihofia usalama wake.

Akisoma hati ya mashtaka, mwendesha mashtaka amesema Januari  4 mwaka huu majira ya saa nane mchana, mshtakiwa huyo akiwa amedhamilia  na akijua kufanya hivyo atawachukiza waumin wa dini ya kiislamu aliamua kukidhalilisha  kitabu kitakatifu cha Quraan kwa kukikojolea na kwenda kukitumbukiza chooni.

Amesema kitendo hicho ni kinyume na kosa kisheria kulingana na kifungu kidogo cha 125 cha kanuni ya adhabu sura ya 16 ya sheria.

Hata hivyo mshtakiwa amekana kosa hilo  na kesi hiyo itasikilizwa tena Februari 16, mwaka huu.
 MKURANGA
MAKAMU wa rais Dk MOHAMED GHALIB BILAL amewataka viongozi wa mikoa  kote nchini kuandaa kambi ya maarifa kwa vijana ili kuwawezesha kupata stadi za maisha na kujiajiri.

Ametoa agizo hili alipokuwa akiwahutubia  wananchi wa kijiji cha Msoga wilayani Bagamoyo katika ufunguzi wa kambi ya maarifa kwa vijana zaidi ya 400 wa mkoa  Pwani.

Amesema kambi hiyo ni msaada mkubwa kwa kundi la vijana katika kujipatia  elimu na ujuzi utakaowasaidia kupata ajira na kuondokana na umaskini wa kipato.

Hata hivyo Dk BILAL amewataka wadau wengine wa maendeleo kubuni mafunzo mengine ya kuwasaidia vijana kupata elimu na ujuzi.

 Pamoja na mambo mengine, makamu huyo wa rais  amechangia milioni 5 zitakazotumika  katika kambi hiyo ya vijana ambayo amesema inamwelekeo wa kukuza uchumi wa nchi.

Awali akimkaribisha makamu wa rais, mkuu wa mkoa wa Pwani, MWANTUMU MAHIZA amesema kambi hiyo ya maarifa kwa vijana ni endelevu  lakini  itakuwapo kwa mwezi mmoja.

Amesema imelenga kuwakusanya  vijana 1000  na kuwajengea uwezo wa stadi  mbalimbali za maisha ikiwamo jinsi ya  kujenga nyumba bora na za kisasa kwa gharama nafuu, mbinu za upandaji miti katika kutunza  mazingira na kilimo cha mpunga katika awamu tofauti tofauti.


FEBRUARI, 3, 2012
KAHAMA
VIONGOZI na wafanyakazi  wametakiwa kuwahudumia wananchi kwa uaminifu na upendo ili kujijengea heshima kabla na baada ya kufariki dunia.

Wito huo umetolewa Paroko wa kanisa katoliki parokia ya Kahama mjini, Padre Rogatus Malulu wakati wa misa ya kuuaga mwili wa aliyekuwa mwenyekiti wa bodi ya afya wilayani  Kahama, Dk  Deusdedit Gedigedi, aliyezikwa  katika manispaa ya Shinyanga.

Padre Malulu amesema uongozi ni dhamana katika jamii na kwamba  baadhi ya viongozi wakubwa duniani walioongoza bila  kufuata  maadili mema na upendo, walishushwa thamani na hata walipokufa, walizikwa kwa kudhalilishwa.

Hivyo amewataka viongozi na wafanyakazi wengine kukumbuka na wao watayaacha madaraka hayo na pia watakufa hivyo wafanye kazi kwa uadilifu na upendo.
DODOMA
WAZIRI wa Ujenzi Dk John Magufuri amewaonya wakandarasi wazembe na wanaofanya kazi chini ya kiwango kuwa atawafukuza katika miradi  na kuwanyima tenda.

Amesema hayo leo bungeni alipokuwa  akijibu swali la  mbunge wa Tabora  mjini, Ismail Rage  na kwamba hatokuwa na  kigugumizi wala huruma kwa wakandarasi wa aina hiyo. Amesema hadi sasa ameshafukuza wakandarasi 2059.

Katika swali lake Rage alitaka kujua kwa nini ujenzi wa barabara ya Tabora- Nzega, Tabora-Manyoni na Tabora-Urambo unakwenda kwa kusuasua.

Waziri Magufuli amesema kusuasua kwa ujenzi wa barabara za Tabora kulichangiwa na mambo mengi ikiwamo makandarasi kuchelewa kufanya upembuzi yakinifu  na kuchelewa kupatika kwa fedha.

Amesema baada ya kupatikana kwa fedha makandarasi hawatakuwa na kisingizio  na kwamba ujenzi wa barabra hizo utagharimu  bilioni  453.
MOROGORO
WALIMU mkoani Morogoro wamepanga kuwakamata viongozi wa chama cha walimu(CWT) mkoani humo, kufuatia kutolipwa madai ya fedha zao.

Hatua hiyo inafuatia baada ya serikali kutangaza kukamilisha hatua ya kwanza na malipo ya madai ya walimu.

Walimu hao zaidi ya 300 wa shule za msingi na sekondari wamesema  malipo yao yanakwamishwa  na uongozi wa CWTmkoani humo.

Pamoja na mambo mengine wanataka viongozi hao waondolewe katika mkoa huo.
MKURANGA  
MAKAMU wa rais Dk MOHAMED GHALIB BILAL ametaka wasichana wasomeshwe hadi   kufikia vyuo vikuu ili kupunguza tatizo la upungufu wa wafanyakazi nchini.

Ametoa wito huo katika mkutano wa hadhara uliofanyika katika viwanja vya shule ya msingi Mwalusembe wilayani Mkuranga, mkoani Pwani.

Amesema nchi inakabiriwa na upungufu mkubwa wa wafanyakazi  na ili kumaliza tatizo hilo ni lazima watoto hasa wa kikke wasomeshwe.


Makamu huyo wa raisa amewataka wazazi na  viongozi kuhakikisha idadi ya wasichana  wasomi inaongezeka zaidi.

Amesema wanawake  si wepesi kuhama katika ajira kama ilivyo kwa wanaume.

Pamoja na mambo mengine  ametaka  kilimo cha mazao ya chakula na biashara hasa zao la muhogo kuimarishwa.
SONGEA
ASKARI polisi wa idara ya upelelezi wa makosa ya jinai wilayani Tunduru mkoani Ruvuma amefariki dunia na wengine saba akiwamo dereva wamejeruhiwa baada ya gari waliokuwa wakisafiria
kutoka mjini Tunduru kwenda kijiji cha Mbesa   kupinduka.

Kamanda Polisi wa mkoani humo, Michael Kamuhanda amesema ajali hiyo imetokea majira ya saa SAA NANE mchana na kwamba aliyefariki ni  Marry Mosha (31).


Amesema siku  ya tukio gari la polisi PT 0834 likiwa na askari polisi wanane likielekea kwenye kazi maalum kwenye kijiji cha Mbesa liliacha njia na kupinduka kufuatia stering road  kuchomoka.

Kamanda huyo amesema baada ya ajali askari polisi watatu  wamelazwa katika hospitali ya misheni iliyopo katika kijiji  hicho  na hali zao zinaendelea vizuri.

Mwili wa marehemu Marry umesafirishwa kwenda wilayani Moshi mkoani Kilimanjaro kwa maziko.

FEBRUARI, 2, 2012
KAHAMA
MKUU wa wilaya ya kahama, mkoani Shinyanga meja mstaafu  Bahati Matala amewataka  wakuu wa shule za sekondari za kata kuacha tabia ya kuwarudisha nyumbani wanafunzi wa kidato cha kwanza mwaka huu wanaoshindwa kukamilisha ada na michango mbalimbali.
Uamuzi wake huo unatokana na baadhi ya shule za sekondari kulalamikiwa na wazazi kuwa inawatoza michango zaidi ya laki moja kinyume na agizo la serikali.
Amesema pamoja na  shule kujijengea utaratibu wa kuboresha taaluma kwa wazazi kuchangia gharama kidogo lakini hawaruhusiwi kumrudisha nyumbani mwanafunzi aliyeshindwa kukamilisha michango hiyo.
Baadhi ya madai ya wazazi ni walimu  kuwalazimisha kulipa michango yote kwa mwaka mzima bila kujali uwezo wao ambapo  baadhi yao wamekubali kulipa kwa awamu.
DODOMA
ZAIDI ya familia 45 katika eneo la Chinyoyo mkoani  Dodoma, hazina mahali pa kuishi baada ya nyumba zao kuezuliwa na mvu iliyonyesha juzi iliyoambatana na upepo mkali.
Mwenyekiti wa mtaa wa Chinyoyo Yusufu Mkono amesema  hali za wananchi ni mbaya na kwamba familia hizo hazina chakula na makazi.  Amesema  misaada ya haraka inahitaji.
Mbunge wa jimbo la Dodoma Mjini Dk David Malole ameomba msaada serikalini  na mashirika mbalimbali kusaidia na ametoa msaada wa mifuko arobaini ya unga.
Pamoja na mambo mengine  ameishutumu  mamlaka ya ustawishaji makao makuu (CDA) kuwa imechangia kuufanya mtaa huo kuwa nyumba kimaendeleo kutokana na kukataa kuwapimia viwanja wananchi ili wajenge makazi bora.
ZANZIBAR
SERIKALI ya  Zanzibar imetakiwa kupata  kipimo cha DNA, ili kitumike kutoa ushahidi dhidi ya kesi mbalimbali.
Ushauri huo umetolewa na mrajisi wa mahakama kuu Zanzibar, Geroge Joseph Kazi, alipokuwa akizungumza na waandishi wa habari.
Amesema kipimo cha DNA ni muhimu katika ushahidi  na kwamba watuhumiwa wa makosa huachiliwa kutokana na kukosekana kwa ushahidi.
Mrajisi huyo amesema makosa mengi yanayofikishwa  mahakamani  yanahitaji ushahidi wa DNA lakini inashindikana kutokana na  kuwa na gharama kubwa.
Kuhusu wabakaji kupewa  dhamana, amesema mahakama inaendesha kesi  kwa mujibu wa sheria za nchi.
Amesema kama serikali inataka wasipewa dhamana ni vizuri sheria  ikafanyiwa mabadiliko  kwa mujibu wa taratibu.
Hivi karibuni, makamu wa pili za rais visiwani Zanzibar,  Balozi Iddi Seif alipendekeza   wabakaji wasipewe dhamana na kwamba tatizo hilo linazidi kuongezeka. 
Alisema wakati umefika kwa mahakama na jeshi la polisi kutotoa   dhamana kwa watu wanaotuhumiwa kufanya makosa ya vitendo vya udhalilishaji wa kijinsia ikiwemo kubaka.


KIBAHA
WATOTO  wawili wa familia moja wamefariki dunia papo hapo  baada ya  nyumba ya nyasi walimokuwamo kuteketea kwa moto. Waliofariki ni  Pili Miraji umri miaka  3, na Zena Miraji,  mwenye umri wa mwaka 1.
Kamanda wa polisi mkoani Pwani, ERNEST MANGU amesema tukio hilo limetokea majira
ya  SITA  mchana   katika kitongoji cha Akupendae.
Kamanda MANGU amesema chanzo cha tukio hilo ni moto uliokuwa umeachwa jikoni na  baba wa watoto hao, Miraji Rajab mwenye umri wa miaka 30 ambaye alitoka na mkewe kwenda shamba na kuacha moto huo, ulioshika  nyasi na kuteketeza watoto na vitu vyote vilivyokuwamo.
Katika tukio lingine, gari namba T 984 ASB Mitsubishi Fuso  likiendeshwa na Ally Juma akitokea Dar es Salaam kwenda Moshi iligongana uso kwa uso na gari namba T 850 APG Mitsubishi Fuso iliyokuwa inaendeshwa na George Yohana.
Ajali hiyo imetokea majira ya saa MBILI usiku katikati ya daraja la mto Wami ambapo madereva walijeruhiwa
Kamanda amesema chanzo cha ajali hiyo ni kufeli kwa breki  la gari lililokuwa likiendeshwa na Ally Juma.
MOROGORO
BARAZA la madiwani wa halmashauri  wilaya ya Ulanga, mkoani Morogoro limewaagiza watendaji   kufanya tathimini yakinifu ili kujua ukubwa wa ardhi inayoweza kutengwa kwa ajili ya uwekezaji .Pia baraza hilo limetaka kukomeshwa kwa vitendo vya rushwa vinavyotumika kugawa ardhi.
Agizo hilo limetolewa na  mwenyekiti  wa halmashauri  hiyo,  Furaha Lilongeli. Amesema tathimini  isipofanyika  na wananchi wasiposhirikishwa ipasavyo katika maamuzi ya ardhi, migogoro itaendelea.
Lilongeli amesema  ardhi ni rasilimali muhimu kwa kizazi kilichopo na cha  baadaye na kwamba ili itumike  kwa manufaa ya wote  ni muhimu wananchi  wakashirikishwa katika michakato mbalimbali.
Amesema hatua hiyo lazima ichukuliwe haraka kufuatia kuwapo kwa ongezeko  kubwa la mahitaji ya ardhi kwa ajili ya uwekezaji.
Mwenyekiti huyo  amesema hatua ya kuzishirikisha pande  mbili iende  sambamba na uingiaji mikataba yenye manufaa kwa pande zote.
Katika hatua nyingine  amewaagiza madiwani kufuata misingi ya utawala bora kwa kukaa vikao vya kisheria na kuitisha mikutano ya kusoma taarifa ya mapato na matumizi.
Amesema kufanyika kwa vikao kutasaidia kutatua migogoro ya mara kwa mara ikiwamo ya wananchi kutoshiriki katika shughuli za maendeleo.



FEBRUARI, 1, 2012
BUKOMBE
HATIMAYE wafanyabiashara wilayani Bukombe wameanza kujitolea fedha na mali kuondoa aibu ya kufungwa kwa shule ya msingi Butambala, Mtinga na Kakoyoyo kutokana na kukosa vyoo.

Mfanyabiashara Daniel Machongo amechangia nondo, Seleman Malale  amechangia  vifaa na fedha taslimu laki moja na viekabidhiwa  kwa  kamati ya shule Butambala.

Machongo amesema ni aibu kwa wanabukombe wote kwa shule kufungwa na wanafunzi kutosoma na kwamba hali hiyo inaonyesha jinsi wananchi wasivyojali elimu

Afisa elimu wa shule za msingi wilayani Bukombe Donard Mpanda amesema  zoezi la kuzifunga shule ambazo hazina vyoo linaendelea na kwamba shule ya msingi Ishigamva na Kiziba ambako walimu na wanafunzi hujisaidia vichakani, pia zitafungwa.

Wakati huo huo  kaimu mkuu wa wilaya ya Bukombe meja mstaafu  Bahati Matala amesema dawa ya viua wadudu wanaoshambulia zao la pamba, imepatikana.

Amesema wilaya ya Bukombe imepata jumla ya chupa 177,926 na chupa 73,926 zimegawiwa kwenye kampuni nne zilizoteuliwa kusambaza kwa wakulima wa vijiji vyote.

Kampuni hizo ni Kahama Oil Mill, KCCL, Fresho na Shirecu.
Amesema wakulima watauziwa kwa  sh 15,000 kwa chupa na si vinginevyo.

Pamoja na mambo mengine ameonya walanguzi watakaobainika kuwauzia dawa hizo wakulima kwa bei tofauti na hiyo na kwamba  hatua za kisheria zitachukuliwa dhidi yao.
xxxxxxxxxxxxxxx
DODOMA
SERIKALI imesema haitaweza kumnyang’anya shamba lililoko kijiji cha Mvomero mke wa waziri mkuu mstaafu, Ester Sumaye kwa kuwa alilinunua kihalali.

Kauli hiyo imetolewa  leo bungeni na naibu waziri wa ardhi,nyumba na maendeleo ya makazi,  Godluck Ole Medeye.

Amesema shamba hilo lenye ukubwa wa ekari 326 ni mali halali ya Ester Sumaye na alilinunua kwa hati namba 21919 kutoka kwa Onasaa Kisanga na Mesaki Ndashau waliokuwa wamiliki.
Alikuwa akijibu swali la mbunge wa Mvomero (CCM) Amos Makala ambaye alitaka kujua taratibu zilizotumika  kumuuzia shamba hilo badala ya kuwapa wananchi wa eneo hilo waliokuwa wakilihitaji.
Pia aliitaka serikali itoe tamko, kufuatia  madai kuwa rais Jakaya Kikwete aliahidi kulichukua shamba hilo  na kuwapa wananchi.
Waziri Ole Madeye amesema hata rais Kikwete  hawezi kulichukua kwa kuwa anaheshimu utawala wa kisheria.
Naibu Waziri huyo amesema  awali shamba hilo lilimilikiwa na Mvomero River Farmers Ltd ya Morogoro kuanzia mwaka 1978 hadi Julai 1985 lilipohamishiwa kwa Wami & Magole Farmers Cooperation Society Ltd.
Amesema mwaka 1996 kampuni hizo zilibadili jina na kuitwa Morogoro Farmers Primary Society Ltd na Novemba 27, 2001 walimuuzia Esther Sumaye ambaye alikamilisha taratibu zote ikiwamo  kulipa ushuru wa serikali kabla ya kupatiwa hati ya kumiliki.
xxxxxxxxxxxxxx
ARUSHA
MAHAKAMA  inayoendesha kesi za mauaji ya kimbari yaliyotokea Rwanda mwaka 1994 imetoa wito kwa mataifa kutoa hifadhi kwa wale waliofutiwa  mashtaka.

Watu 5 kati ya watu 10 waliofutiwa mashtaka ya kuhusishwa katika mauaji hayo wanasema hawawezi kurejea nchini Rwanda.

Wanaishi chini ya ulinzi wa polisi katika nyumba moja mjini Arusha, ambako ndiko makao ya mahakama hiyo ya ICTR.
Mahakama hiyo ya ICTR inatarajiwa kufungwa mwishoni mwa mwaka huu.

Watu 800,000 kutoka jamii ya watusi na wahutu wenye msimamo wa kadiri waliuwawa katika kipindi cha siku 100 nchini Rwanda mwaka 1994.

Msemaji wa ICTR, Roland Amoussouga amesema mahakama hiyo inakbiliwa na changamoto ya kuwahifadhi watu hao na kwamba ni mzigo mkubwa.

Amesema wameshirikiana nao kwa miaka mingi, pamoja na mawakili wao kutafuta nchi ambako wanaweza kupelekwa lakini hawajanafikiwa.

Wote 5 walioko mjini Arusha ni  wahutu na miongoni mwao ni afisa wa zamani wa jeshi wa cheo cha Brigadier generali, mawaziri wa zamani na mfanya biashara mmoja.

Wote wana familia nchini Ubelgiji, Canada na Ufaransa lakini hadi sasa hawawezi kupewa vibali kujiunga na familia zao, licha ya maombi kutoka baraza la usalama la umoja wa mataifa.

xxxxxxxxxxxxxxxxx
WAZIRI wa tawala za mikoa na serikali za mitaa(TAMISEMI) George Mkuchika amesema serikali ipo mbioni kukamilisha waraka utaosambazwa na waziri mkuu nchi nzima, utakaoelezea kuwa huu ni mwaka wa kumaliza tatizo la madawati kwa shule zote.
Pia  serikali imesema  bilioni  18.4 kutoka katika fedha zilizorudishwa za rada zitatumika kununulia madawati kwa shule za msingi na sekondani nchini.

Kauli hiyo imetolewa  na Naibu Waziri wa Tawala za mikoa na serikali za Mitaa (Elimu ), Kassim Majaliwa wakati akijibu swali la nyongeza kutoka kwa mbunge viti maalumu (CCM), Martha Mlata.

Mlata alitaka ufafanuzi ni kiasi gani cha fedha kilichotengwa kutokana na fedha za rada ambacho kitatumika kwa ajili kupunguza tatizo la madawati  kwa shule nyingi nchini.

Naibu Waziri amesema katika mwaka wa fedha wa 2009/10 serikali ilitoa bilioni 1 kwa  mamlaka za serikali za mitaa ili kununua  madawati kwa shule za sekondari na mwaka 2010/11 ilitoa  bilioni  3  kununua madawati kwa shule za msingi.

Amesema walimu wakuu wa shule wamepewa mamlaka ya kutumia fedha zinazotengwa  kwa ajili ya ukarabati, kufanya ukarabati wa madawati yanayoharibika.
Xxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxx
BAADHI ya wanafunzi wa shule ya sekondari Luegu wilayani Namtumbo mkoani Ruvuma wanaugua ugonjwa wa kuwashwa mwili na kupata  upele.

Wamesema tatizo hilo ni la muda mrefu na kila mwaka  hujitokeza na kwamba wanakosa kutibiwa kufuatia  zahanati ya kijiji  kuwa mbali.

Hali hiyo imepelekea wanaougua ugonjwa huo kushindwa kuhudhulia masomo na hata kushindwa kumudu kuelewa vizuri masomo wanayofundishwa.

Mwalimu mkuu  wa  sekondari  hiyo,  Menzeslaus Luoga   amesema  utafiti wa  haraka walioufanya ni kuwa ugonjwa huo unasabishwa na baadhi ya  majani  shuleni hapo ambayo yakiguswa husababisha muasho mwilini na kupelekea kupata upele.

Pamoja na mambo mengine amesema shule hiyo yenye jumla ya wanafunzi 524, wasichana 342 na wavulana 182, pia  inakabiliwa na tatizo la ugonjwa wa maralia na taifodi.

Kaimu afisa elimu wa shule za sekondari wilayani  Namtumb,  Lydia Helbert  uongozi wa halmashauri  hiyo unatafuta ufumbuzi wa tatizo hilo ikiwamo kuwahimiza wataalamu wa afya kutembelea kila wakati shuleni hapo.

Mwalimu mmoja amesema miaka ya nyuma, afisa afya wa kata ya Luegu alikuwa akifika kila mwaka na kutoa dawa kwa kila mwanafunzi  lakini ni takribani  miaka minne sasa dawa hizo  hazijafikishwa shuleni hapo.


JANUARI 31, 2012
DODOMA
SPIKA wa Bunge Anne Makinda, amethibitisha kwa wabunge kuanza kulipwa posho mpya ya LAKI MBILI kwa kila kikao katika Bunge lililopita baada ya Rais Jakaya Kikwete kutoa kibali.
Amethibitisha hay oleo alipokuwa akizungumza na waandishi wa habari ofisini kwake mara baada ya kipindicha maswali na majibu. Amesema si kwamba wataanza kutoa, ila  zimeshanzwa kutolewa.
Makinda amesema posho hiyo iko katika waraka wa serikali  uliotolewa Julai mwaka juzi ambapo wenyeviti wanapata sh 200,000, wajumbe ni sh 150,000 na  wengine 100,000.
Kitendo cha kuongezeka kwa posho za wabunge kinaitia katika wakati mgumu serikali ya awamu ya nne kutokana na kelele nyingi zinazopigwa na wanachi pamoja na wanaharakati.
Pamoja na mambo mengine Spika Makinda amesema ni jambo la kawaida kwa wananchi kuhoji uhalali wa posho za wabunge wakati mishahara na posho ya watendaji  wengine haihojiwi.
Amesema baadhi ya wabunge wamekuwa wakikopa  hadi mafuta ya  gari ya kwenda  bungeni na kwamba si matajiri kama baadhi ya watu wanavyofikiri na kwamba wengine  hufariki dunia muda mfupi baada ya kumaliza kipindi chao cha ubunge kutokana na ugumu wa maisha.
Spika huyo amesema hali hiyo inatia uchungu na kwamba hawana la kufanya kuhusiana jambo hilo na badala yake wanafanya kazi ya kujiimarisha na kuvumilia katika ugumu wa maisha.
DODOMA
WAZIRI wa fedha na uchumi Mustafa  Mkulo amemgomea spika wa bunge Anne Makinda baada ya kukataa kujibu swali alilotakiwa na spika huyo kuhusu fedha za cheji ya rada.
Mkulo aliitwa zaidi ya mara nne akitakiwa kujibu swali na spika na yeye kushindwa kusimama na kuonyesha kutojali kitu kitendo kilichoonyesha mshangao hata kwa wabunge.
Kitendo cha Mkulo kukataa kusimama kilitokana na swali lililoulizwa na Mbunge wa Viti Maalumu Mkoa wa Singida Martha Mlata (CCM) ambaye alitaka kujua kama fedha za rada zingetumika kwa ajili ya kununua madawati ya wanafunzi mashuleni.
Mlata alisimama na kuuliza swali la nyongeza katika swali la msingi namba mbili lililoulizwa na Vicent Nyerere (Musoma Mjini Chadema) ambaye alitaka kujua serikali imejipanga vipi kuhusu suala la madawati.
Swali hilo lilijibiwa na Naibu Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa (Elimu) Kassim Majaliwa lakini ghafla liliibuka swali la Mlata lililogusa fedha za rada.
Wakati wote ambao Makinda alikuwa akimtaka Mukulo kusimama na kutoa majibu, Waziri huyo alikuwa akiteta jambo na Waziri wa Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa, George Mkuchika ambaye alisimama pia kutaka kutoa majibu lakini Makinda alimzuia kabla ya kumruhusu kwa mara nyingine kutolea ufafanuzi jambo hilo.
Baada ya kuona hali hiyo, Majaliwa alilazimika kusimama na kusogelea kipaza sauti na kulieza bunge kuwa zaidi ya Sh 18 bilioni zitapelekwa huko kwa ajili ya kununulia madawati.
Makinda alishawahi kutangaza bungeni kuwa Mawaziri wanatakiwa kuwa makini kwa kila swali au jibu linalotolewa ndani ya ukumbi kwani wakati wowote yeye anaweza kumtaka mtu ajibu swali au kutoa ufafanuzi.
PWANI
WAJASILIAMALI nchini wametakiwa kutumia ujuzi wao kutengeneza bidhaa zenye ubora kulingana matakwa ya wateja ili  kupata soko la uhakika na kujiongezea kipato.
Wito huo umetolewa mkoani Pwani na meneja wa mpango wa kuendeleza biashara nchini, MARCO VINGILAH na kwamba wasitegemee  taasisi za fedha na mabenki kujiimalisha.
Amesema ujuzi ni mtaji mkubwa na muhimu kuliko fedha na walioutumia ipasavyo  ujuzi wamefanikiwa.
VINGILAH amesema fedha ni njia ya kufikia lengo la biashara lakini si  chanzo cha mafanikio  katika  biashara.
Amewataka wajasiliamali kujenga tabia ya kujitegemea kuliko kusubiria mikopo kutoka taasisi mbalimbali za fedha.
Kuhusu shindano la mpango wa kuendeleza biashara nchini amesema washiriki 1148 wamepatikana kufuatia mchujo  wa kwanza uliokuwa na washiriki 1350 na kwamba  washiriki 900 ndio watakuwa washindi.
ZANZIBAR
TUME ya uchaguzi Zanzibar imetupilia mbali rufaa iliyowasilishwa na wagombea wa chama cha CUF na CHADEMA ya kumuwekea pingamizi la kugombea, mgombea wa CCM Mohammed Raza katika uchaguzi mdogo wa jimbo la Uzini.
Uchaguzi  huo utakaofanyika  Februari 12, mwaka  ni kufuatia  kifo cha aliyekuwa mwakilishi wa jimbo hilo Mussa Khamis Silima, aliyefariki kwa ajali mkoani Dodoma mwaka jana.
Afisa  habari wa tume ya uchaguzi Zanzibar(ZEC) Idrissa Haji Jecha  ameiambia REDIO KAHAMA FM kuwa  baada ya ZEC  kusikiliza malalamiko ya pande zote imekubaliana  na uamuzi uliotolewa na msimamizi wa uchaguzi jimbo  hilo, kuwa Raza  ashiriki katika uchaguzi huo
Hata hivyo Jecha amesema suala la malipo ya fomu halikufika katika afisi ya tume na kilichoangaliwa zaidi ni kama  taratibu za uchukuaji  fomu  na  kiapo cha mgombea, ulifuatwa kikamilifu na kwa mujibu wa sheria.
Amesema kasoro zilizowekwa na  mgombea wa CUF , na wa CHADEMA ni za kisiasa tu..
Raza aliwekewa pingamizi na vyama vya CHADEMA na CUF wakidai amekiuka taratibu za uchaguzi ikiwamo kifungu cha 46 cha uchaguzi (4) kinachotaka mgombea kula kiapo mbele ya hakimu wa mkoa  na  fomu yake iwe na muhuri wa hakimu wa mkoa na kwamba fomu ya Raza haikuwa na  muhuli wa malipo.
Fomu ya uchaguzi ya Raza ilijazwa na hakimu wa mahakama kuu, ambapo mkuu wa uchaguzi alisema hayo si makosa ambayo yanaweza kumuengua Raza katika kinyanganyiro hicho.
Kampeni cha uchaguzi huo zimeanza rasmi Jumamosi iliyopita JANUARI 30, 2012
BUKOMBE
AFISA elimu wa shule za msingi wilayani Bukombe, mkoani Shinyanga, DONARD MPANDA amezifunga shule tatu  za msingi kwa kukosa vyoo.

Shule hizo ni shule ya msingi Butambara, Mtinga na Kakoyoyo.

Hatua hiyo  imefuatia baada ya wazazi kukataa kutoa michango ya ujenzi wa vyoo hivyo.

Imedaiwa kuwa wengi wa wananchi wamekataa kutoa michango hiyo kufuatia kukatazwa kufanya hivyo katika kampeni za uchaguzi uliopita.

Afisa elimu huyo amesema waliofungiwa ni wanafunzi kuanzia darasa la kwanza hadi la sita na kwamba wanafunzi wa darasa la saba wataendelea na masomo.

Pamoja na mambo mengine diwani wa kata hiyo, SOUD NTANYAGALA amewaomba  wazazi kuchangia ujenzi huo ili kunusuru hatma ya elimu ya watoto wao.
SHINYANGA
WANANCHI wameaswa kuwa makini katika kuchagua viongozi hali itakayosaidia kuondoa migogoro isiyokuwa ya lazima ambayo  ni kikwazo cha maendeleo nchini.

Wito huo umetolewa mkoani Shinyanga Waziri mkuu mstaafu, Edward Lowassa  katika harambee ya kuchangia ujenzi wa Kanisa kuu la Kiinjili ya Kilutheri Tanzania(KKKT) Dayosisi ya mashariki ya Ziwa Victoria.

Amesema kujengwa kwa kanisa hilo kutasaidia kumpata askofu mkuu wa kanisa hilo na kuwataahadharisha katika uchaguzi wa kumpata lazima busara itumike katika kumpata kiongozi huyo.

Awali akitoa taarifa fupi mchungaji Philbert Celestine amesema  kuanzishwa kwa dayosisi mpya ya Shinyanga na mkoa mpya wa Simiyu kutasaidia kuleta maendeleo katika mikoa hiyo.
Katika harambee  hiyo jumla ya  milioni 204 zilipatikana   huku fedha  taslimu ni milioni 116 ambapo Lowasa alichangia milioni 21  taslimu kama mchango wake yeye na familia yake.
MBEYA
BAADHI ya wazazi na walezi wameiomba serikali kuangalia uwezekano wa kupunguza michango holela shuleni.
Wamesema  michango holela  inachangia kwa kiasi kikubwa wananfunzi wengi wakiwamo baadhi ya waliofaulu kujiunga kidato cha kwanza kushindwa kuendelea na masomo.
Wakizungumza na REDIO KAHAMA FM kwa nyakati tofauti mkoani Mbeya wamesema mazingira ya kupta fedha ni magumu na kwamba hata wakiipata, fedha hiyo haina thamani hivyo inawawia vigumu kuchangia michango shuleni.
Fatuma Idd  amesema  wanatambua jitihada za serikali  katika kuhakikisha kila mtoto anapata elimu ya msingi na sekondari  lakini wingi wa michango ndio  kikwazo katika kufanikisha mipango hiyo
Hata hivyo mkuu wa wilaya ya Mbeya, Evance Balama amesema serikali haina taarifa ya kuwapo kwa michango  holela shuleni na ameomba kufichuliwa kwa walimu wanaoshinikiza michango hiyo.
Amesema anachojua ni kuwa serikali  imeidhinisha michango ya madawati na mingine ambayo haiwezi kuathiri uchumi wa wazazi.
ZANZIBAR
SERIKALI ya Zanzibar imetakiwa kuangalia  upya suala la mikopo kwa wanafunzi wa elimu ya juu.
Wito huo umetolewa  na wahitimu wa chuo kikuu cha elimu Chukwani na kwamba mfumo wa mikopo uliopo ni tatizo linalowakosesha utulivu katika kujipatia taaluma.
Muhitimu, Mohammed Ngarima amesema upatikanaji wa mikopo umekuwa kikwazo kwa wanafunzi na ameitaka serikali kuuboresha.
Mkuu wa chuo  hicho Dk  Lezzedin Abdullrahman amesema wamejipanga kuongeza kiwango na ubora wa taalum.
 Akizungumza katika mahafali hayo Makamu wa pili wa rais  Zanzibar,  Balozi Seif Ali Iddi amewataka wahitimu hao kukabiliana na changamoto ya upatikanaji wa ajira.
Amewata kutumia busara na maarifa katika kukabiliana na changamoto  hiyo na kwamba serikali inaendelea na juhudi mbalimbali za kubuni mbinu za ajira ili kupunguza wimbi tatizo hilo.
Jumla ya wahitimu  219 wamehitimu  katika ngazi ya Shahada ambapo 83 ni wa fani ya Kiarabu, 30 fani ya Sayansi na 106 wa fani ya Jamii.
JANUARI 29, 2012

SHINYANGA
WAZIRI mkuu mstaafu,  EDWARD LOWASA  hii leo amechangisha jumla ya  million 204 katika kanisa la KKKT  la mkoani Shinyanga ambapo yeye na familia yake wamechangia  milioni 21.

Pamoja na mambo mengine ametaka fedha hizo zisaidie  kujenga kanisa ili waumini waswali katika mazingira mazuri pamoja na kuiombea nchi amani ya kudumu.

Amesema kwa sasa nyumba za ibada zinajengwa na wananchi wenyewe tofauti na miaka ya nyuma,ambapo zilijengwa kwa misaada kutoka nje ya nchi.

Askofu wa kanisa hilo Andrew Petro Gulle amesema baraka za MUNGU  zinatoweka  kufuatia  watu kushindwa kumtolea mungu.

Naye kaimu katibu mkuu wa kanisa hilo Philibert Celestin amesema lengo la harambee hiyo ilikuwa ni kupata milion 114  na kwamba wamekwisha tumia milioni 135 katika ujenzi wa kanisa hilo 

Katika harambee hiyo wakuu wote wa wilaya mkoani Shinyanga, mbunge wa jimbo la shinyanga mjini, Steven Masele, baadhi ya wafanyabiashara kutoka  wilayani  Bariadi, Nzega na mkoani mwanza walihudhulia

SHINYANGA
SERIKALI imetakiwa kutoa elimu ya uraia ipasavyo kwa wananchi ili wajue haki zao ikiwamo ya  kuchagua kiongozi atakayeleta  maendeleo na si mtoa rushwa.

Hayo yamesemwa  katika mdahalo uliofanyika wilayani Kishapu mkoani Shinyanga, uliandaliwa na mashirika yasiyo ya kiserikali Shingonet, uliokuwa unahusu wajibu wa viongozi kwa wananchi na wananchi kwa viongozi.

Pamoja na mambo mengine wamesema hawana elimu ya kuweza kuchagua viongozi wanaofaa na kwamba wanachagua pasipo kuangalia vigezo vya kiongozi bora na mzalendo.
Wamesema katika chaguzi nyingi wapiga kura wamekuwa  wakipewa rushwa ili kuchagua wagombea katika nafasi zote.
Wamesema baada ya kuwachagua, viongozi   huwapotosha katika masuala mbalimbali na kujinufaisha wenyewe bila kuleta maendeleo.

MOROGORO
HALMASHAURI ya wilaya ya Mvomero mkoani morogoro imewaonya watendaji wa kata wanaozembea kazi ikiwamo kushindwa kukusanya mapato  kuwa itawachukulia hatua  za kinidhamu ikiwamo kuwafukuza kazi.

Onyo hilo limetolewa na mwenyekiti wa halmashauri hiyo,Jonas Zeland katika kikao cha kamati ya ushauri ya wilaya hiyo.

Amesema ufinyu wa mapato unatokana na watendaji kushindwa kusimamia makusanyo katika kata zao.

Zeland amesema mpango mkakati wa halmashauri hiyo ni  kusimamia na kukusanya ipasavyo mapato katika kila kata ili kufanikisha mipango ya maendeleo ya wananchi.

Amesema ufinyu wa ukusaji mapato umesababisha mipango  mingi ya  maendeleo ikiwamo ujenzi wa miundombinu mbalimbali kama ya barabara, kukwama.

Hata hivyo baadhi ya wajumbe wamesema ili kufanikisha mipango ya halmashauri ni lazima watendaji waboreshewe  vitendea kazi  ikiwamo kupewa pikipiki

Pia wameitaka halmashauri hiyo kubuni vyanzo vingine vya mapato na kuachana na kutegemea fedha za ushuru wa mazao pekee.

KISARAWE
ASKARI mgambo wametakiwa kutotumia mbinu mbali mbali za kijeshi walizojifunza,  kwa kufanya  vitendo vya uhalifu
Wito huo umetolewa na mkuu wa wilaya ya kisarawe mkoani Pwani Hanifa Karamagi na kwamba  mgambo watumie mbinu hizo  kuleta mabadiliko  chanya katika jamii ili wawe mfano wa kuigwa

Amesema  hivi sasa kumekuwapo  na changamoto nyingi ikiwamo ya wizi na rushwa  hivyo kama mgambo watatumia fursa waliyonayo wataweza  kukomesha maovu katika jamii

Karamagi amezita   halmashauri na wadau wengine kuwapa ajira na mgambo na kuwatumia  katika kufichua maovu kwa kushirikina na polisi ili kukomesha vitendo viovu na kushiriki kikamilifu katika kazi za maendeleo

Pia amesema mgambo wakitumika vyema ni msaada mkubwa katika kulinda maliasili za nchi.

Pamoja na mambo mengine amewataka askari mgambo kuunda  vikundi na kuanzisha  miradi ya maendeleo ili kujiinua kiuchumi  na si kutegemea kuajiriwa tu.

JANUARI 28, 2012
KAHAMA
MGOGORO wa uongozi katika chama cha Demokrasia na maendeleo CHADEMA wilayani kahama bado unaendelea kufukuta.

Hatua hiyo inafuatia baada ya ofisi ya chama hicho iliyopo Nyasubi kufungwa kufuatia viongozi wa wilaya wa chama hicho, kutoitambua.
Mwenyekiti wa CHADEMA wilayani Kahama Juma Protas amesema wamechukua uamuzi huo kutokana na kutowatambua viongozi wa chadema jimbo la kahama kufuatia kufukuzwa uanachama.
Amesema watu hao ambao wanajiita viongozi wamekuwa wakitumia nembo ya chama hicho kinyume cha utaratibu.
Naye mwenyekiti wa CHADEMA jimbo la Kahama, Charles Lubala amelaani kitendo  hicho na kwamba  ofisi hiyo ilifungwa baada ya wao kuondoka muda wa mchana jana.
Mjumbe wa kamati tendaji ya  chama hicho jimbo la Kahama, William Machimu amesikitishwa na kitendo hicho, akisema   ni ukiukwaji wa misingi ya haki na utawala wa sheria.
Kamanda wa polisi mkoani Shinyanga Diwani Athuman amesema polisi waliambatana na  viongozi wa CHADEMA wilayani  Kahama, kufuatia kuwasililisha  vielelezo kupinga uhalali wa uwepo wa ofisi hiyo ya Nyasubi na kuomba msaada wa kuifunga.
Pamoja na mambo mengine Kamanda Diwani amezitaka pande mbili hizo zenye mgogoro kufikisha matatizo yao ngazi ya juu ya chama ili kupatiwa ufumbuzi.
SHINYANGA
WAUMINI wa dini ya kiislamu katika kata ya Kitangiri manispaa ya Shinyanga wamejikuta katika wakati mgumu kufuatia kuwakuta nguruwe wawili ndani ya msikiti na kutaka kuwauwa  kwa moto.
Wakizungumza kwa hasira  waumini hao katika eneo la msikiti wa Kitangiri “B”  wamesema nguruwe hao wamechafua kwa kinyesi sehemu ya kuswalia ndani ya msikiti
Imamu wa msikiti huo Sheikh Hamad Kanyuguta amesema uongozi wa msikiti ulilazimika kufanya kazi ya ziada  kuwazuia waislamu wasichukue sheria mkononi.
Amesema baada ya kupata taarifa za kuingia msikitini kwa nguruwe hao aliwasiliana na mwenyekiti wa mtaa,  Gabriel Swila pamoja na diwani wa kata ya Kitangiri,  George Kitalama ambao walifika katika eneo la tukio na kushuhudia wenyewe nguruwe hao wakiwa wamefungwa kamba nje ya msikiti huo.
 Muumini Juma  Abdalah amesema   hivi karibuni walimfikisha  mahakamani mfugaji wa nguruwe hao, Richard Maige na kuhukumiwa   kifungo cha nje cha miezi tisa.
Jeshi la polisi mkoani Shinyanga limethibitisha kutokea kwa tukio hilo na nguruwe hao wamekamatwa na kufikishwa katika kituo cha polisi mjini Shinyanga.
Hata hivyo mkuu wa upelelezi mkoani Shinyanga,  Hussein Kashindye amesema uchunguzi wa awali umebaini nguruwe hao walikuwa wamechimba shimo na kulala kandokando ya msikiti huo.
RUVUMA
MADIWANI mkoani Ruvuma wametakiwa kutumia madaraka yao kuhakikisha wananchi walengwa wananufaika na mgao wa pembejeo za ruzuku kwa njia ya vocha zinazotolewa na serikali zinafika kwa wakati na hakutokei udanganyifu.
Agizo hilo limetolewa na mkuu wa mkoa  huo,  Said Mwambungu katika kikao cha kawaida cha baraza la madiwani wa halmashauri hiyo.
Amesema madiwani ndio wenyeviti wa kamati za maendeleo za kata hivyo ni muhimu wakashirikiana na serikali katika kuhakikisha walengwa wanapata  pembejero za ruzuku za kilimo kwa taratibu zilizowekwa.
Mkuu huyo wa mkoa amesema serikali haitamwachia yeyote atakayekwenda kinyume na zoezi la vocha za pembejeo na kwamba  zinapaswa kutumika ipasavyo ili kuongeza uzalishaji wa mazao na kujihakikishia uhakika wa chakula.
Katika msimu huu wa kilimo mkoani Ruvuma zaidi ya wakulima laki moja na tisini watanufaika na pembejeo za ruzuku za kilimo zikiwamo mbegu bora za mahindi, mpunga, mbolea ya kupandia na kukuzia
Katika hatua nyingine, Mwambungu  amewataka madiwani wa halmashauri ya Tunduru kuhamasisha wakulima kuzalisha zao la mpunga ambalo linastawi kwa wingi wilayani humo ili liwe zao mbadala la biashara badala ya kutegemea korosho pekee.
KOROGWE,
ASKARI wawili wa jeshi la polisi waliokuwa katika msafara wa makamo wa rais, Dk Mohamed Ghalib Bilal wamefariki dunia kwa ajali na wengine wanne wamejeruhiwa.           

Ajali  hiyo imetokea jana baada ya gari lililokuwa limebeba askari hao  wa kikosi cha kutuliza ghasia kupinduka katika eneo lenye mteremko mkali la Nduru-Mombo wilaya Korogwe mkoani Tanga.

Mganga mkuu wa kituo cha afya cha Magungu Dk RASHID SAID amethibitisha kufariki kwa askari hao na kwamba hali za askari wanne waliojeruhiwa katika ajali hiyo inaendelea  nzuri.
          
Msafara huo ulikuwa unatokea wilayani Lushoto kwenda hale wilayani Korogwe kwa ajili ya mapumziko ya makamu wa rais ambaye yupo mkoani Tanga kwa  ziara ya kikazi.
          
Gari lililohusika katika ajali hiyo ni lenye namba za usajili PT-2000 ambalo lilikuwa nyuma ya msafara huo wa makamu wa rais.
          
Miili ya askari waliokufa imehifadhiwa katika kituo cha afya cha Magungu.

JANUARI 27, 2012
GEITA
MBUNGE wa jimbo la Nyangw’ale, mkoani  Geita, Ahmed Amar ameahidi kuwalipia ada wanafunzi 300 waishio katika mazingira magumu wakiwamo yatima ambao wamechaguliwa kujiunga  kidato cha kwanza.

Pia ametoa milioni 46 kwa kata kumi na mbili zilizopo katika jimbo hilo kwa ajili ya utekelezaji wa miradi ya maendeleo katika sekta ya elimu na afya.

Ameyasema  hayo katika mikutano ya hadhara iliyofanyika kwa nyakati tofauti katika kata za Nyugwa,Kharumwa, Mwingiro, Busolwa, Kakora, Nyabulanda na Izunya.
Amesema ada hiyo italipwa kwa kuzingatia vigezo na sifa za kukidhi kulipiwa ada ili kuepuka uchakachuaji. Mbunge huyo amesema kila kata itatoa wanafunzi 25.

Amefikia uamuzi huo baada ya wananchi kudai wanafunzi waliofaulu kutoka familia maskini  na yatima wapo hatarini kutojiunga na masomo ya sekondari kutokana na kukosa ada.
Pia ametoa  msaada wa mifuko 1,110 ya saruji, mabati na kompyuta kwa ajili ya shule za sekondari na amewataka wadau wakiwamo wananchi kujenga utamaduni wa kuwekeza na kuchangia elimu.
PWANI
SERIKALI imewaagiza maafisa elimu kote nchini kuhakikisha  usaili kwa wanafunzi wa kidato cha kwanza unafanyika, wa kama wanajua kusoma ua la.

Akizungumza mkoani Pwani hii leo, Waziri wa elimu na mafunzo stadi, Dk Shukuru Kawambwa amesema hilo ni agizo rasmi la serikali.

Amesema ni lazima maafisa elimu wote wahakikishe wanapata miongozo kutoka wizarani ya jinsi ya kusimamia zoezi hilo.

Waziri Kawambwa amesema ni lazima kila mwanafunzi aliyefaulu kuingia kidato cha kwanza afanyiwe usaili huo.

Pamoja na mambo mengine amesema usaili huo utasimamiwa na walimu wakuu wa shule husika na kwamba mwanafunzi atakayebainika kutojua kusoma ua kuandika, atarejeshwa nyumbani.

DAR ES SALAAM
ZAO la pamba nchini linakabiliwa na changamoto nyingi ikiwamo ya uhaba wa maafisa ugani katika maeneo ya vijijini na kupelekea wakulima wa zao hilo kushindwa kutumia mbinu bora za kilimo
Hayo yamesemwa na  mkurugenzi wa bodi ya pamba, Marko Mtunga alipokuwa akiongea na wadau wa zao  hilo kutoka Afrika.
Amesema changamoto hiyo ni mojawapo ya baadhi ya wakulima kushindwa kuzalisha zao hilo kwa wingi na kwamba kwa heka wanazalisha kilo 300 huku kitaalamu wanatakiwa kuzalisha kilo 1000.

Naye Mkurugenzi wa shirika la viwango nchini(TBS) Charles Ekelege amesema kuwa ili zao la pamba liwe na ubora wa kimataifa, wakulima wanapswa kutumia na kufuata utaratibu na kuhakikisha wanatumia maabara za upimaji wa zao hilo

Katika hatua nyingine, Ekelege amewataka  watanzania kuweka utaratibu wa kupima  na kutoa ubora wa mazao yao kabla ya kuingiza sokoni hali ambayo itachangia kwa kiwango kikubwa kukuza uchumi wao na wa nchi kwa ujumla.

DAR ES SALAAM
SERIKALI ya Sudan Kaskazini imesema ipo tayari kuleta madaktari ili wasaidie kutoa mafunzo kwa madaktari wa Tanzania hasa kwenye fani ya upasuaji wa moyo.

Hayo yamesemwa leo na balozi wa Sudan nchini Dk  Yassir Ali alipokuwa akizungumza na waziri mkuu Mizengo Pinda ofisini kwake magogoni, jijini Dar es Salaam.

Balozi huyo amemweleza waziri mkuu kuwa wameanza  mazungumzo na wizara ya afya na ustawi wa jamii ili kuona utekelezaji wa suala hilo.

Pia amesema wanaangalia uwezekano wa kutoa mafunzo kwa wataalamu wa tanzania kwenye eneo la uzalishaji nishati na umeme.

Kwa upande wake, waziri mkuu alimshukuru balozi huyo na kumuahidi kufuatilia suala la uanzishwaji wa tume ya pamoja ya ushirikiano  ili maamuzi yanayofikiwa yaweze kuwa na mfumo maalum wa ufuatiliaji.

Aliiomba nchi hiyo iisaidie Tanzania kufundisha pia wataalamu wa kilimo cha umwagiliaji maji kama njia ya kuinua uzalishaji wa mazao nchini.
Wakati huo huo mapema hii  leo, waziri mkuu alikutana na balozi mpya wa Japan nchini, Masaki Okada na kujadiliana naye masuala mbalimbali yakiwamo ya uendelezaji kilimo, miundombinu na miradi ya maji.

Na ameishukuru  serikali ya Japan kwa misaada ambayo imeipatia tanzania kwa kipindi chote cha ushirikiano baina ya nchi hizi mbili.
ZANZIBAR
SERIKALI  imetakiwa kuzisaidia asasi za kiraia zitazotoa elimu ya uraia kuhusu katiba na kuhamasisha jamii kujitokeza kutoa maoni katika mchakato wa uundwaji wa katiba mpya.
Wito huo umetolewa na mjumbe wa baraza la katiba Zanzibar ambaye pia ni mwanasheria wa kujitegemea, Awadh Ali Said alipokuwa akizungumza na waandishi wa habari kuhusiana na maoni ya baraza hilo katika  sheria ya mabadiliko ya katiba namba 8 ya mwaka 2011
Amesema serikali ikisaidia katika suala hilo, itachangia kwa kiasi kikubwa  wananchi kufanya maamuzi sahihi katika utoaji wa maoni yao.
Mwanasheria huyo amesema wananchi wanapaswa kushirikishwa ipasavyo  katika mchakato wa upatikanaji wa katiba mpya ili waikubali na kuiridhia.

Pamoja na mambo mengine ametaka kuwapo kwa  mjadala wa kitaifa kuhusu  sheria hiyo ili kujenga mwafaka wa kitaifa na kwamba bunge maalum la katiba lisiendeshwe kwa utashi wa kisiasa na liwe kwa maslahi ya taifa.

Kuhusu muundo wa tume ya kuratibu upatikanaji wa maoni ya wananchi,  Awadh amesema uteuzi wa wajumbe wake udhibitishwe  na  baraza la wawakilishi au Bunge ili kuondoa hofu.
Pia amependekeza wajumbe wa tume hiyo waendelee kubaki katika bunge maalum hata baada ya mwenyekiti wake kuwasilisha rasimu ya katiba katika Bunge hilo ili waweze kutimiza wajibu wa kutoa ufafanuzi pale itakapostahiki


JANUARI 26, 2012
DAR ES SALAAM
SERIKALI imewataka madaktari wote nchini walio kwenye mgomo kurejea katika vituo vyao vya kazi na kufanya kazi za utabibu ili kuokoa maisha ya wagonjwa.
Akizungumza na waandishi wa habari hii leo jijini Dar es salaam waziri wa afya na ustawi wa Jamii, Dk Haji Mponda amesema serikali inatambua mchango wa wataalam wa afya katika utoaji wa huduma za afya na inaendelea kuboresha maslahi yao.
Amesema madaktari kupitia chama chao (MAT) wamewasilisha madai mbalimbali serikalini ikiwamo nyongeza ya posho ya kuitwa kazini baada ya kazi na madaktari kupewa nyumba za kuishi karibu na hospitali.
Katika hilo amesema serikali imepata fedha kutoka mfuko wa dunia kwa ajili ya kujenga nyumba za madaktari na kwa kuanzia wilaya 18 zilizo pembezoni zimechaguliwa kujengewa nyumba 8 kila wilaya kama hatua ya kuboresha upatikanaji wa nyumba
kuhusu madai ya kutaka nyongeza za mishahara ya shilingi milioni 3.5 kwa mwezi waziri  Mponda amesema mishahara ya watumishi serikalini hufuata miundo ya utumishi iliyopo na kwamba  muundo wa malipo ya watumishi wa umma katika sekta ya afya umeboreshwa.
KAHAMA
MGANGA mkuu wa hospitali ya wilaya ya kahama Dk Leonard Subi amesema unyanyapaa kwa watu wanaoishi na virusi vya VVU ni mojawapo ya sababu  inayozolotesha mapambano ya ugonjwa wa ukimwi wilayani  humo.

Pia amesema hali hiyo inachangia kwa kiasi kikubwa ongezeko la maambukizi ya virusi vya ukimwi  wilayani humo ambayo yamefikia asilimia 9.3
Ameyasema hayo alipokuwa akifungua mafunzo ya siku kumi ya kuwajengea uwezo watoa huduma kwa wagonjwa wa ukimwi majumbani  kutoka katika  kata na vijiji
Amesema unyanyapaa kwa watu wanaoishi na VVU imekuwa ni tatizo linalowafanya  wasijitokeza kupima afya zao
Dk Subi ametaja sababu nyingine  ni wataalamu kutotunza siri za watu waliobainika kupata maambukizi.
Amesema wilaya ya kahama ina jumla ya watu 14,000 iliyowasajili  kuwa wanaishi na VVU lakini wanaojitokeza kutumia  dawa ya ARVs ni 7500 kwa sababu ya unyanyapaa.
Hivyo amewataka  waelimishaji hao kutoa elimu ipasavyo ya umuhimu wa kupima afya na kuondokana na tabia ya kuogopa kupima na kutumia dawa.
DODOMA
SERIKALI imetangaza kumfukuza  shule mwanafunzi  yeyote atayekutwa na simu ya mkononi shuleni.
Uamuzi huo umetangazwa hii leo mkoani Dodoma na   naibu  waziri wa nchi ofisi ya waziri mkuu (TAMISEMI), Kassimu Majaliwa.
Amesema uamuzi huo, umefikiwa ili kudhibiti nidhamu za wanafunzi wawapo shuleni.
Waziri Majaliwa amesema matumizi ya simu kwa wanafunzi wawapo shuleni unaathiri kwa kiasi kikubwa mwenendo wao wa masomo.
Amesema wengi wao wanapokuwa na simu  hizo shuleni hufanya mawasiliano mbalimbali na watu walio nje ya shule na kwamba kwa kiasi kikubwa inaathiri utulivu na umakini wawapo darasani.
Hivyo amewataka wanafunzi kutokwenda shuleni na simu hizo za mkononi.

MVOMERO
SERIKALI wilayani Mvomero, mkoani Morogoro, imeliagiza    baraza la madiwani wa halmashauri  hiyo  kuikagua miradi  iliyoshindwa kumalizika tangu mwaka 2006 ili kujiridhisha kama inaendana na thamani halisi ya fedha zilizotolewa.
Agizo hilo limetolewa na kaimu mkuu wa wilaya ya Mvomero, Halima Dendego katika kikao cha kamati ya ushauri ya wilaya hiyo na kuudhuliwa na viongozi mbalimbali wakiwamo wa vyama vya siasa .
Dendego, ambaye  ni mkuu wa wilaya ya Kilosa amefikia uamuzi huo kufuatia kutoridhishwa na taarifa ya utekelezaji wa miradi ya maendeleo  katika sekta ya kilimo ambayo mingi ilikuwa haijakamilika.
Miradi iliyotiliwa shaka ni  uchimbaji wa lambo katika kata ya Mvomero ulitolewa fedha zake tangu mwaka 2006/07, ujenzi wa soko la Makayu tangu 2007/08, ujenzi wa soko katika kata ya Mlali  na miradi mingine.
Licha ya fedha ya miradi hiyo  kutolewa katika kipindi hicho lakini hadi sasa haijakamilika na inahitaji  kuongezewa fedha ili kukamilika.
Baada ya kupitia taarifa zake wajumbe wa kikao hicho walihoji kwanini imeshindwa kukamilika wakati ilishatengewa fedha katika kipindi hicho .
ZANZIBAR
WIZARA ya biashara, viwanda na masoko  visiwani Zanzibar ina mpango wa kufanya utafiti utakaosaidia kufufua viwanda vya serikali na kuanzisha viwanda vipya kulingana na raslimali zilizopo.
Naibu waziri wa wizara hiyo Thuwaiba Kisasi, amesema  utafiti huo utalenga kujua chanzo cha kufa viwanda vya zamani na jinsi ya kivianzisha na kuwa endelevu.
Hata hivyo amesema viwanda vingi vilikufa kutokana na ukosefu wa raslimali, taaluma na kuajiri idadi kubwa ya wafanyakazi
Wakati huo huo, serikali ya Zanzibar imesema hakuna uwiano wa kutosha wa nafasi  za kazi kwenye ofisi za kibalozi nje ya nchi kati ya vijana wa Zanzibar na Tanzania bara.
Waziri wa nchi ofisi ya makamu wa pili wa rais Mohammed Aboud amesema tatizo hilo ni moja ya kero za muungano zinazoshughulikiwa ili wanzanibari waweze kuajiriwa katika ofisi hizo.
Hata hivyo waziri Aboud amesema kuchelewa kuyapatia ufumbuzi matatizo ya muungano likiwamo suala hilo, kunawapelekea wazanzibari kutokuwa na imani kwa vile hawafaidiki na muungano uliopo.

IDADI YA WASOMAJI

TUSIKILIZE LIVE KUPITIA TUNEIN

UNGANA NASI FACEBOOK HAPA

10 ZILIZOSOMWA ZAIDI

Labels